Umri sahihi wa kumfundisha mtoto

Umri sahihi wa kumfundisha mtoto

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Ni umri gani sahihi kuanza kumfundisha mtoto kufua nguo ya ndani na socks? Pamoja na kuosha sahani aliyotumia?
 
mimi nakumbuka wakati nipo darasa na kwanza ndio nilifundishwa hizi vitu, mpaka leo hii nina familia, na siku nikiwa home wife na madogo huwa ni wenye furaha tele maana nawasaidia kazi nyingi tuu...kuhusu watoto mmoja ana miaka minne tayar anafua soksi zake na vyombo humsaidia mama yake kuosha na kupanga japo sio kiviile kama mtu mzima, anafagia na deki anapiga....tena ni wakiume aisee....
 
mfundishe kwanza kuweka vitu katika mahali sahihi. then taratibu ndo atakuja kufundishwa kufua na kupasi. ila kuanzia miaka mitatu si mbaya
 
Nilianza kufua pichu na socks nikiwa na miaka saba kumbe mother alichelewa kidogo
 
Nokia za kufua pichu na socks nikiwa na miaka saba kumbe mother alichelewa kidogo
wala hakuchelewa. unaweza ukakuta ukiwa na miaka mitano alikuwa anakupa usuuze nguo za ndani alizofua za kwako then taratibu anakwambia fua. then ukaachiwa jaramba la kujifulia ukiwa na miaka saba rasmi.
 
Ni muhimu kuwafundisha wote wa kike na wa kiume. Miaka kumi wawe wanajua kubadilisha shuka kitandani na kufua nguo zao angalao kusafisha chumba anacholala ifikapo weekend
 
Kuanzia miaka mitano mtt--kike na kiume--anaanza kua physically strong. Hivyo anapewa kazi ndogo ndogo. Mathalan akiwa na 4 yrs huyo anatembea. Hivyo anaweza kutoa sahan aliyolia na kuibeba. 5 yrs anaanza kusuuza kidogo kidogo vyombo vilivyooshwa. Miaka 7 nadhan nguo ni anaanza kifua like underwears. By 10 yrs mtt ni lazima ajue kufua na kuosha vyombo pia kufagia chumba chake

sent live and direct from KOROMIJE
 
Ni umri gani sahihi kuanza kumfundisha mtoto kufua nguo ya ndani na socks? Pamoja na kuosha sahani aliyotumia?
Angalia kwanza mtoto mwenyewe learning ability yake ikoje kuna wengine wana speed miaka 3 tu analilia akusaidie kufua, kuosha vyombo, deki nk. We mpe afanye taaaratibu ndo kujifunza kwenyewe hata akiwa anafikicha tu kwa hatua za mwanzo baaye atajifunza, kiufupi mpe mtoto mazingira ya kujaribu kufanya kila linapowezekana
 
Malezi bora ya mtoto yanafanyika kipindi cha miaka 0 hadi miaka 6.Kama unataka mwanao awe na tabia njema na ajue kujituma na awe mfanyakazi bora inatakiwa ayo mambo umfundishe ndani ya huo muda.kipindi hichi ndo kipindi mtoto anajifunza kila kitu toka umbali sifuri kwa maana wale watu wakaribu hadi wambali maana ndo kipindi anachoonyesha tabia yake yakuzaliwa(inborn behavior).kwaiyo hapo nirahisi kumfundisha chochote na akadumu nacho hadi uzee.Jinsi tulivyo sasa ndivyo jinsi ulivyokua kipindi tuko na umri chini ya miaka 6.Tunachokuja kukiongeza tukishavuka miaka 6 ni tabia ambazo ni intellectual zaidi.
 
Nilianza kujifunza kaz na miaka 6, Nilianza shule umri huo kipind hicho nilikuwa nafua Sox, na nguo za ndani, kutumwa tumwa dukan, kujichotea maji ya kuoga Kwenye kidumu, kuosha vyombo ninavyotumia Mwenyewe.

Nilipofika darasa la pili nikaanza kufua uniform zote na siku moja moja nguo za kushindia.

Hapo makonzi, vifinyo na mabao Kutoka kwa mama yalikuwa hayachezi Mbali akute nguo haijatakata nilikuwa naifua kwa kilio.

Darasa la nne hapa kazi zikazidi nikawa sifuliwi kabisaa, kabla ya kwenda shule asubuhi Lazima nisaidie hom kaz mojawapo, kupika , kuosha vyombo, kudeki

Duh namaliza la Saba Niko vizur hata kwa kuolewa nilikuwa Safi kila idara

Ashukuriwe mama maana kuna mabinti utawaonea huruma hawajui kitu Chochote.

Wamama msidekeze Watoto wa kike atasipoolewa mwanamke kutambua majukumu yake ya ndani ni raha Sana.
 
Kwa wale wavivu unadhani ni njia nzuri kutumia vijizawadi na kuwa pongeza wanapo shiriki kazi ili kuwapa motisha?
 
Nilianza kufua pichu na socks nikiwa na miaka saba kumbe mother alichelewa kidogo
Mkuu miaka minne ndio sahihi. Nina my son wa 4 yrs hataki kutawazwa na dada wa kazi hata na mama ake. Labda mimi anakubali nimhudumie tena kwa kumwagilia maji tu ajisafishe mwenyewe, anafua chupi mwenyewe na inatakata vizuri ila maji ndoo nzima ya lita 10 inaisha. Anasafisha choo vizuri kwa dawa akimaliza kupata huduma. Hakufundishwa wala kulazimishwa alianza mwenyewe kugoma kuhudumiwa na housegirl mgeni.
 
Back
Top Bottom