UMEYA DAR: Dr. Massaburi aibuka kidedea...............

Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
631,987
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 631,987 280
Magazeti yamepambwa na habari hii.............

Gazeti la Uhuru lina kichwa cha habari kisemacho...............Umeya Dar: Dr. Massaburi aibuka kidedea......................

Huku gazeti la Mwananchi nalo likisheheni kichwa cha habari kisemacho...........Umeya CCM pindupindu............................

12_10_mzbe3s.jpg

Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
631,987
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 631,987 280

Masaburi kumrithi Kimbisa Dar es Salaam

Imeandikwa na Oscar Job; Tarehe: 16th December 2010 @ 06:13

NYOTA ya Umeya wa Jiji la Dar es Salaam imemwangazia Diwani wa Kata ya Kivukoni katika Manispaa ya Ilala, Didas Masaburi, baada ya jana kushinda katika kinyang'anyiro cha nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kutokana na uchache wa viti vya udiwani vya vyama vya Upinzani ukilinganisha na vile vya madiwani wa Chama Cha Mapinduzi, ni dhahiri kuwa Mbunge huyo wa Bunge la Afrika Mashariki ndiye atakayekuwa mrithi wa Adam Kimbisa aliyeongoza Dar es Salaam kwa miaka mitano iliyopita.

Kimsingi, Masaburi ndiye Meya mpya wa Dar es Salaam kwani katika Jiji la Dar es Salaam, CCM inavyo viti 111 wakati wapinzani wana viti 14 tu. Kati ya hivyo, Ilala wanacho kimoja, Temeke viwili na Kinondoni 11.

Madiwani hao wa vyama vyote kesho watapiga kura kumchagua Meya wa Jiji. Masaburi alichaguliwa na Baraza la Madiwani la CCM la Jiji la Dar es Salaam jana kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, kwa kuwashinda wagombea wenzake wawili, Tarimba Abbas na Hashimu Saggaf kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee.

Masaburi alishinda kwa kupata kura 61 kati ya kura 111 zilizopigwa na wajumbe wote huku Tarimba anayetokea Kata ya Hananasif katika Manispaa ya Kinondoni, akipata kura 33 na Saggaf aliyewahi kuwa Mbunge wa Dodoma Mjini na sasa Diwani wa Mchafukoge, aliambulia kura 17.

Awali, kabla ya kutangaza matokeo hayo, Msimamizi wa uchaguzi huo, Ritta Mlaki, aliwataka wajumbe na wagombea wote kutulia wakati wa kuyatangaza matokeo hayo huku akisisitizia ushindi uliopatikana hapo ni wa huru na kuwa wagombea wamepigiwa kura kutokana na namna wanavyokubalika na wajumbe.

Aidha, aliwapongeza wajumbe wote kwa kufanikisha uchaguzi huo katika hali ya utulivu na amani huku pia akisifia demokrasia iliyokomaa ndani ya chama hicho tawala kwa kuzingatia kuwa hakuna kura hata moja iliyoharibika katika uchaguzi huo.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, baadhi ya wajumbe waliokuwemo katika ukumbi huo, walishangilia kwa nderemo huku mke wa mshindi huyo, Janet Masaburi aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, akiangua kilio sambamba na kupiga magoti na kumwomba Mungu.

Masaburi aliahidi kushirikiana na wenzake kumaliza kero mbalimbali za wakazi wa Jiji na kuwataka madiwani wenzake kuvunja kambi ndani ya CCM ili kusimama kama kitu kimoja kwa maslahi ya chama hicho.

Aidha, katika uchaguzi huo uliofanyika katika ngazi za Manispaa zote tatu za Jiji la Dar es Salaam, Temeke, Kinondoni na Ilala, pia matokeo yaliyotolewa yaliangusha nderemo kwa baadhi ya wajumbe.

Katika Manispaa ya Ilala, Diwani wa Jangwani na Meya wa siku nyingi wa Ilala, Abuu Jumaa alikula mwereka kwa kijana mdogo, Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jerry Silaa baada ya kushindwa kwa kura 25 dhidi ya zake 10. Silaa alikuwa Naibu wa Jumaa katika Baraza la Madiwani lililopita.

Mgombea mwingine, Salumu Bisalala kutoka Kata ya Kariakoo aliambulia kura mbili. Nafasi ya Naibu Meya ilikwenda kwa Eli Kessy kutoka Kata ya Kisutu aliyepata kura 20 na kuwashinda wenzake, Abdulkadiri Salum ‘Masamaki' aliyepata kura 11 na Mtumwa Mohamed aliyepata kura tano.

Kwa upande wa Temeke, Maabad Hoja alichaguliwa kuwania nafasi ya umeya wa Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam, kwa tiketi ya CCM.

Hoja alitangazwa jana katika uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Manispaa hiyo, baada ya kuwashinda wagombea wengine wawili.

Wakati Hoja akitangazwa kuwa mgombea mteule wa nafasi hiyo, wajumbe walimteua Aisha Mpanjila kuwania nafasi ya unaibu meya wa manispaa hiyo.

Akitangaza matokeo Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke, Saad Kusilawe, alisema kura zilizopigwa katika nafasi ya umeya ni 39 na kwamba hakuna zilizoharibika; na katika hizo, Hoja alipata kura 30 huku akiwaacha Michael Mwakasindile aliyepata sita na Zena Mgaya kura tatu.

Kwa nafasi ya unaibu meya, wajumbe walikuwa 39 na hakuna kura iliyoharibika ambapo Mpanjila aliteuliwa baada ya kupata kura 34, huku Abdallah Chaurembo akipata tatu na Muhidini Sanya mbili.
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
631,987
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 631,987 280
Umeya CCM pindu pindu
Wednesday, 15 December 2010 21:50

Waandishi Wetu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) jana kilipitisha majina ya wagombea wake wa umeya katika maeneo kadhaa nchini zikiwamo anispaa za Jiji la Dar es Salaam huku wakongwe wa nafasi hizo wakitupwa.Miongoni mwa vigogo waliokumbwa na kimbunga hicho ni aliyekuwa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kwa miaka 20 na mbunge kwa miaka 30, Samuel Ruangisa..Ruhangisa ambaye ni Diwani wa Kata ya Kitendaguro alipata kura mbili katika uchaguzi huo uliofanyika jana ukiwashikirikisha madiwani 14 wa kata, madiwani wanne wa viti Maalumu na kura tatu za wabunge.

Katibu wa CCM wa Bukoba mjini, Sangija Sankcoba alisema alipokuwa akitangaza matokeo hayo kuwa katika nafasi hiyo ya umeya, kulikuwa na wagombea watatu ambao ni Robert Katunzi ambaye hakupata hata kura moja, Samuel Ruangisa, kura mbili na diwani wa Kata ya Kagondo, Anathory Amani, aliyepata kura 15.

Katibu huyo wa CCM pia alimtangaza Diwani wa Kata ya Buhembe, Alexander Ngalinda kuwa Naibu meya wa Manispaa hiyo baada ya kupata kura 13 kati ya kura 17 zilizopigwa.

Ngalinda ameibuka mshindi dhidi ya aliyekuwa Dauda Kalumuna aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo kwa miaka 20. Kalumuna ambaye ni Diwani wa Kata Ijuganyondo aliyekura nne.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa baada ya matokeo hayo, Ruangisa alidai kuwa hayatambui bila kutaja sababu.

Wakati hayo yakijiri mkoani Kagera, jijini Dar es Salaam nako mambo si shwari kwa aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Abuu Juma, aliyeangushwa na aliyekuwa naibu wake, Jerry Silaa, katika kinyang'anyiro cha hicho.

Silaa alimwangusha Jumaa baada ya kupata kura 25 kati ya kura 37 zilizopigwa kwenye uchaguzi huo huku meya huyo wa zamani akiambulia kura kumi tu.

Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Ernest Chale, alimtangaza Silaa kuwa mshindi na kwamba ndiye atakayeiwakilisha CCM kwenye uchaguzi wa meya unaotarajia kufanyika kesho.

Akitangaza matokeo hayo, Chale alisema Silaa ambaye ni diwani wa kata ya Ukonga, alishinda kwa kura 25 huku Juma akipata kura 10 na Salumu Kisalala kura mbili.

Aidha Chale alimtangaza Kherry Kessy kuwa mgombea wa nafasi ya Naibu Meya wa manispaa hiyo baada ya kuwashinda wapinzani wake kwa kupata kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa.

Katika uchauzi huo Mtumwa Mohamed alipata kura 5 na mgombea mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Masamaki alipata kura 11.

Katika Manispaa ya Temeke, Diwani wa Kata ya Pemba Mnazi Hoja Selemani, alitangazwa mshindi katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye manispaa hiyo jana.

Jina la Hoja litawasilishwa kwa mkurugenzi wa manispaa hiyo leo tayari kwa kushiriki uchaguzi wa kiti cha meya unaotarajiwa kufanyika kesho.

Akitangza matokeo hayo Kusilawe alisema Hoja alipata kura 30 akifuatiwa na Victor Mwakasindile aliyepata kura sita huku Zena Mgaya akiambulia kura tatu.

Katika uchaguzi huo, Aisha Rashid, aliibuka mshindi nafasi ya Naibu Meya baada ya kupata kura 34 akiwagaragaza Chaurembo Abdallah aliyepata kura tatu na Sanya Muhidin kura mbili.

Baada ya kutangaza matokea hayo Kusilawe: "Ijumaa ninatarajia kupata kura 37 za ndio na kura nne tu ndizo zitakuwa za hapana"alisema Kusilawe na kuwasuhi madiwani hao kufuta makundi.

Wakati huo huo, Katibu wa CCM, wilaya ya Kinondoni, Sixtus Mapunda, amemtangaza diwani wa Kata ya Mikocheni, Yusuph Mwenda kuwa mgombea wa kiti cha umeya katika kuchaguzi unaotarajiwa kufanyika kesho.

Kwa mujibu wa katibu huyo, Mwenda ameshinda baada ya kupata kura 28 dhidi ya wapinzani wake, Ibrahim Kisoki aliyepata kura sita na Richard Chengula kura nne.

Pia katibu huyo wa CCM alimtangaza diwani wa kata ya Mwananyamala Songoro Mnyonge, kuwa mgombea wa nafasi ya unaibu meya baada ya kupata kura 28.

Alisema diwani huyo aliibuka mshindi dhidi ya Lucas Mgonja aliyepata kura saba na Hajat Hemed ambaye aliambulia kura sifuri.
Naye diwani wa Kata ya Kivukoni Didas Masaburi, ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha kugombea Kiti cha Meya wa Jiji la Dar es Salaam kupitia tiketi ya CCM.

Masaburi aliibuka kidedea katika kinyang'anyiro hicho baada ya kupata kura 61 akifuatiwa na diwani wa Kata ya Ananasifu, Abas Tarimba aliyepata kura 33 na Diwani wa Kata ya Mchafu Koga, Hashim Sagafu kupata kura 17.

Msimamizi wa uchaguzi huo, Rita Mlaki alisema wanachama waliopiga kura katika uchaguzi huo walikuwa 111 na hakuna kura iliyoharibika.

Matokeo hayo yalimfanya mkewe Masaburi, Janeth Masaburi aliyekuwa amekaa sehemu ya juu katika ukumbi mkubwa wa Karim Jee, kuangua kilio cha furaha na kupiga mayowe.

Baada ya kumalizika uchaguzi huo majira ya saa 11:28 jioni, Sagafu alimpongeza Masaburi na kuahidi kushirikiana naye.

Sagafu pia aliwataka wanaCCM kuacha makundi yaliyojitokeza na kuwa kitu kimoja katika kuleta maendeleo ya jiji la Dar es Salaam.
Awali, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, aliwataka madiwani kushughulikia migogoro kwa kutumia busara na kusuluhisha pale panapohitajika ili kutuliza hali ya mgawanyiko uliotokea katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Guninita aliwataka wanachama wa CCM, kuwa wamoja na kuacha kusononeka kwa kutafuta mchawi kwa sababu hilo litazidi kuwabomoa.

Mkoani Dodoma mchuano wa kuwania kiti cha meya na naibu wake ulikuwa lakini diwani wa kata ya Chigongwe, Emanuel Mwiliko aliibuka kuwa mshindi.

Mwiliko aliibuka mshindi dhidi ya wapinzani wake Msinta Mayao wa Kata ya Majengo ambaye alipata kura 11 na Wallece Lusingu aliambuliwa kura tatu.

Awali katika mchakato huo kulikuwa na mvutano mkali huku wengi wakidai kuwa mchakato wa uchaguzi katika Manispaa hiyo ulikuwa umegubikwa na ukabila jambo lililozua mtafaruku mkubwa.

Tofauti na kiti cha umeya, uchaguzi wa naibu meya ulikuwa na mvutano mkali uliotokana na maswahiba wawili wa muda mrefu kuwania nafasi hiyo jambo ambalo lilifanya wapambe wao wameguke.

Waliokuwa wakichuana katika nafasi hiyo ni Jumanne Ngede ambaye ni Diwani wa Kata ya Chamwino, William Njilimui (Mtumba) na Naibu Meya aliyekuwa akitetea kiti chake, Jaffari Mwanyemba wa kata ya Viwandani.

Katika uchaguzi huo Mwanyemba ambaye amekuwa Naibu Meya kwa kipindi kirefu, aliangushwa na swahiba wake, Jumanne Ngede baada ya Ngede kujikusanyia kura 24 dhidi ya kura 20 za Mwanyemba na kura moja ya Njilimui.

Katika uchaguzi huo ambao ulisimamiwa na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Dodoma Mjini,madiwani pia walimchagua Diwani wa Kata ya Makole Moses Komba kuwa Katibu wa madiwani wa chama hicho tawala.

Komba alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 23 na kumshinda Diwani wa Kata ya Hazina, Peter Ishebabi ambaye alipata kura 21.

Manispaa ya Dodoma ina madiwani 50, kati yao 46 wanatoka CCM na madiwani wanne wamechaguliwa kutoka Chadema.

Habari hii imeandaliwa na Geofrey Nyangóro, Raymond Kaminyoge, Dar na Lilian Lugakingira , Bukoba, Habel Chidawali, Dodoma
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
631,987
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 631,987 280
Thursday December 16, 2010 Local News
Masaburi new Dar es Salaam Mayor

By DAILY NEWS Reporter, 15th December 2010 @ 22:00, Total Comments: 0, Hits: 208

DAR ES SALAAM councillors on CCM ticket have chosen Dr Didas Massaburi the Mayor of Dar es Salaam City, scoring more than half of the total number of votes counted.

In the election held at Karimjee Hall in Dar es Salaam on Wednesday, Massaburi who is the councillor of Kivukoni Ward, Ilala Municipality scored 61 out of 111 votes. He defeated the other hopefuls namely, Mr Abbas Tarimba with 33 votes and Hashimu Sagaf with 17 votes.

Before announcing the final results, the election supervisor, Mrs Ritta Mlaki requested all delegates and the aspirants to remain calm, insisting that the election was carried out in a free and fair atmosphere and the results reflected on the people's choice.

She commended all participants for professional undertaking of the exercise such that not a single vote was spoilt. "This proves maturity in democracy among the party members," Ritta said.

"And the winner is Mr Didas Massaburi," she declared the winner followed by ululations, clapping, whistling and joyous shouts. The wife of the winner also an MP, Special Seats, Janet Massaburi could not ‘withstand the heat,' as she cried in joy and knelt down praising the Almighty God for the husband's victory.

Surprises never ended in three other municipalities of Dar es Salaam namely Ilala, Temeke and Kinondoni where similar scenes of celebrations and disappointment were noted. Some of the defeated hopefuls appeared devastated while the winners expressed gratitude to the voters who put them in office.

Mr Abuu Jumaa the former mayor of Ilala municipality and councillor of Jangwani ward was among the defeated. The new mayor of Ilala Municipality is Jerry Silaa from Gongo la Mboto Ward who scored 25 votes defeating other aspirants, Mr Abuu Jumaa (10) votes and Mr Salumu Bisalala from Kariakoo Ward with 2 votes.

The new deputy mayor is Eli Kessy from Kisutu Ward who clinched 20 votes, beating Salumu Masamaki (11) and Mtumwa Mohamed (5) votes.

Meanwhile Temeke municipality yesterday finalized the primaries ahead of the similar exercise and at the end of the process Maabad Hoja was declared the CCM candidate for the post of Temeke Municipal mayor.

Hoja was declared the candidate at the end of the meeting held at the municipal council chamber, defeating two other aspirants while Aisha Mpanjila was chosen to stand for the position of the deputy mayor.

Announcing the results, CCM Temeke district secretary, Saad Kusilawe said a total of 39 votes were cast and none was spoilt. Hoja scored 30 votes, followed by Mr Michael Mwakasindile with six votes and Zena Mgaya three votes.

As for the post of deputy mayor 39 votes were counted and none was spoilt as well, leading to the declare of Aisha Mpanjila the candidate after scoring 34 votes against Abdallah Chaurembo (3) votes and Muhidini Sanya (2) votes.
 
M

matawi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2010
Messages
2,055
Likes
12
Points
135
M

matawi

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2010
2,055 12 135
Huyu Ocampo asiangalie mauaji tu hata ufisadi tutaomba auingize kwenye shughuli zao maana watu wanacheza sana na maisha ya watu shenn*********
 
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,863
Likes
8,686
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,863 8,686 280
HII NI AKILI AU MKOJO

YAANI DIWANI/MBUNGE/MEYA VYOTE MTU MMOJA KAMA SIJAELEWA WANA CCM MNA MATATAIZO YA AKILI KWA KWELI EMBU SOMA HAPO...MMEKOSA WA KUWACHAGUA

NYOTA ya Umeya wa Jiji la Dar es Salaam imemwangazia Diwani wa Kata ya Kivukoni katika Manispaa ya Ilala, Didas Masaburi, baada ya jana kushinda katika kinyang'anyiro cha nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kutokana na uchache wa viti vya udiwani vya vyama vya Upinzani ukilinganisha na vile vya madiwani wa Chama Cha Mapinduzi, ni dhahiri kuwa Mbunge huyo wa Bunge la Afrika Mashariki ndiye atakayekuwa mrithi wa Adam Kimbisa aliyeongoza Dar es Salaam kwa miaka mitano iliyopita.

Kimsingi, Masaburi ndiye Meya mpya wa Dar es Salaam kwani katika Jiji la Dar es Salaam, CCM inavyo viti 111 wakati wapinzani wana viti 14 tu. Kati ya hivyo, Ilala wanacho kimoja, Temeke viwili na Kinondoni 11.

Madiwani hao wa vyama vyote kesho watapiga kura kumchagua Meya wa Jiji. Masaburi alichaguliwa na Baraza la Madiwani la CCM la Jiji la Dar es Salaam jana kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, kwa kuwashinda wagombea wenzake wawili, Tarimba Abbas na Hashimu Saggaf kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee.

Masaburi alishinda kwa kupata kura 61 kati ya kura 111 zilizopigwa na wajumbe wote huku Tarimba anayetokea Kata ya Hananasif katika Manispaa ya Kinondoni, akipata kura 33 na Saggaf aliyewahi kuwa Mbunge wa Dodoma Mjini na sasa Diwani wa Mchafukoge, aliambulia kura 17.BOGUS KABISA MMEKOSA WATU VYEO VYOTE MTU MMOJA??
 
Ally Msangi

Ally Msangi

Verified Member
Joined
Jun 29, 2010
Messages
594
Likes
17
Points
35
Ally Msangi

Ally Msangi

Verified Member
Joined Jun 29, 2010
594 17 35
CCM si wanabebana kwa vyeo,
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Messages
16,581
Likes
3,132
Points
280
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2007
16,581 3,132 280
Mh huyu jamaa si ndiye aliyehua MRADI WA MABASI YA WANAFUNZI DAR ES SALAAM?
 
Mdau

Mdau

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2008
Messages
1,781
Likes
267
Points
180
Mdau

Mdau

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2008
1,781 267 180
Manji OYEEEEEEEE!!! Nchi hii ya ki***** sana ku******!!!
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
27,260
Likes
30,563
Points
280
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
27,260 30,563 280
Masaburi akiwa Mwenyekiti wa vijana Dar aliua mradi wa mabasi ya wanafunzi na kuanzia hapo maisha yake yalibadilika na kuwa ya hali ya juu. Ajabu ni kuwa wakati huo katibu wake wa Mkoa alikuwa Guninita ambaye leo ndiye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dsm.
Hivyo Masaburi Meya wa Dar, Guninita Mwenyekiti wa CCM Dar. Is it coincidence or a long term plan?
Na jee kweli DSM itasalimika au ndio vurugu mechi tuu na kuliwa kwenda mbele?
 
mfianchi

mfianchi

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2009
Messages
8,767
Likes
2,321
Points
280
mfianchi

mfianchi

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2009
8,767 2,321 280

Masaburi kumrithi Kimbisa Dar es Salaam

Imeandikwa na Oscar Job; Tarehe: 16th December 2010 @ 06:13

NYOTA ya Umeya wa Jiji la Dar es Salaam imemwangazia Diwani wa Kata ya Kivukoni katika Manispaa ya Ilala, Didas Masaburi, baada ya jana kushinda katika kinyang'anyiro cha nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kutokana na uchache wa viti vya udiwani vya vyama vya Upinzani ukilinganisha na vile vya madiwani wa Chama Cha Mapinduzi, ni dhahiri kuwa Mbunge huyo wa Bunge la Afrika Mashariki ndiye atakayekuwa mrithi wa Adam Kimbisa aliyeongoza Dar es Salaam kwa miaka mitano iliyopita.

Kimsingi, Masaburi ndiye Meya mpya wa Dar es Salaam kwani katika Jiji la Dar es Salaam, CCM inavyo viti 111 wakati wapinzani wana viti 14 tu. Kati ya hivyo, Ilala wanacho kimoja, Temeke viwili na Kinondoni 11.

Madiwani hao wa vyama vyote kesho watapiga kura kumchagua Meya wa Jiji. Masaburi alichaguliwa na Baraza la Madiwani la CCM la Jiji la Dar es Salaam jana kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, kwa kuwashinda wagombea wenzake wawili, Tarimba Abbas na Hashimu Saggaf kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee.

Masaburi alishinda kwa kupata kura 61 kati ya kura 111 zilizopigwa na wajumbe wote huku Tarimba anayetokea Kata ya Hananasif katika Manispaa ya Kinondoni, akipata kura 33 na Saggaf aliyewahi kuwa Mbunge wa Dodoma Mjini na sasa Diwani wa Mchafukoge, aliambulia kura 17.

Awali, kabla ya kutangaza matokeo hayo, Msimamizi wa uchaguzi huo, Ritta Mlaki, aliwataka wajumbe na wagombea wote kutulia wakati wa kuyatangaza matokeo hayo huku akisisitizia ushindi uliopatikana hapo ni wa huru na kuwa wagombea wamepigiwa kura kutokana na namna wanavyokubalika na wajumbe.

Aidha, aliwapongeza wajumbe wote kwa kufanikisha uchaguzi huo katika hali ya utulivu na amani huku pia akisifia demokrasia iliyokomaa ndani ya chama hicho tawala kwa kuzingatia kuwa hakuna kura hata moja iliyoharibika katika uchaguzi huo.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, baadhi ya wajumbe waliokuwemo katika ukumbi huo, walishangilia kwa nderemo huku mke wa mshindi huyo, Janet Masaburi aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, akiangua kilio sambamba na kupiga magoti na kumwomba Mungu.

Masaburi aliahidi kushirikiana na wenzake kumaliza kero mbalimbali za wakazi wa Jiji na kuwataka madiwani wenzake kuvunja kambi ndani ya CCM ili kusimama kama kitu kimoja kwa maslahi ya chama hicho.

Aidha, katika uchaguzi huo uliofanyika katika ngazi za Manispaa zote tatu za Jiji la Dar es Salaam, Temeke, Kinondoni na Ilala, pia matokeo yaliyotolewa yaliangusha nderemo kwa baadhi ya wajumbe.

Katika Manispaa ya Ilala, Diwani wa Jangwani na Meya wa siku nyingi wa Ilala, Abuu Jumaa alikula mwereka kwa kijana mdogo, Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jerry Silaa baada ya kushindwa kwa kura 25 dhidi ya zake 10. Silaa alikuwa Naibu wa Jumaa katika Baraza la Madiwani lililopita.

Mgombea mwingine, Salumu Bisalala kutoka Kata ya Kariakoo aliambulia kura mbili. Nafasi ya Naibu Meya ilikwenda kwa Eli Kessy kutoka Kata ya Kisutu aliyepata kura 20 na kuwashinda wenzake, Abdulkadiri Salum ‘Masamaki' aliyepata kura 11 na Mtumwa Mohamed aliyepata kura tano.

Kwa upande wa Temeke, Maabad Hoja alichaguliwa kuwania nafasi ya umeya wa Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam, kwa tiketi ya CCM.

Hoja alitangazwa jana katika uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Manispaa hiyo, baada ya kuwashinda wagombea wengine wawili.

Wakati Hoja akitangazwa kuwa mgombea mteule wa nafasi hiyo, wajumbe walimteua Aisha Mpanjila kuwania nafasi ya unaibu meya wa manispaa hiyo.

Akitangaza matokeo Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke, Saad Kusilawe, alisema kura zilizopigwa katika nafasi ya umeya ni 39 na kwamba hakuna zilizoharibika; na katika hizo, Hoja alipata kura 30 huku akiwaacha Michael Mwakasindile aliyepata sita na Zena Mgaya kura tatu.

Kwa nafasi ya unaibu meya, wajumbe walikuwa 39 na hakuna kura iliyoharibika ambapo Mpanjila aliteuliwa baada ya kupata kura 34, huku Abdallah Chaurembo akipata tatu na Muhidini Sanya mbili.
Kutoka ubunge wa Afrika Mashariki hadi kuomba udiwani na hatimaye Umeya ,si bure
 
Forum statistics

Threads 1,236,304
Members 475,050
Posts 29,253,487