satininus
Senior Member
- Feb 11, 2021
- 135
- 171
Mimi niliwahi mara kacha kulala stesheni ya Shinyanga kutokana na ukweli kwamba treni za kwenda na kutoka Mwanza(Locomotives) zilikuwa zinapita usiku hivyo mimi mara zote nilikuwa nashuka kutoka Dodoma mishale ya saa 6 usiku kwa vile wazazi walikuwa wanaishi Kahama nilipaswa nilale hapo stesheni ili kukicha niendelee na safari.
Sasa yaliyokuwa yanatokea usiku huo ni mengi kuna wenzetu wenye matatizo ya akili huwa wanalala stesheni na wana maeneo maalum katika moja ya mabenchi halafu usiku kucha wanaongea peke yao au kupiga kelele na kuvuta goso wakati mwingine bange, kundi la pili ni vibaka wanajifanya wasafiri ili kufanya timing ya abiria wanaochukuliwa usingizi ili wawaibie pesa ama mizigo, enzi hizo hakukuwa na simu za mkononi.
Hivyo ilifanya usiku uwe mrefu sana pia kulikuwa na baridi kali, kunguni, mbu na mende halafu pale Shinyanga choo cha abiria kilikuwa nyuma ya nyumba ya abiria halafu unakuwa kama unashuka bondeni yaani sijui ilikuwa ni kusababisha tafrani kwa abiria maana mazingira yote yalikuwa hatarishi bila ulinzi, mwanga wala chakula.
Hebu wadau nanyinyi tiririkeni.