Umoja wa maendeleo wa kata

Mpendwa_Ellie

Member
Jul 8, 2012
6
1
Umoja wa Maendeleo

Nahitaji anzisha Chama cha kijamii katika Kata yangu ambacho hakitakuwa na itikadi yoyote ya kisiasa, jinsia wala rangi ni kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo katika kata yetu. Tatizo nililonalo ni kuwa sijui taratibu za kuzifuata ili kuanzisha huo Umoja wa Maendeleo ya Kata. Naomba kwa yoyote mwenye ufahamu wa jinsi ya kuanzisha na kuendesha Umoja wa maendeleo wa Kata anipe darasa. Thanx in advance.​


 
Uko wapi?
Unachohitaji ni muhtasari wa kikao cha kukubaliana kuanzisha umoja na kuipitisha katiba.
Kuna options mbili: 1. kusajiri wilayani 2. kusajiri wizarani. Kama uko Dar es salaam nakushauri usajiri wizarani kwa sababu later unaweza kutanua shughuli kitaifa.
1. Wilayani - nendo ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya kwa maelezo zaidi.
2. Wizarani - nendo wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto kitengo cha NGOs kwa taratibu.

Ipo pia option ya kusajiri wizara ya mambo ya ndani au BRELA, lakini kwa jinsi ulivyotarget kata options hizi zitakusumbua tu.
 
Back
Top Bottom