Jinsi kuanza kula mlo kamili na bora

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,910
6,706
Kuanza kula mlo kamili ni bora na ni kazi sana, wengi wetu tunashindwa kutokana na miundo ya Familia zetu tumezoa tukiamka asubuhi ni viporo, vitumbua nk, mchana ugali na usiku wali. Hii inatufanya tuishi kwa ajili ya kula na si kula kwa ajili ya kuishi.

Kama ungependa kuanza kula kwa ajili ya kuishi hizi ni njia chache za kukusaidia.

A nza kwa kuhesabu matokeo

– nini unapata kutokana na mlo unakula sasa? unapata matokeo chanya au hasi? wengi tunaichukia miili yetu kwa kuwa minene, vitambi na kuchukia baadhi ya maeneo ya miili yetu. Lakini haya si matokeo makubwa sana kuna yale ambayo si ya kuchekea kama

matatizo ya moyo

hatari ya kupata kansa

kunenepa kupita kiasi

kuanza kujichukia na mengineyo mengi.

Kisha fikiria faida za kula mlo kamili na bora
kupunguza nafasi ya kupata magonjwa

kujiamini

kuwa productive

kuwa na nguvu na vingine vingi vizuri


jifunze faida za vyakula mbalimbali hii itakusaidia kujua kipi kinakufaa na kipi hapana

follow accounts zinazo elimisha kuhusu vyakula bora

anzisha urafiki na watu wenye lengo moja na wewe

jifunze kupika vyakula bora kisasa ili uweze kufurahia mlo wako

Anza taratibu
Kosa kubwa ambalo watu wengi wanalifanya ni kutaka kuanza kwa ukubwa na hii si kwenye chakula tu bali hata katika maisha yetu ya kawaida, huwezi kumuachisha mlevi pombe kwa ghafla atateseka anza kwa kupunguza milo fulani taratibu kama vile punguza kula sukari na chai na anza kunywa chai na sukari, punguza kula viporo au vitumbua badala yake tafuta mikate ya brown etc. kama umezoea kula unhealthy food kwa week nzima jaribu kupunguza ziwe ziku sita au tano taratibu mpaka utakapo zoea kabisa.

Gawanya – namna rahisi ya kuacha tabia mbaya ni kuzireplace na zile nzuri, replace unhealthy food na zile healthy food
Kunywa green tea badala ya coffee

maji na fresh juice badala ya soda

mchele wa kahawia badala ya mchele mweupe

mafuta ya nazi au olive badala ya yale processed ya kupikia.

Jifunze mapishi marahisi yenye kutumia muda mchache –

jifunze mapishi rahisi ya mlo kamili hii itakusaidia kuepukana na kununua vitu vya madukani au junky food, fanya hii iwe tabia yako. unaweza kutafuta siku mbili au tatu ukapika vyakula vingi na kuvihifadhi kwenye fridge ili pale usikiapo njaa unapasha na kula badala ya kwenda kununua chips au burger

Remba sahani yako – vyakula hivi vinaweza visiwe na sura nzuri sana usoni mwako kwaio jambo jema ni kujaribu kukifanya kiwe kizuri kadri ya uwezo wako na utakavyo weza kula, ongeza taste unazo zipenda, weka vitu vya rangi rangi kama carrot, hoho za kijani, njano, nyekundu etc.
Rudia hizi tips mara kwa mara na utajikuta umezoea.
msosi.jpg


Sent from my itel A16 using JamiiForums mobile app
 
Huwa nashangaa taarifa zinazosema vijijini Wana utapiamlo. Mjini kuna utapiamlo tena Kwa watu wazima. Mjini familia za kishua wanajaza uchafu mwilini..soda, sukari, maziwa ya kopo, blue band, fortified cooking oil, fortified unga wa ngano, mayai na kuku wa kisasa, mikate, n.k Kiujumla vijijini ndo kuna mlo kamili na organic.
 
Back
Top Bottom