Ummy Mwalimu aitetea Serikali kuhusu Lissu

Ummy Mwalimu aitetea Serikali kuhusu Lissu

Status
Not open for further replies.

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,302
Waziri Ummy Mwalimu amejibu tuhumu zinazotolewa na baadhi ya watu dhidi ya serikali baada ya kutaka kuombwa kugharamia matibabu ya Lissu, na kusema kwamba serikali imelazimika kufanya hivyo kwa sababu mgonjwa alijitoa kwenye utaratibu wa serikali.


Waziri-Ummy-Mwalimu.jpg

Ummy Mwalimu ambaye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ametoa maelezo hayo leo kwenye ukurasa wake wa twitter, na kusema kwamba serikali isingeweza kuingilia kati bila kuombwa na familia ya Tundu Lissu, kwani mgonjwa alishatolewa kwenye utaratibu wa serikali kwa kupelekwa Nairobi, na hiyo sio mara ya kwanza kwa serikali kufanya hivyo.

"Mgonjwa alitolewa kwenye utaratibu wa serikali alipopelekwa Nairobi, sasa gharama/tiba zaid yahitajika, serikali inaingiaje bila ridhaa ya familia? Na hii sio mara ya 1 kutokea. Mzee wetu S.Sitta (RIP), alikwenda matibabu London kwa utaratibu binafsi kisha alileta maombi serikali ishiriki", ameandika Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Mwalimu ameendelea kwa kuandika akisema kwamba mgonjwa ni Mbunge anayehitaji matibabu zaidi, lakini kwa kuwa sasa hivi yupo nje ya utaratibu wa serikali, ili serikali iweze kushiriki ni lazima yawepo maombi ya kufanya hivyo.

hapo juzi serikali ilitoa tamko ikisema kwamba watakubali kusimamia matibabu ya Tundu Lissu popote duniani iwapo familia yake itaomba kufanya hivyo, na sio vinginevyo, kitendo ambacho kimeibua sintofahamu nyingi kwa baadhi ya wananchi wakiilaumu serikali kwa kutojali matatizo ya Tundu Lissu.



Luwi-Capello-in-a-OVO-cap.jpg

Alichokiandika Waziri Ummy Mwalimu kwenye twitter.
 
Vema serikali iingie katikz kulipia gharama, kama ni kawaida yso kufanya hivyo inapoombwa na familia. Japo desturi
ikiendekezwa, basi iwe kwa wote sio political heavyweights tu. Kupigisha watu magoti kazi
 
Familia ndiyo imempeleka Lissu Nairobi??

why leo baada ya siku 15??

akae tu kimya huyu mama, juzi akiwa Tanga eti anajifanya anashangaa kwanini michango inachangishwa wakati serikali ina uwezo, Yani amekaa kisiasa na anadhani watanzania ni wajinga kuwa hawaoni kinachoendelea.
 
Ni sawa kabisa utaratibu huu upo hata kwa watumishi wengine usipofuata mfumo Wa serikali ujigharamie hata awe rais. Mabadiriko hayawezi kuanza kwa lissu lazima utaratibu ufuatwe huku tukizingatia kubana matumizi
 
Ni sawa kabisa utaratibu huu upo hata kwa watumishi wengine usipofuata mfumo Wa serikali ujigharamie hata awe rais. Mabadiriko hayawezi kuanza kwa lissu lazima utaratibu ufuatwe huku tukizingatia kubana matumizi

Kwa utaratibu huu mgonjwa hujiandikia barua ya maombi au huandikiwa na mtu?
 
Kwa nini mnataka kujibu kila kitu?
Risasi 30+ na hakuna aliyekamatwa mpaka leo.Vidole vinaelekezwa kwa vyombo vya dola bado mnatoka na kutoa ufafanuzi kila kukicha.
Tupeni update ya upelelelezi mgonjwa ni "critical lakini stable!!!
 
Sasa kama hiyo serikali imeona ni muhimu wanafamilia kuomba msaada alikuwa na maana gani kuelezea umma? Ange wafuata familia awaeleze utaratibu. Kwani walipo mtibu huyo Sitta walitangazia umma?

Wasituletee mambo ya aibu hapa. Tutachanga mia, mia tano ,elfu, kamanda ataeudi road.
 
Sasa kama hiyo serikali imeona ni muhimu wanafamilia kuomba msaada alikuwa na maana gani kuelezea umma? Ange wafuata familia awaeleze utaratibu. Kwani walipo mtibu huyo Sitta walitangazia umma?
Wasituletee mambo ya aibu hapa.
Tutachanga mia, mia tano ,elfu, kamanda atarudi road.
 
wakuu hapo juu wote mnaongea kwa hasira, uchungu na gubu. Ila ndio iko hivyo. ni serikali hiyo ni dudu kubwa ambalo halina aibu lina system a procedures. hauzifuati wala haikuangalii
 
Tangu awali hawa watu walionyesha nia ya kutoshirikiana na nyie. Hili suala waachieni wenyewe wanajua watamtibua vipi mgonjwa wao, kwa nini mnawalazimisha? Magufuli na watu wako mnajitengezea matatizo wenyewe, mna nia njema. Lakini hawa watu hawana nia njema na nyie.
 
Kwan mwanajeshi akiwa vitani huwa mnasubiri familia iwaombe kumrudisha marehemu kwa ajili ya mazishi?

Lisu kashambuliwa akiwa eneo lake la kazi Dodoma,so mlitaka ndg zake wawapigie magoti baada ya Siku 15 na kwa Hali ya Lisu angekua Mzima?

Kaa kimya mh unadhidi kutia aibu
 
Kwa utaratibu huu mgonjwa hujiandikia barua ya maombi au huandikiwa na mtu?
Kama hujiwezi unaandikiwa na ndugu na rufaa hupangi wewe anayepanga ni doctor anayekutibia ndo anakupa Barua ya kwenda kwa matibabu zaidi siwezi kutoka nyumbani Mtwara kwenda muhimbili afu nitegemee serikali kunilipia hakuna miujiza hiyo
 
Sasa kama hiyo serikali imeona ni muhimu wanafamilia kuomba msaada alikuwa na maana gani kuelezea umma? Ange wafuata familia awaeleze utaratibu. Kwani walipo mtibu huyo Sitta walitangazia umma?
Wasituletee mambo ya aibu hapa.
Tutachanga mia, mia tano ,elfu, kamanda ataeudi road.
Mbona wanatangizia umma kuwa wamenyimwa matibabu na serikali jiulize na hilo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom