Umewahi kukaa hoteli au sehemu na Kivulana cha tabia hii?

Nipo Restaurant moja maarufu katikati ya Jiji. Mbele yangu kimekaa kivulana ( ingawa anaonekana kuwa na umri wa kuitwa Mwanaume) kipumbavu.

Toka kimefika kinapiga kelele kwenye simu kuonesha kinatukana wafanyakazi wake, kina ongea deals kubwa kubwa za millions of money na mizigo mingi iliyopo Bandarini.

Hiki kijamaa kimegeuka kuwa kituko maana watu wamekereka wamechoka. Mmoja kamwita mhudumu kuwa akamwambie jamaa apunguze makelele watu wamekuja kula na kupumzisha akili.

Kijamaa kinatumia mbinu za miaka ya nyuma mikoa ya mbali kama Bukoba nakumbuka miaka ya late 1990s ndo tulikuwa sisi wa town tulienda na simu zetu za Motorrolla tunakuwa na beat la namna hii.

Ka ajamaa kanakuja kufanya fujo hizo hii ya 2020s. Kamening'iniza funguo kiunoni,kameshika simu mbili na power bank. Yaani kana ushamba mwingi sana.

Anyway....hayo yote hayatuhusu. Issue kubwa ni hizi kelele kanazopiga muda wote kakitukana wafanyakazi wake....kama kanao. Yaani kanaonesha kenyewe ni ka Boss...

Watu wamefikia hatua wameanza kucheka. Maana wanaona ni vituko tu yale yanayotokea hapa.

Nikawaza haya mambo kweli kwenye buses,daladala,ndege,train,meli hayakosekani? Abiria aliyejaa deassmuda wote wa safari? Unaweza tamani ashushwe au ushuke.
Punguza wivu na stress
 
Mi naona wala sio hizo kelele zake,wivu tu ndio unaowasumbua,kama wafanyakazi wanamzingua asiwakemee?,naona kama nyie ndio mmepanic vile
 
Back
Top Bottom