Umoja wa Mataifa: Ulimwengu umeshindwa kulinda Watoto

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa siku ya Jumatano, inasema ulimwengu umeshindwa kumlinda mtoto na hatari za kiafya zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na lishe hafifu.

Ripoti hiyo iliyopewa kichwa cha habari 'Hatma ya watoto ulimwenguni'imetolewa na timu ya wataalamu zaidi ya 40 waliokusanywa na shirika la afya duniani (WHO), shirika la kuwahudumia watoto (UNICEF) na jarida la masuala ya afya la Lancet.

Kulingana na ripoti hiyo hakuna hata nchi moja duniani ambayo inakilinda kizazi kijacho kutokana na athari za uzalishaji wa gesi ya kaboni, uharibifu wa asili na ulaji wa vyakula vilivyosindikwa.

WHO inaamini kuwa zaidi ya theluthi tatu ya vifo vya sasa vinatokana na athari za mazingira kwa watoto,na uchafuzi wa hewa ambapo mtoto mmoja kati ya 10 havuti hewa safi.
 
Back
Top Bottom