Umiliki wa kadi za chama

Baba mtata

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
280
0
Heshima mbele!

Naomba kujua mtu kama alikua CCM akaamua kuhamia CUF je ni lazima ile kadi irudishe?au ni mali yake au anaweza hata kuitupilia mbali au sheria ikoje kwenye umiliki wa kadi.
 

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,783
2,000
Kadi ni kielelezo tu cha kuthibitisha uanachama. Uanachama ni wa hiari, hivyo siku mtu unaamua kuacha chama inatosha kuacha.

Kwa katiba ya CCM kujiunga na chama kingine ni sababu tosha ya kujitoa uanachama wa CCM. So kadi ya mtu aliyehamia chama kingine inabaki batili tu.

CCM kushupalia hoja hii ni upotoshaji wa makusudi na ukwepaji wa kubaki kwenye masuala ya msingi.
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
12,088
2,000
Kadi ni kielelezo tu cha kuthibitisha uanachama. Uanachama ni wa hiari, hivyo siku mtu unaamua kuacha chama inatosha kuacha.

Kwa katiba ya CCM kujiunga na chama kingine ni sababu tosha ya kujitoa uanachama wa CCM. So kadi ya mtu aliyehamia chama kingine inabaki batili tu.

CCM kushupalia hoja hii ni upotoshaji wa makusudi na ukwepaji wa kubaki kwenye masuala ya msingi.


Nakubaliana na wewe mkuu
 

S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
1,103
2,000
Kadi ya chama ni makarasi tu yasio na mpango na wanaoendeleo kufikiri kwamba makarasi ya chama ndio ushindi Wa kura au hoja za matatizo ya watanzania ni wavivu Wa kufikiri na wachovu waliokimbia ule wimbo Wa mchaka mchaka Wa jua lile litelemke mama!
 

Baba mtata

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
280
0
Thanx mtu wa shamba kwa maelezo na mchanganuo mzuri na nakubaliana na wewe lengo ni kututoa kwenye mambo ya msingi but tutashinda tu
 

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,455
2,000
Rostam Azizi aliamua kujiuzuru ubunge akisema kachoshwa na siasa uchwara. Badala ya kueneza sera za chama panazushwa umiliki wa kadi ya chama pinzani kana kwamba ni tija kwa wananchi.
 

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
2,653
0
Kadi ya chama ni makarasi tu yasio na mpango na wanaoendeleo kufikiri kwamba makarasi ya chama ndio ushindi Wa kura au hoja za matatizo ya watanzania ni wavivu Wa kufikiri na wachovu waliokimbia ule wimbo Wa mchaka mchaka Wa jua lile litelemke mama!

Wapo watu wengi, wenye kadi za vyama mbalimbali. Mifano ni mingi. Steven Wasira, ni mmoja wao. Mpaka sasa, bado anamiliki kadi ya NCCR- Mageuzi. Wakati anarejea CCM, alisema hatarejesha kadi yake ya NCCR- kwa kuwa ni mali yake.

Je, Wasira ni mwanachama wa NCCR? Hata Nape anamiliki kadi ya CCJ. Hajairejesha. Je, Nape ni mwanachama wa CCJ? Orodha ni ndefu. Kuna Dk. Harrison Mwakyembe. Ana kadi ya CCJ na CCM. Yupo Samuel Sitta. Anamiliki kadi ya CCJ na CCM. Je, Sitta na Mwakyembe, ni wanachama wa CCJ? 

dotto

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
1,725
1,500
Kipi muhimu Kadi ya uanachama au pesa zilizofichwa uswisi?? Nini Nape angesema akaeleweka kati ya kadi ya Dr.Slaa na Pesa za wezi wenzie walizosweka huko Uswisi na kwingineko. Kwa hoja hizi ndo zinaweza kuisambaratisha CDM kweli!!!???
 

Baba mtata

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
280
0
Ni kweli doto mambo ya msingi ya kujadili yapo lakini wanaanza kuibua hoja zisizo za maana ila mwisho wao unakuja FREEDOM IS COMING TOMMOROW
 

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
7,446
2,000
Hoja ya umiliki wa kadi ya chama fulani ulichokua mwananchama wake wakati fulani haina mshiko wowote, naanza kupata shida sana na uelewa wa bwana mdogo nape, kama suala hili kweli linatoka kwenye ubongo na moyo wa nape, basi niseme tu kua nchi hii ina bahati mbaya sana kua na viongozi wa aina yake, lakini akili yangu haitaki kabisa kuamini kama kweli dogo kayasema hayo aikwa anayaamini toka ndani ya moyo wake, hapa niwe mkweli, ANAJUA UELEWA WA WATANZANIA WENGI NI MDOGO, vinginevyo asingeshupalia kitu cha kitoto kama hicho, hivi nani asie jua kua zamani kuwa mwanachama wa ccm ilikua ni lazima kwa wote? Wakati namaliza darasa la saba tu, mwaka 1987 nilikabidhia kadi ya umoja wa vijana (leo wanauita uvccm) kwanini, kwasababu, kwenye somo la siasa wakati huo tulikua tunasoma katiba 2, ya Jamuhuri ya mungano na katiba ya magamba, tulipokua tumaliza form 4 tulilazimika kuwa wanachama wa magamba by AUTO, mwaka uliofuata yaani 1992 sheria hiyo ikafutwa rasmi kwa vile tayari kulikua na mfumo wa vyama vingi, sasa je? wote waliokua na kadi za magamba miaka hiyo na sasa aidha sio wanachama wa chama chotechote au wapo upinzani, Je? wanalazimika kurudisha kadi zao za magamba huko magambani?

Ukweli, kinacho mfanya mtu kuwa mwanachama wa chama fulani, sio umiliki wa kadi bali je? bado analipia hiyo kadi yake kila mwaka? kama jibu ni ndio then huyo ni mwanachama wa hicho chama, lakini kama halipii kadi yake, huyo mwanachama ni mfuu, Nape akija kwenu, muulizeni hivi, Je? Dr. Slaa anaruhusiwa kuchagua viongozi wa ngazi yeyote nadani ya magamba? kama jibu ndio basi na mimi nitakua mtu wa kwanza kumdharau Dr. Slaa, lakini kama jibu ni hapana, basi nape aache kuwadharau Watanzania as from today!
 

Teacher1

JF-Expert Member
Jan 29, 2011
333
250
Shetani alijivuna mbele za Munu kuwa Ayubu ni Mtu wake, Mungu akamwambia amjaribu alone kama ni wake akajaribu na kushindwa. Naomba CCM wamtumie Dr slaa kuhubili siasa zao za kifisadi akikubali basi wao kadi kitu gani? Mbona kadi zao nyingi hupokelewa kweye mikutano mbali mbali ya vyama pinzani. Wanambie Kama wameweka utaratibu wa kuzifuata na wameshakusanya ngapi hadi sasa. Ni lini seif aridudisha kadi na wapi. Huyo mbwabwajaji Nape kadi yake ya CCJ alirudisha tar ngapi?
 

Bartazar

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
1,040
2,000
Nafikiri hii mbinu inatumiwa na ccm ili kuwaondoa watu kwenye tafakuri ya msingi ya kuzorota kama sio kukwama kwa maendeleo ya nchi kulikosababishwa na chenyewe ili watu wasifikiri sana madudu ambayo inayafanya na serikali yake, na badala yake wajikite kujadili hoja za kipuuzi za mara kadi, sijui ooh... kuoa mke wa mtu.....!!!! CDM ni watu makini hawawezi kupoteza concentration kwa ajili ya mambo ya kijinga jinga kama haya. Uanachama wa mtu unatoka moyoni na si makaratasi ambayo Nape na ccm wanayang'ang'ania!
 

tenende

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
6,512
1,195
Eeeh haya majibu yanamfaa Nepi NNauye a.k.a mtoto wa BABU NNAUYE na mwalimu wa ukakamavu mkoa wa Lindi wa mwaka 1965 (yaani miaka 47 iliyopita). Mzee Moses NNAuye au baba Mariamu, wakati huo alikuwa amerudi kutoka CHINA!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom