Umewahi pata adhabu hizi??

Adhabu kubwa zaidi niliyowahi kupata shule ni kufagia
 
Hilo zoezi linafaa kwa afya
 
Nakumbuka usagara shelutete wakati ni mwalimu wa chemistry late 70's alitoa kama hio na kubeba desk lako!
 
Kwa sisi tuliopitia Jitegemee hiyo ni ndogo sana,Hasa siku hiyo umkute Bwenge ana hasira zake huko alipotoka......
 
natupa hapo chini nakimbia mpaka nyumbani sirudi tena shule,nakumbukaa nikiwa std six mwalimu alitoa dhabu ya viboko 12 du nikaona hapa shida sana ile apenichapa 1 nikaanguka chini nikabana pumzi at nimezimia fasta nikakimbizwa hospitali ile nes wanaanza kuniwekea drip nikawaambi nimepona sikutandikwa tena mpaka namaliza shule ,
 
Hilo zoezi linafaa kwa afya

Work is said to be done when a certain amount of force is applied in the direction of the force.
Workdone = Force x Distance.
Zoezi kama kukimbia, kucheza mpira ni moja ya kazi(zoezi), lakini kubeba tofali na kutulizwa mahali pamoja hiyo si kazi bali ni uonevu na udhalilishaji tu.
 
Hizi adhabu sometimes zilikuwa zinatujenga kiaina.
 
hapa umenena mkuu............
 
Haya ni maandalizi ya kupambana na maisha magumu ya Tanzania kwa siku za usoni.
 

Adhabu za kukomoana hizo !!

Adhabu imbayo ingefaa hapa ni kuwaambia wachimbe shimo la takataka, kung'oa visiki, kufagia uwanja, kupiga deki madarasa, n.k. Yaani adhabu 'zinazolipa', adhabu zinazozalisha au kutoa huduma fulani kwa shule.
 

Hahahahaha janja sana wewe
 
Ulikosa nini hadi ukaadhibiwa kufagia?

Nilichelewa nikaambiwa nikafagie, nikaomba msamaha mwalimu akakataa akanigooomba vizuri, na mie nikaliiiiia vizuri, mpaka akatokea jamaa mmoja anaitwa Mussa na rafiki yake anaitwa Anthony (bless their hearts), wakanbembeleza weee, nikanyamaza wakafagia wao πŸ™‚
 

Hahahaaa..duuuh!

Yaelekea ulikuwa mwanafunzi mtiifu sana wewe.

Sie wengine tushawakosa kosa ngumi walimu.
 
Hahahaaa..duuuh!

Yaelekea ulikuwa mwanafunzi mtiifu sana wewe.

Sie wengine tushawakosa kosa ngumi walimu.

Hehehe mie sio nilikuwa mtii, ni mtii hadi sasa. Hapati mtu tabu hapa πŸ˜‰

Kisa cha kumkosa kosa mwalimu ngumi?
 
Hehehe mie sio nilikuwa mtii, ni mtii hadi sasa. Hapati mtu tabu hapa πŸ˜‰

Kisa cha kumkosa kosa mwalimu ngumi?

Kisa ni kukataa kunyanyaswa!

Wewe mtu unapigwa kama mtumwa sababu tu monita kakuandika jina eti ulikuwa unapiga kelele?

Halafu unaamriwa ushike dawati au ukuta halafu ucharazwe mboko sita, na kabla ya hapo unapapaswa kuona kama umeweka makaratasi kwenye kaptura.

Hapana bana. Siyo mtumwa miye. Ukinigusa kwa nguvu inakurudia, ima fa ima.

Nchi za watu mwalimu hagusi mwana wa mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…