Umewahi Kuwekwa Lockup (Lupango)?

Umewahi Kuwekwa Lockup (Lupango)?

Kuna mshkaji wetu shughuli zake ni kusukuma mkokoteni alipita mitaa ya Msisiri na mkokoteni wake akaambiwa aliuiba auache.

Akaja kutushtua tukatoka tunaufuata mkokoteni, alichosahau kutuambia jamaa ni kua waliompora mkokoteni ni wachoma chips ye alitutajia idadi tu kua wako watano.

Sisi tulienda saba yeye wa nane, wale walikua watano lakini walikua na visu. Dula pompo kichaa sana kufika tu kaufuata mkokoteni kaanza kuusukuma, jamaa mmoja akafikia kumkwida, Dula akapeleka ngumi kama nne za fasta, jamaa chini.

Wale wengine ndiyo wakainuka na visu sasa, jamaa kaniletea kisu badala nikimbie mi nikataka kumdaka mkono. Nilifurahi.

Mwisho wa yote askari wakafika tukawekwa mahabusu mpaka kesho ishu ikaishia hewani.

Long Live Tilalila
 
2005 ile siku ya uchaguzi ambao mzee wa Msoga alishinda kwa % nyingi,tupo kwenye folen ya kujongea sanduku la kura tukamchague raisi kijana{tuliaminishwa hivyo}hapo jua limeshanitandika kisawa sawa sasa jamaa katoka alikotoka anakuja kusimama mbele yangu kibabe akidai kwamba alikuja kabla yangu.

Ktk kubishana bishana jamaa akanipa punch moja matata basi mimi kule,nagara gara kwenye michanga na mavumbi kikadi chenyewe nilikishika mkononi sikioni sasa ile najizoa zoa niamke nikajikuta nimegusa kipande cha jiwe nikakishika,aah hakikurudi nilimtusua kwenye paji la uso kupiga kura kukaishia hapo hapo.

Siyo mimi wala jamaa aliyepiga kura,aliwahishwa hospital mimi nikaishia kuwekwa lockup pale Lumumba kipindi kile kikiwa kituo kabla hapajafanywa office za serikali za mitaa,hii ilikuwa pale Mnazi Mmoja shule ya msingi kama humu kuna mtu alikuwepo siku ile atakumbuka jinsi kura zilivyosimama kupigwa kwa mbilinge lililokuwepo siku hiyo.
 
Hapana Ila huko hakuna mwenyewe yeyote aweza kwenda.
 
Sungusungu sijui spidi yao wanaitoa wapi. Enzi hizo hapa mtaani kulikua na askari anaitwa sura mbaya.

Mimi mdogo tu. Night kali tunarudi mitaa ya home kufika sehemu hivi kuna uwanja tunaliona difenda, tukageuka tutafute ruti nyingine. Kumbe wanatuchora, ile tunapiga hatua kadhaa ghafla askari na sungusungu wakatuungia.

Hapo ilikua pale Makaburini mwananyamala, tukavamia makaburi tukawa kama tunaenda uelekeo wa kwa mzee Madai/ Biafra.
Tulikua kundi la watu kumi lakini ghafla nashangaa ile ruti niliyochagua nipo mimi na A. Tukafika ukuta wa nyumba ya mzee Madai A akaurukia kachupa yupo ndani mimi kurukia kukanishinda, kimo hakiruhusu.

Nikiwa najaribu kukanyaga matofali nipande juu namsikia Sura Mbaya anatishia kunishuti huku anakoki jegeja. Nikawa mpole. nikapelekwa mahabusu nikalala kesho nikafuatwa.
 
Hahahahaha ukasikia analitekenya zeze?
 
Mi walinshikilia kwa masaa kadhaa ya usiku then wakaniachia
 
kuna siku sisi vijana wa ccm tumewapiga chadema..police wakaja kutuliza Ile vagi..tukakamatwa tukapelekwa central..tukakaa kama nusu saa hivi..ikapigwa simu kutoka juu kuwa sisi vijana wa ccm tuachiwe..wale wa chadema walipelekwa mpaka gerezani wakanyimwa na dhamana
 
mwanaume mtafutaji either kwa njia yyote ile ujanja ujanja na hata kwa njia ya haki, kwenda lockup ni kitu cha kawaida, coz hata hao polis adhabu yao huwa ni kukaa lockup wanapofanya utovu wa kinidhamu
 
Sungusungu sijui spidi yao wanaitoa wapi. Enzi hizo hapa mtaani kulikua na askari anaitwa sura mbaya.

Mimi mdogo tu. Night kali tunarudi mitaa ya home kufika sehemu hivi kuna uwanja tunaliona difenda, tukageuka tutafute ruti nyingine. Kumbe wanatuchora, ile tunapiga hatua kadhaa ghafla askari na sungusungu wakatuungia.

Hapo ilikua pale Makaburini mwananyamala, tukavamia makaburi tukawa kama tunaenda uelekeo wa kwa mzee Madai/ Biafra.
Tulikua kundi la watu kumi lakini ghafla nashangaa ile ruti niliyochagua nipo mimi na A. Tukafika ukuta wa nyumba ya mzee Madai A akaurukia kachupa yupo ndani mimi kurukia kukanishinda, kimo hakiruhusu.

Nikiwa najaribu kukanyaga matofali nipande juu namsikia Sura Mbaya anatishia kunishuti huku anakoki jegeja. Nikawa mpole. nikapelekwa mahabusu nikalala kesho nikafuatwa.
sante kwa kunipunguzia stress
 
Mi vyote nilishakutwa navyo aseee
Mahabusu miaka mitatu
Kizimbani mara nyingi kwa kesi tofauti
Magereza miaka kumi na minne kwa mujibu wa hukumu ya kwanza, baada ya rufaa miaka tisaaa

Yoooote tisa

Nimekaa kifungo cha nafsi miaka 18

Mpaka sasa namshukuru Mungu niko huru nje ndani
Niko na taasisi yangu imara ya ndoa na familia yangu toka mwaka 90.
Baada ya yote hayo
 
Nilishawahi kuwekwa lockup walivyoondoka wale walioniweka wale maaskar wakanitoa tukawa tunapiga stor huku tukishushia na lager nyama ya mbuzi ikiwa jikon nyuma ya kituo cha msimbaz.
gahawa hii mkuu
 
Nlishawahi kaa lock up pale magomen almost siku 3 hv...afu hapo miez ka mitatu nyuma nmetoka lock up pande za Tarime kwa kosa la.......ntarud kueleza ilkuaje nkaingia na nlchokutana nacho huko
 
Back
Top Bottom