Umuhimu wa kuanza uwekezaji mapema!

Umuhimu wa kuanza uwekezaji mapema!

Joined
Aug 26, 2022
Posts
64
Reaction score
119
Miaka miwili iliyopita, nilimshauri rafiki yangu kuwekeza kwa kununua hisa za CRDB zikiwa Tsh 400 kwa kila hisa. Leo, tumekutana tena, na akaniuliza, “Sasa hivi zimefikia shingapi?”

Nikamtazama, nikatabasamu kisha nikamwambia, “Tsh 800 kwa hisa, sawa na ongezeko la 100%... na hapo hujaweka gawio kwa kipindi hicho cha miaka miwili!”

Alibaki mdomo wazi, kisha akaguna, “Bora ningewekeza kipindi hicho!” 😯

Hii ndiyo hali ya wengi…

📌Watu wengi hupoteza fursa za uwekezaji kwa visingizio vifuatavyo:
🚫 “Sina pesa ya kutosha” – Umesahau kuwa hata kwa mtaji mdogo unaweza kuanza. Kusubiri mpaka upate mtaji mkubwa ni kujichelewesha, huku muda ukikupiga teke.

🚫 “Afadhali nikawekeze kwenye biashara” – Uwekezaji haukukatazi kufanya biashara! Badala yake, unakupa chanzo cha mapato tulivu ambacho kinaweza kukuongezea mtaji wa biashara yako baadaye.

✅ Katika uwekezaji, kuna watu wenye faida ya mtaji mkubwa, lakini pia kuna watu wenye faida ya muda—yaani, wale walioanza mapema hata kwa kidogo walichonacho.

Muda ni mali! Usisubiri miaka miwili ijayo ujikute unajuta kama rafiki yangu. Anza leo, hata kwa kidogo!

By, GODFREY DENIS
(Co-founder of Millennium Investors Community)
[0763721523]

#WekezaMapema
#MudaNiMali
 
Asante .
Vipi, no reform no election imefika hapo ulipo ?
 
Back
Top Bottom