Umri gani wa kupishana kati ya watoto?

doooh...hapo gap kubwa sana!Mi napendelea 3 years...wanakua pamoja, sio wapishane sana mpaka hata hawawezi kucheza pamoja!!!Ni mtazamo tu..
Mi ningependa kupishanisha one year.., vp inakaaje wakuu?
 
A scientific answer can be obtained from taasisi ya LISHE, Tanzania (Tanzania Food and Nutrition Centre) among other authorities
 
HII HAINA FOMULA,KILA MTU ANA MTAZAMO WAKE NA WENGINE WANAPATA MIBA KWA BAHATI MBAYA ILHALI WENGINE WANATAFUTA MIMBA KWA MIAKA KADHAA

inategemea
 
kwa kweli wangu ana mwaka mmoja na miezi nane na wife ana ujauzito miezi tisa and naona iko pouwa tu
 

Raha gani unayokula mkuu embu tuambie hapo!!!!
 
Watoto wakipishana sana kuna athari kimalezi. Mtoto anayepata mdogo wake after say 5 years ni sawa na mtoto aliyezaliwa peke yake. Anakuwa spoiled kind of, na anaweza kumchukia mdogo wake. Kwa hiyo nakubaliana na wanaosema watoto wanatakiwa wasipishane sana ili wawe wanacheza pamoja na kujifunza ku share. Nimeshaona design zote mbili (waliopishana sana na waliokaribiana) na nadhani ni vizuri watoto wasipishane sana. Faida nyingine ni kumaliza biashara ya kuzaa na kuanza ku enjoy life. It is real hard kwa mama kufikiri kuzaa baada ya muda mrefu kupita. Kuzaa ni kazi bora mtu umalize maisha mengine yaendelee, including career development.
 
Very good comment mkuu.
 
Hivi kuna watu bado wanafikiria kuwa na 'timu ya mpira' katika karne hii!
 
Watoto wakipishana sana kuna athari kimalezi. Mtoto anayepata mdogo wake after say 5 years ni sawa na mtoto aliyezaliwa peke yake. Anakuwa spoiled kind of, na anaweza kumchukia mdogo wake.
nafikiri inategemea na huyo mtoto aliyetangulia alikuwa anapewa malezi ya vipi. Mdogo wangu anayenifatia tumepishana zaidi ya miaka kumi na ninampenda sana tena sana.
 
It as if mnamwingilia Mungu..........okey mie nitapishananisha miaka 10 ili akikua anisaidie kulea mwenzie..............lakini ni lazima kuwa na watoto zaidi ya 1?
 
Mimi naona inategemea sana na umri wa mama wakati unamuoa na mnapenda kuwa na watoto wangapi, hivi mfano unamuoa mwanamke ana miaka 34 na mwanaume ana miaka 36 mtazaa kwa mapngilio gani hapo, so ina depend na umri wa mama zaidi, lakini ni jambo linalopaswa kuzungumzwa na wote wawili mke na mume
 
nafikiri inategemea na huyo mtoto aliyetangulia alikuwa anapewa malezi ya vipi. Mdogo wangu anayenifatia tumepishana zaidi ya miaka kumi na ninampenda sana tena sana.

10 yrs Husninyo?Si kawaida!!
 
Kama bado hujaingia kwenye ndoa, haya ni mambo ya kujadiliana na mwenzako na kufikia uamuzi wa pamoja kabla, na maamuzi yanategemea mambo mengi: Umri wenu, idadi ya watoto mliokubaliana nk. Na mnapoamua mfano mtakuwa na wawili tu, wengi wangependa wawe wa jinsia 2 tofauti, so ni vema kuwekana sawa na kuwa tayari kupokea matokeo yoyote! Vinginevyo mtajikuta mnaunda timu ya watoto kwa kutafuta mtoto wa jinsia tofauti na mliyopata kama wawili wa kwanza watakuwa wa jinsia moja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…