Umri wa msichana kuolewa ni upi?

Blue Bahari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,327
1,309
Wajemeni habari zenu,
nauliza umri wa msichana/kigori wa kitanzania kuolewa ni upi?
Hapa nauliza sana sana umri kisheria wa msichana kuingia ktk ndoa. Lakini ukatanabaisha pia umri sahihi kimila na desturi zetu, au hata pia imani za kidini.
Karibuni.
 
Hivi karibuni kulikuwa na mijadala iwe 21 sina uthibitisho kama imeshapitishwa na serikali ila dabate ilikuwepo.

Sheria ya 1971 ya Ndoa inatoa ruhusa kwa ke akiwa na 14 ila kwa ruhusa ya mahakama. Uhalali ni 18 kwa 18 maana wanaooana wanatakiwa wawe watu wazima. Ila kumbuka sheria za shule zinamlinda utakaye muoa akiwa na huo umri hivyo usiingie kichwa kichwa.

Ni kama sheria ya Ajira kwa mtoto hamna. Ila Mtoto wa 14 anaweza kuajiriwa ila sio kwa kazi zote uhalali mpaka 18 . Wanasheria Watasema zaidi.
 
Wajemeni habari zenu,
nauliza umri wa msichana/kigori wa kitanzania kuolewa ni upi?
Hapa nauliza sana sana umri kisheria wa msichana kuingia ktk ndoa. Lakini si mbaya pia ukitanabaisha pia umri sahihi kimila na desturi zetu, au hata pia imani za kidini.
Karibuni.
 
Kuanzia 25 na kuendelea,
Atakuwa kamaliza elimu, utoto hamna, kwa hiyo atatulia kwenye ndoa yake.
 
Kibongo umri wa msichana kuolewa ni pale sheria ilipobainisha ukomo wa utoto. So 18+ aheria inaruhusu kuolewa.

Kimila kwa tamaduni nyingi za kiafrika binti akishavunja ungo basi huyo anafaa kuolewa.

Kidini kuna imani binti anaolewa hata akiwa na miaka 10. Japo bado anakuwa ni mtoto kwa mujibu wa sheria ya ndoa.

Labda utuambie sasa mantiki ya wewe kuuliza hili swali
 
Inamaana ukimuoa binti wa chini ya miaka 18, ni kosa kisheria?
Kisheria sio sawa, japokuwa ile sheria ya ndoa ya 1971 inasema ni ruksa kuanzia miaka 14.. Wadau na wanaharakati wa haki za wanawake wanapigania ibadilishwe (haifai na haiendani na watoto wa kizazi hiki)...Lakini mimi nijuavyo umri sahihi ni 18+ kwa maana hapo hata sheria za nchi zinatambua ni mtu mzima(mkubwa) kwa hiyo anaweza kujitegemea na akili zimekomaa..mimi ndio nijuavyo hivyo...Lakini wapo wanaooa chini ya miaka 18 sijakataa
 
Sorry, sasa sheria zinazotumika sasa ni za mwaka gani?
Je, na kama bado zinatumika hizo hizo za miaka ya 70, je , nikioa binti wa miaka 16, ntakuwa namakosa?
 
Back
Top Bottom