Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Uongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM umeripotiwa kumuunga mkono Raisi wa Umoja wa Vijana wa ANC, Julius Malema, ambaye kamati ya nidhamu ya ANC hivi karibuni inasemakana ilimfukuza unachama wa ANC na kumvua uraisi wa Umoja wa Vijana wa ANC katika kile kinachoonekana ni kudhibiti nguvu ya Malema ya kufanya kampeni za kutounga mkono nia ya raisi wa Afrika Kusini Jacob Zuma kuongoza nchi kwa awamu ya pili.
Taarifa kutoka gazeti la Sunday Independent la Afrika ya Kusini limenukuu sms iliyotumwa na Beno Malisa, raisi wa Umoja wa Vijana wa CCM yenye maneno yafuatayo, "Comrade, we wish you well, aluta continua. Think of paying a visit to Tanzania with my invitation brother, u have our full support. Young people here they sing your name".
Kinachofurahisha hapa ni kwamba JK na Zuma wana urafiki wa karibu, na bila shaka urafiki huu wa Umoja wa Vijana wa CCM kwa Julius Malema hautamfurahisha raisi Jacob Zuma, ambaye si ajabu akamuuliza swahiba wake JK, "kulikoni na vijana wako mkuu?".