Umoja Huu wa Madereva wa Pikipiki ni Hatari

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,502
86,050
Wana Jamvi,
Kuna hii tabia ya madereva wa pikipiki almaarufu kama Bodaboda ambao hutumika au hufanyakazi pale mmoja wao anapopata tatizo. Japo sina tatizo na umoja wao huo kutokana na matukio ya kikatili wanayofanyiwa na waporaji wa pikipiki zao lakini kwa bahati mbaya sasa umoja huu hufanya vurugu, hupiga huumiza na pengine kuua kwa kisingizio kuwa mmoja wao amegongwa, hata kama aliyegongwa alifanya makosa yeye.
Nimeshashuhudia pale Sinza Mori mmoja wao aligongwa na wakapiagiana simu, wakafika vijana wengi sana na pikipiki zao wakaanzisha vurugu, kule tegeta imesharipotiwa pia ambapo walifanya vurugu na kusababisha gari kuchomwa moto, Ubungo vivyo hivyo na juzi niliwakuta pale maeneo ya manzese-bgi brother. Yawezekana kuna matukio mengi zaidi ya haya pia

Angalizo langu; vijana hawa wapatiwe elimu sahihi ya udereva vinginevyo watakuja kusababisha tatizo kubwa zaidi la umwagaji damu kwa watu ambao hawana tatizo.
 
mkuu hawa jamaa ni noma sana! na wengi wao wanafanya kazi za wizi usiku wamanane, kule bunju wao ndo hutumika kubeba nyama za ng`ombe walioibiwa! hiyo kufanya vurugu kwenye matukio ni style yao ya kutimiza uhalifu wao tu hamna kingine coz wao ndio wenye makosa kwa asilimia nyingi sana kwenye ajali wanazohusika. ukigonga muendesha pikipiki we sepa tu mpaka kituo cha polisi, ndo utakuwa salama.
 
Na nyinyi wenye magari kwa nini muwagonge waendesha pikipiki? Kisa hajui sheria tu? Adhabu yake agongwe/ auwawe? Ninyi wenye magari na munaozijua sheria za barabarani basi ongezeni uangalifu mnapokuwa kwenye vyombo vyenu vya moto mkijua kwamba mwendesha pikipiki yeye mwenyewe ni bodi. Ukimgonga unamuua au unampa kilema cha maisha akipona. Kukosea kwao sheria siyo kibali cha ninyi kuwakanyaga. Bado mwaweza kuepusha shari kama mtakuwa waangalifu. Nje ya hapo mtawaua wengi.
 
Hawa jamaa ni kweli hawazingatii sheria za barabarani. Hapa jambo la muhimu ni kutolewa elimu ya usalama barabarani kwa hawa jamaa.
 
Mpwa, sijasema wala hakuna aliyesema kwamba kwakua hawajui sheria basi wagongwe, hebu soma mara mbili kabla ya kupost, point niliyokuwa nasisitiza ni kwamba hawa jamaa zetu hawana na wala hawajui sheria na hivyo mamlaka husika wawasaidie shule kidogo....
Na nyinyi wenye magari kwa nini muwagonge waendesha pikipiki? Kisa hajui sheria tu? Adhabu yake agongwe/ auwawe? Ninyi wenye magari na munaozijua sheria za barabarani basi ongezeni uangalifu mnapokuwa kwenye vyombo vyenu vya moto mkijua kwamba mwendesha pikipiki yeye mwenyewe ni bodi. Ukimgonga unamuua au unampa kilema cha maisha akipona. Kukosea kwao sheria siyo kibali cha ninyi kuwakanyaga. Bado mwaweza kuepusha shari kama mtakuwa waangalifu. Nje ya hapo mtawaua wengi.
 
Wengi wa bodaboda walikuwa wezi mitaani hivyo akili zao ndo hizo hizo.
(kunguru hafugiki)
 
Kuna siku jamaa wa bodaboda alijibamiza kwenye gari yangu na pikipiki yake ikaanguka na kuvunjika side mirrors. Niliposhuka kuangalia iwapo ameharibu gari yangu (bahati nzuri alijibamiza kwenye ngao), nikajikuta nimezungukwa na pikipiki kibao huku wakijaribu kunitisha. Nikawaambia wamuulize mwenzao iwapo nimemgonga au amejibamiza mwenyewe. Waliponisogelea zaidi kwa shari nilichomoa 'mguu wa kuku' kiunoni, wakatawanyika, nami nikawasha gari yangu na kuondoka. Kama alivyodokeza mkuu mwingine hapo juu, mara nyingi hawajali kama wao ndio wenye makosa au la. Sasa hivi hizi bodaboda ni chanzo kimojawapo cha ajali za barabarani. Vijana wengi wanajifunza kuendesha asubuhi na jioni wanabeba abiria. Wengi wao hawajui kabisa sheria za barabaranii.
 
  • Thanks
Reactions: len
moroco jana wamechoma BMW
Arusha hii pia ilitokea.
Mwanamke alikuwa anafundishwa gari jipya (PRADO) na mumewe eneo la SAKINA, na kwa bahati mbaya akamgonga mwendesha bodaboda, na kumuumiza...kilichofuatia pale ni kuwa bodaboda waliitana kutoka vijiwe vyote na kujazana mahali hapo, na mara wakaafikiana kulichoma prado hilo, na liliteketea hadi jivu!
Hawafai hawa watu, usiombe upate nao kadhia barabarani, hasa kama wewe una gari!
 
legelege,hovyohovyo,vululuvululu, yaani ni kama kambale ndevu kwenda mbele.
unategemea nini hapo?
 
Kuna siku jamaa wa bodaboda alijibamiza kwenye gari yangu na pikipiki yake ikaanguka na kuvunjika side mirrors. Niliposhuka kuangalia iwapo ameharibu gari yangu (bahati nzuri alijibamiza kwenye ngao), nikajikuta nimezungukwa na pikipiki kibao huku wakijaribu kunitisha. Nikawaambia wamuulize mwenzao iwapo nimemgonga au amejibamiza mwenyewe. Waliponisogelea zaidi kwa shari nilichomoa 'mguu wa kuku' kiunoni, wakatawanyika, nami nikawasha gari yangu na kuondoka. Kama alivyodokeza mkuu mwingine hapo juu, mara nyingi hawajali kama wao ndio wenye makosa au la. Sasa hivi hizi bodaboda ni chanzo kimojawapo cha ajali za barabarani. Vijana wengi wanajifunza kuendesha asubuhi na jioni wanabeba abiria. Wengi wao hawajui kabisa sheria za barabaranii.

Pole sana mkuu, hata mimi yameshanikuta hayo. Jamaa amejimamiza mwenyewe halafu anakuona wewe ndio umemgonga. Ni vile mimii niliwaonea huruma jinsi walivyoanguka maana alikuwa na abiria, nikawaomba niwawaishe hospital, yule abiria akaingia kwenye gari yangu tukapatana jamaa wa pikipiki atufuate nyuma. tulipofika mbali kidogo yule abiria akadai nimpe tu hela ataenda kujitibu mwenyewe, nikampa elfu 40, tukapeana na namba za simu ili kujuliana hali baadae, Yule mwenye pikipiki akawa amepotea gafla hatumuoni, tukaachana naye, baadae yule abiria anasema eti mwenye pikipiki amekutana naye na eti kumbe alienda polisi, kwahiyo anaomba tukutane tena. Nikajua hapa kuna mchezo nataka kuchezewa, walivyoendelea kunisumbusumbua nikaamua kuzima simu. sasa sijui ndio alikuwa ameenda kuwaita wenzake ili waje wanifanyie fujo hapo sijui. Ila ni kweli kabisa hawa jamaa sasa wamekuwa tishio.
 
Kuna siku jamaa wa bodaboda alijibamiza kwenye gari yangu na pikipiki yake ikaanguka na kuvunjika side mirrors. Niliposhuka kuangalia iwapo ameharibu gari yangu (bahati nzuri alijibamiza kwenye ngao), nikajikuta nimezungukwa na pikipiki kibao huku wakijaribu kunitisha. Nikawaambia wamuulize mwenzao iwapo nimemgonga au amejibamiza mwenyewe. Waliponisogelea zaidi kwa shari nilichomoa 'mguu wa kuku' kiunoni, wakatawanyika, nami nikawasha gari yangu na kuondoka. Kama alivyodokeza mkuu mwingine hapo juu, mara nyingi hawajali kama wao ndio wenye makosa au la. Sasa hivi hizi bodaboda ni chanzo kimojawapo cha ajali za barabarani. Vijana wengi wanajifunza kuendesha asubuhi na jioni wanabeba abiria. Wengi wao hawajui kabisa sheria za barabaranii.

Sasa sio wote tunaweza ku access hiyo kitu mkuu, then wengine tuna hasira kama za marehemu Dito...unaweza kuta ushatawanya ubongo wa mtu ikawa sooo...hamna approach nyingine nzuri ya kukomesha hii tabia ya vijana hawa?
 
Yaaaanii nashindwa hata kuelezea sijui tufanye nini, naona bora usafiri wa bodaboda upigwe marufuku mara moja maana hili limeshakuwa tatizo! afadhali hata jamaa wa bajaj
 
Tutakuja au watakuja kushtuka jamaa wanachoma gari la IKULU au Ambulance au magari ya Fire, sie tupo, lakini kama hakutakua na hatua madhubuti hawa vijana watafanya maasi mengi sana kwa kisingizio cha umoja...
Yaaaanii nashindwa hata kuelezea sijui tufanye nini, naona bora usafiri wa bodaboda upigwe marufuku mara moja maana hili limeshakuwa tatizo! afadhali hata jamaa wa bajaj
 
ni makada wa CCM

wapanda+pikipiki+wakisindikiza+msafara+wa+JK+alipokuwa+anaingia+uwanja+wa+Majimaji+leo+(5).jpg
 
Hakuna alievaa kofia ngumu (helmet) hata mmoja, na hakuna aliyechukuliwa hatua, sasa nashangaa kuona hizi sheria za barabari kwanini zinakuwa za msimu na wakakyi fulani tu?? Pumbafu kabisa
 
Back
Top Bottom