Umri wa kuoa ni miaka 30

mazingira anayopitia mtu ndio umkomaza kufikia maamuzi ya kuoa hasa akishapata kipato cha kutosha, kwa maana hiyo sio lazima uwe zaidi ya miaka 30, wengine wameingia chini ya 30 na maisha yanasonga vizuri kabisa....
 

Ni mpango mzuri...hivi mfano umedate na mtu akiwa na miaka chini ya hiyo unayoitaka na mkapendana haswaa,akaamua kutangaza ndoa na ukicheki anakama miaka 3 hivi ndo agote hiyo 30,utamwambia asubiri ama itakuaje hapo?
 
Ni mpango mzuri...hivi mfano umedate na mtu akiwa na miaka chini ya hiyo unayoitaka na mkapendana haswaa,akaamua kutangaza ndoa na ukicheki anakama miaka 3 hivi ndo agote hiyo 30,utamwambia asubiri ama itakuaje hapo?

Nitamwambia aubiri na nitampa sababu ya kufanya hivyo moja Wapo ni kuwa tuna mda wa kuburudika kabla ya kuingia kifungoni
 
Mi nakubaliana na wewe mkuu. Ila cha muhimu ni Ukomavu wa akili, Kujitambua ndo vitu muhimu. Na vijana wengi wanaooa wakiwa below 28 wanawasumbua sana wake zao. Mi naita wanakuwa na ndoa za uboyfriend na ugirlfriend.
 

Uzuri mmoja hilo nalo lina sabuni na maji yake... ndio maana tunanawa kila siku
 


usemayo ni kweli ila kwa life La kishenzi la bongo unakuta 18 yrs kaoa...

hata akona Dada hapa bongo wanaona 30 years wamechelewa wakati wenzao Wa ulaya ni tofauti...

Mi huwashauri Sana vijana angalau watimize 30 ndo waoe
 
Miaka 50?Makadirio ya kuishi ni miaka mingapi TZ?Unaanza kulea watoto na kiinua mgongo.Natafakari.
 
Oa ukiwa na vitu vitatu
1. Kiuchumi uko sawa kuendesha familia.
2. Kiakili uko sawa kukabili changamoto za ndoa
3. Umepata mwanamke sahihi wa kukusaidia kwenye 1 na 2

Haya yote hayategemei umri, ni tofauti ya mtu na mtu. Wengine hadi miaka 40 wanakuwa hawajafanikiwa kwenye 1 na 2, wakati wengine na miaka 20 washamaliza yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…