Umoja Huu wa Madereva wa Pikipiki ni Hatari

Hawa jamaa wapigwe marufuku hasa kwenye maeneo ya katikati ya mji na wamekuwa wasumbufu sana kwa waendesha magari. Mimi nilishawai kugongwa na mwendesha piki piki akavunja side mirror yangu na kukwangua rangi. Yeye alianguka, baadae kidogo wakati nafungua mlango jamaa akapanda kwenye piki piki na kutimua mbiyo. Huyo kijana singeweza kumkimbiza nikabaki kusikitika nikaenda kutengeneza gari. Barabara zetu zote za mjini hazina sehemu ilyotengwa ya waendesha baisikeli, boda boda au mkokoteni. Iweje wapewe ruksa au leseni ya kufanya biashara na Kwa sheria ipi? Haya ni matunda ya wasomi wetu walioweka shahada zao ukutani wakijisifia wamesoma.
Nchi nyingi zilizoendelea zina sehemu maalum za kuendeshea baiskeli. Kwenye pikipiki hapo nina wasiwasi. Ktk nchi nyingi pikipiki zinachanganyika na magari. Na wote wanaheshimiana siyo kama hapa kwetu ambapo mwenye gari hamjali wala hamuoni mwenye pikipiki akidhani barabara ni yake peke yake. Na ndo maana maajali yanakuwa mengi. Lakini wazee wa bodaboda wamegundua kwamba wanaonewa kwa kuminywa sasa wameamua kuwa na umoja na kulipa kisasi kwa kuwachoma moto wenye magari. Bila hiyo dharau ya wenye magari nadhani waendesha bodaboda wasingefikia hatu hiyo. Na wametambua kwamba wakimpeleka mwenye VX polisi atatoka tu kwani pesa iko, yaani hakutakuwa na haki. Kwa hiyo ni bora kumalizana naye hapohapo barabarani.
Kwa mtazamo wangu waendesha magari na bodaboda wanahitaji kozi ya udereva. Kwa kadiri nionavyo makundi yote mawili hayajui sheria za barabarani. Ukweli ndiyo huyo! Tusiwalaumu wenye bodaboda peke yake.
Mimi ninayendika hapa huwa nachukia sana ninapojikuta kwenye zebra ambapo ni haki yangu kupita tena kwa mwendo wa kawaida bila wasiwasi lakini inanibidi nisubiri wenye magari wapite kwanza na nipige mahesabu vizuri ili kuvuka barabara kwa kasi (kwa kukimbia) kabla gari jingine halijafika pale. Nalazimika kufanya hivi kwa vile waendesha magari hawana habari na haki ya mtembea miguu, na wala hawapunguzi mwendo, ukizubaa eti una haki ya kuvuka barabara kwa vile ni zebra wanakukata kiuno. Je, hiyo ndo ethics ya driving?
 
Naona ndio wamepigwa BAN ya kwenda mjini posta, sijui itafanya kazi kweli hata sijui kwa kweli
 
Msinidai ushahidi, naskia wale bodaboda waliochoma moto daladala pale makonde wanapukutika mmoja baada ya mwingine
 
duh, itakua ile daladala ya mtu wa Tanga au Mzaramo tu au sijui wapi kule
Msinidai ushahidi, naskia wale bodaboda waliochoma moto daladala pale makonde wanapukutika mmoja baada ya mwingine
 
duh, itakua ile daladala ya mtu wa Tanga au Mzaramo tu au sijui wapi kule
Imani za kishirikia zimechukua nafasi yake dini za waafrica... Mtu chombo chake cha kujitafutia mlo wake unachoma moto wakati hujui kosa ni la nani una hukumu tu wacha kiwapate cha mtema kuni...

Polisi wanawatafutia dawa yao Kuna kamanda jana anasema taarifa hizi wanazo za umoja wa waendesha pikipiki kujichukulia sheria mkononi
 
Back
Top Bottom