Elli
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 55,609
- 86,300
Wana Jamvi,
Kuna hii tabia ya madereva wa pikipiki almaarufu kama Bodaboda ambao hutumika au hufanyakazi pale mmoja wao anapopata tatizo. Japo sina tatizo na umoja wao huo kutokana na matukio ya kikatili wanayofanyiwa na waporaji wa pikipiki zao lakini kwa bahati mbaya sasa umoja huu hufanya vurugu, hupiga huumiza na pengine kuua kwa kisingizio kuwa mmoja wao amegongwa, hata kama aliyegongwa alifanya makosa yeye.
Nimeshashuhudia pale Sinza Mori mmoja wao aligongwa na wakapiagiana simu, wakafika vijana wengi sana na pikipiki zao wakaanzisha vurugu, kule tegeta imesharipotiwa pia ambapo walifanya vurugu na kusababisha gari kuchomwa moto, Ubungo vivyo hivyo na juzi niliwakuta pale maeneo ya manzese-bgi brother. Yawezekana kuna matukio mengi zaidi ya haya pia
Angalizo langu; vijana hawa wapatiwe elimu sahihi ya udereva vinginevyo watakuja kusababisha tatizo kubwa zaidi la umwagaji damu kwa watu ambao hawana tatizo.