Umewahi kupigwa hadharani? Mimi yalinikuta!

Mimi Mtaani kwetu walikua wananiita bluu siri maana enzi hizo ndio zmetoka jojo za chata ya bluu siri nilikua fiti sana kwa mateke, sasa bwana ilitokea kuna dogo alikuja jirani mgeni nakumbuka zilikua zmebaki siku chache krismas

Mi niliwakuta wanacheza mpira nikaomba namba wakanininyima nikaingia kwa nguvu mbaya zaidi nilikua golini nikaudaka nikaukatalia kumbe mpira ni wayule dogo

dogo akaja kuniomba mpila nikagoma huku naondokanao nikaona anavimbisha kifua nikamsukuma nikaona anakunja shati baaaasiiii nlikua mkorofi balaa nikamfata yaani sjui nlirusheje teke

Teke ya kwanza ikashikiliwa nikaanza kuburutwa kama nyoka mwishie nkaanguka jamaa kaniweka chini nikajaribu kutumia mabavu kumgeuza nikapigwa ngumi maeneo ya sikio nilijua nakufa nililia kwa nguvu huku nikiomba wamtoe nmetosha

hapo hakukua na watu wakubwa waliokuepo wote madogo tu kilichonsaidia alipita baba mmoja akatuachanisha kwa fimbo lijamaa ndo kukimbia mimi npo hoi huyo moja kwa moja nyumbani.

tokea hapo sjagombana tena


exalioth
jf geita
 
Una kipaji cha uandishi.

Nimecheka mpaka mbavu zimeniuma [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
[emoji23] huku kata rufaa
 
Kuna watu wana mfupa mmoja kwenye mkono huyo akikupiga ngumi lazima akushushe hata kama anamwili mdogo
 
Nimecheka sana.
 
Mimi sinaga nguvu ila na hasira kali sana.Nilichokuwa nakifanya ntakutemea mate usoni au ntakumwagia mchanga usoni then mbio nyingi sana nyumbani.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Daah nimekumbuka mbali sana Shule ya Msingi Yombo Dovya
 
Kumbe dogo kabisa sisi tumezaliwa ata jojo hazipo dunianj
 
Mimi sinaga nguvu ila na hasira kali sana.Nilichokuwa nakifanya ntakutemea mate usoni au ntakumwagia mchanga usoni then mbio nyingi sana nyumbani.
Kama mimi tu. Ilikuwa unaweza kunipiga sana ila ukiniachia lazima nirushe mawe na matusi juu. Ukifanikiwa kunikamata tena nakuomba msamaha, upenyo ukipatikana nduki na mitusi tena
Ila utoto raha sana.
 
Reactions: EEX
Nakumbuka nikivyokuwa form 1 mwaka 2004 kuna muhuni alikuwa form 3 alikuwa anapenda sana sifa hasa akiona madem

So kuna siku alinikuta nakula mihogo akaiputa na kuimwaga dah kiukweli sikuwa na nguvu na nilikuwa muoga lakin nilimtia kichwa yule muhuni mpaka kapandaisha mashetan mi mbio tangu siku hiyo nilikiwa maharufu kwa jina la mzee wa mashetan
 

Nikiwa Darasa Pili bana Kuna Binti alikuwa White Sanaa class, ana Dadaake Darasa la tano,Mwanaume nikaleta uhuni wa Kitaa Kwa Kuanza kumpiga Sound Classmate, Mtoto akawa hataki, nikawa na force, akanisemelezea Kwa Sistaake wa Darasa la tano.

Darasa la Pili na La Tano yapo Mkabala, ukiwa Darasani kwetu wa Darasa la tano unamuona,vivyo hivyo wa Darasa la tano, yule Sistaake akawa ananioneshea Kidole Kunionya na kuniambia nitaona tukitoka shule.

Basi Kwa Ujeuri na plus kupewa Bichwa na wanangu wa Kitaa Class kuwa Demu anakutisha vipi, baadae Mpe kichapo

Basi bana, baada ya Kengele ya Parade, na baada ya kuruhusiwa tu Dada Mtu akaniibukia Kwa Mbele, Niko na Wanangu kadhaa, tukacheka sana, Wanangu walivyo Mashabiki, wakaanza kunifungua vifungo vya shati na kunipa Bichwa, Dada katulia tuliiii, Mikono kaweka Kwa Nyuma, ananisikilizia tu Navyojazwa na Wanangu.

Kumbe Dada Kwa Nyuma kashika Mfagio wa Chelewa, e bana eeeh, ghafla akanijia, nilichapwa Jamani na Lile Fagio, Dakika tano usoni sitamaniki, nilikuja kuokolewa na Kaka Mkuu aliyekuwa anapita ile Njia.

Wanangu wale walivyokuwa Wasenge wote wakasepa wakati Kamanda wao nimeingia Matatani.

Yule Demu White classmate sijui yuko wapi.
Natamani nikutane nae Ukubwani, Kwa Lile tukio najua anaweza kunipa game Ukubwani huku akinicheka.

Since then Mimi Sijawahi Kupigana kabisa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Mimi tangia nikiwa mdogo mzazi aliniambia ukiona watu wanapigana kimbia ,ndo ikawa desturi yangu,wakianza tuuuh kupigana mimi nachukua marathon mpaka nyumbani.


Kwa kawaida shuleni nilikuwa mpole sana,sikuwa napenda ugomvi na mtu,nilikuwa mtu mkimya na mwenye maneno machache kuliko wanafunzi wote.
Nikiwa darasa la saba ,siku moja nikiwa darasani ,mara paaap nikaaanzisha ugomvi na binti wa watu ,nilikuwa najiamini kweli,kumbe nilipanda mtumbwi wa vimbwengo,nikaona ngoja na mimi nionyeshe ubabe kidogo wakati huo,kila mara naona watu wanapigana,aiseeeh kilinichonikuta nikasema sitaaanzisha ugomvi tena,mimi nilipigwa ngumi moja na mtoto wa kike uso ukavimba vibaya mno ,nililia mpaka ticha anakuja kunibembeleza ,akaona sio kesi akaninunulia na ubuyu,nikapokea na pole nyingi kwa wenzangu ,saivi nikiona kuna dalili ya ugomvi kutokea na slow down,ili niepukane na aibu.


Ile siku sitaisaaahau mabinti wa vijijini wana mikono migumu sana ,mimi ata skutumia nguvu ilipigwa moja nikawa naona [emoji93] [emoji93] [emoji93] [emoji93][emoji93][emoji93][emoji93][emoji93][emoji93][emoji93] tuuuh .
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…