Hoja ya umiliki wa kadi ya chama fulani ulichokua mwananchama wake wakati fulani haina mshiko wowote, naanza kupata shida sana na uelewa wa bwana mdogo nape, kama suala hili kweli linatoka kwenye ubongo na moyo wa nape, basi niseme tu kua nchi hii ina bahati mbaya sana kua na viongozi wa aina yake, lakini akili yangu haitaki kabisa kuamini kama kweli dogo kayasema hayo aikwa anayaamini toka ndani ya moyo wake, hapa niwe mkweli, ANAJUA UELEWA WA WATANZANIA WENGI NI MDOGO, vinginevyo asingeshupalia kitu cha kitoto kama hicho, hivi nani asie jua kua zamani kuwa mwanachama wa ccm ilikua ni lazima kwa wote? Wakati namaliza darasa la saba tu, mwaka 1987 nilikabidhia kadi ya umoja wa vijana (leo wanauita uvccm) kwanini, kwasababu, kwenye somo la siasa wakati huo tulikua tunasoma katiba 2, ya Jamuhuri ya mungano na katiba ya magamba, tulipokua tumaliza form 4 tulilazimika kuwa wanachama wa magamba by AUTO, mwaka uliofuata yaani 1992 sheria hiyo ikafutwa rasmi kwa vile tayari kulikua na mfumo wa vyama vingi, sasa je? wote waliokua na kadi za magamba miaka hiyo na sasa aidha sio wanachama wa chama chotechote au wapo upinzani, Je? wanalazimika kurudisha kadi zao za magamba huko magambani?
Ukweli, kinacho mfanya mtu kuwa mwanachama wa chama fulani, sio umiliki wa kadi bali je? bado analipia hiyo kadi yake kila mwaka? kama jibu ni ndio then huyo ni mwanachama wa hicho chama, lakini kama halipii kadi yake, huyo mwanachama ni mfuu, Nape akija kwenu, muulizeni hivi, Je? Dr. Slaa anaruhusiwa kuchagua viongozi wa ngazi yeyote nadani ya magamba? kama jibu ndio basi na mimi nitakua mtu wa kwanza kumdharau Dr. Slaa, lakini kama jibu ni hapana, basi nape aache kuwadharau Watanzania as from today!