Umoja wa nchi unavunjwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umoja wa nchi unavunjwa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by haki na usawa, May 1, 2012.

 1. h

  haki na usawa JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 476
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jamani kama kiongozi anasamehe wezi wakubwa je ni haki? Nani anavunja umoja wetu? Maana hakuna haki kati ya masikini/fukara na Tajiri
  Maana wezi wakubwa hata TAKUKURU haina uwezo nao ila wanyonge wanakamatwa na kuwekwa ndani na kufukuzwa kazi/kusimamishwa kazi lakini wezi wakubwa wanatamba mtaani na hakuna wa wakuwagusa!
  Usalama wa Taifa nao hauna uwezo wa kuwashughulikia wezi hawa wakubwa na ukiangalia kwa DPP ndo kabisaa hata faili likifika halishughulikiwi maana wezi hawa ni hatari kama kiongozi mkuu anawaomba warudishe fedha kwa hiari ujue ni hatari hata kwake japo yeye ana Jeshi na Walinzi wa usalama kibao je DPP kwanini asifiche faili?
  Je nani anavunja UMOJA NA MSHIKAMANO wetu?
  Kama hakuna USAWA na HAKI usitegemee Umoja uwepo maana wenye shida wataungana na wenye raha wataungana je kuna Umoja?
   
Loading...