Biblia iliandikwa na watu tu, enzi za ujinga kabla watu hawajaaanza kugundua umri halisi wa dunia.
Hivyo ni wazi kuwa imebeba makosa yaliyotokana na ujinga wa enzi za uandishi wake.
Kila anayejua kufikiri ataona hilo, hata kama imani itamtaka alifumbie macho.
Sasa kama biblia imeandikwa na watu bila révélation ya mungu,kwa nini ifufue misukule?
Inafufuaje misukule?
Na kwa nini kinachoandikwa na watu kisiwe na uwezo wa kufufua walio katika hali tata?
Wahindi, Wachina na Wamisri wamefanya yote hayo kabla biblia haijaandikwa, biblia itakuwaje chanzo cha hayo?
Hakuna mtu aliefufua watu,isipokuwa watumishi Wa mungu
Hujathibitisha kwamba mungu yupo.
Your argument is circular.
In latin they call that "circulus in probando".
Nakuuliza uthibitishe kwamba mungu yupo, unaniambia mungu yupo kwa sababu watumishi wake wanafufua watu.
Ukishaenda kwenye kusema "watumishi wake" usharuka hatua ya kunionyesha kwamba yupo.
Unajuaje kwamba hao wanaofufua watu ni watumishi wa shetani na si wa mungu? Au hawafufui watu, wanawazindua tu kutoka near death experiences?
Latin ndo lugha ya wakatoliki ,na huko wanajua mungu anafufua,lakini mungu hatumuamini kwa kufufua kwanza Bali kwa uumbaji unaotuzunguka ulio programmed. Lakini injili inatushirikisha nguvu ya uumbaji tukitenda katika imani,hapo tunakuja kuelewa kumbe kweli vinavyoonekana viliumbwa na vitu visivyo dhahiri,ndio njia pekee ya kuprove. Hebrews 11:1-3
...by faith we understand...
Not by facts
Na Mungu alitokea wapi?,kuna uhusiano wa mawingu na mbingu?,mbinguni ni wapi?,vipi kuhusu Mars,Neptune,Pluto ,Jupiter ziliumbwa kabla au baada ya dunia na kwenye maandiko yapi?
Kama mungu ni muweza yote na ana upendo wote kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekanika?
Mungu hakutaka kutufuga kama bata,aliumba watu wenye utashi ili awe na wilfull communion. Ata wewe ungependa mwanamke aliyekupenda kati ya wanaume,kuliko yule anaekufuata kwa kuwa umempiga limbwata
Mungu hakuweza kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya na binadamu anatumia utashi wake kuchagua mazuri tu?
Aliweza au hakuweza?
mabaya yanaweza kuwa machoni pako ila kwa mungu sio mabaya
kwa kuwa kuba watu wanafurahia vifo vya watu wengine wanachukia
iweje wewe na mungu muwe na mtazamo mmoja ??
Kama angefurahishwa na hilo,asingeumba binadamu Bali angebaki na wanyama tu wakaishi bila shida. Lakini alitaka kuumba Wa kufanana nae,apambane na matatizo na kuyatawala kama yéyé. Pia shetani alianguka huku kwa kujiinua,na mungu hawezi kupigana na shetani ni kujishushia hadhi Bali aliumba wanadamu wasio na uwezo Bali wamuaminio mungu asiyeonekana ata wakamuadhibu shetani,hii itamuuma zaidi kwa sababu shetani alishawahi kuishi mbinguni
Kama si mabaya sasa kwa nini mungu anataka kuadhibu watu kwa kutenda dhambi?
dhambi ni nini ?
Niambie wewe unayeamini kuwapo kwa mungu anayeadhibu watu kwa dhambi.
Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo
kwa nini unaongelea kitu ambacho hujui ?