Umuhimu wa kufanya mazoezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umuhimu wa kufanya mazoezi

Discussion in 'JF Doctor' started by Michael Amon, Mar 30, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mwili wako uliumbwa kwa ajili ya kufanya kazi (manual labour) kama vile kusukuma, kuvuta, kubeba, kutembea, kuruka, kuimba, kucheza, kusakata rhumba, kuinama, kuinuka, kukimbia, kukusanya, kupanda (climb) kuwinda nk.


  Tunapofanya kazi yoyote kimwili ubongo huweza kutoa aina za kemikali (endocrines) ambazo hutuwezesha kuji-balance na kutupa hisia za kuwa well being.


  Unajua kuna watu wabishi inawezekana na wewe msomaji ni mmoja wao, hivi ni lini umefanya zoezi? na kwa nini hufanyi mazoezi?


  Huku unajiuliza mbona mwili unanilemea, mbona sijisikii vizuri, mbona stress kila siku? wakati mwingine tunawasumbua madaktari bure kumbe dawa zipo ni wewe kufanya mazoezi.


  Ni kweli kufanya mazoezi kutakufanya ujisikia vizuri na lazima ufanye hivyo kwa faida yako, hata hivyo wengi wetu hutumia muda mwingi kufanya kazi ambazo tunakuwa tumekaa tu kwenye kiti kwa muda mrefu bila kuufanyisha kazi mwili na ikifika weekend unashinda unatazama Tv full speed bila kujishughulisha na manual work.


  Pia ukitoka ofisi unaingia kwenye gari hadi nyumbani kama unaishi maisha ya aina hii lazima ufanye mazoezi otherwise unaweza kuharibu afya yako, kitaalamu mazoezi mara mbili kwa wiki muhimu.


  Kufanya mazoezi husaidia kupunguza uzito, kuondoa nyama zembe mwilini, kupunguza mafuta (fat), kubalance blood pressure, pia kisukari.


  Kufanya mazoezi (siyo magumu)hukuwezesha wakati wa kulala kuweza kufumba macho haraka na kuingia nchi ya ahadi ya usingizi haraka.
  Mazoezi huongeza mental skills.


  Ukiwa na afya yenye mgogoro maana yake hata mambo ya sita ka sita yataleta mgogoro hivyo basi fanya mazoezi ili uwe na afya njema na ukiwa na afaya njema maana yake better sex life.


  Mwanamke ambaye misuli ya kegel imejikaza anakuwa na wakati mzuri linapokuja suala la sex kuliko Yule ambaye misuli imelegea na huweza kuwa na misuli iliyokaza kama hufanyi mazoezi, unataka kushinda bahati nasibu wakati hukucheza, thubutu!


  Na mwanaume ambaye anafanya mazoezi ni hivyo hivyo atampeperusha kipepeo hadi anapotakiwa kufika.


  Fanya mazoezi kwa ajili ya kuweka sawa ubongo pia kujiweka social na wengine.


  E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
   
 2. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na mada yako, amini ukifanya mazoezi hutahitaji cha viagra wala supu ya pweza, hutahitaji konyagi wala value kukufanya ufanye vizuri kitandani! Piga zoezi utaona maajabu
   
 3. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,027
  Likes Received: 2,647
  Trophy Points: 280
  You are right,yaani mtu asiyefanya mazoezi jamani huwa mpaka namuonea huruma,try and feel it,ni ngumu mwanzoni kwani lazima kuna kuumwa misuli ambapo ni kitu cha kawaida sana na baada ya muda mfupi maumivu yote huisha na hutajutia kabisa kuwa mwana mazoezi.
   
 4. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Ujumbe wako umefika mkuu. Naamini ujumbe wako utawasaudia watu kubadilisha mienendo yao.
   
 5. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Usemayo ni kweli kabisa mkuu.
   
 6. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,442
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Well said mkuu. Hiyo kitu nimeithibitisha na hakika inasaidia sana. Ni ushauri mzuri na yatupasa kuuzingatia.
   
 7. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Nashukuru kwa kuliona hilo mkuu.
   
 8. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa.
  Mazoezi yana faida nyingi sana, Young Master umezifafanua kwa ufasaha kabisa.
  Well done Bro..
   
 9. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #9
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Tuheshimiane mkuu. Mimi sio dogo.
   
 10. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Poa Bro. Pamoja
   
 11. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #11
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Haina nouma.
   
 12. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Thanks, ngoja hii nimprintie mama yoyo, maana niingiapo barabarani kufanya Joging nikimkaribisha kufanya hivyo anadai "watu watatuchora"
   
 13. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Mkuu ungeongezea na upunguzaji wa pombe,mazoezi huku unakunywa pombe kuna madhara yake,ukiweza kunywa kiasi au kuacha kabisa na kufanya mazoezi ni nzuri sana kwa afya yako
   
 14. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #14
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Mimi namshauri afanye mazoezi kwa sababu yana umhimu sana si tu kwa ajili ya afya yake bali pia yamtamsaidia kujilinda mwenyewe hasa na wale waheshimiwa wanaopenda kufunua sketi za wadada bila ridhaa yao.
   
 15. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Mkuu umenena. Mimi ni shuhuda wa mazoezi. Nilikuwa na kilo zaidi ya 90, nikaanza kufanya mazoezi January hadi sasa nina kilo 76. Aisee ni mwepesi kwa kila jambo.Mazoezi yanaondoa maradhi,stress na unakuwa feet kweli kweli.
   
 16. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Nashukuru kwa kuwaelimisha kwa hlo. Mimi angalau huwa najitahdi kwa hlo. Angalau jmos,jpili,jnne na alhamisi huwa nacheza mpira.Magonjwa yenyewe yananikimbia.
   
 17. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ukosawa mkuu, hyo makitu inaumuhimu sana kwa mwili, mwanzoni nilitaka kukata tamaa wakati naanza coz mwili ulikuwa unaniuma sana, ila kwasasa nimefikia mpaka kuwafundisha wenzangu hapa chuoni...
   
 18. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ukosawa mkuu, hyo makitu inaumuhimu sana kwa mwili, mwanzoni nilitaka kukata tamaa wakati naanza coz mwili ulikuwa unaniuma sana, ila kwasasa nimefikia mpaka kuwafundisha wenzangu hapa chuoni......
   
 19. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #19
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Ulikuwa na kilo 90 mkuu? Duh! hii kali. Ila hongera sana kwa kupunguza kilo.
   
 20. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #20
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Form student to a teacher. Ha ha haaaa!!! Hongera sana mkuu. Keep it up maana ukiacha halafu ukija kuanza tena mwili utauma tena kama mwanzoni.
   
Loading...