Umewahi kufikiri kuwa angel investor?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,529
Natambua kwamba kuna watu wengi ambao wangependa kuwa wafanyabiashara, wajasiriamali au hata wawekezaji. Pia wapo wengi ambao pamoja na kutamani hayo yote bado wanakuwa na changamoto ya kupata mitaji inayoeleweka ili waweza kufanya biashara.

Ukifikiri kwa utaratibu utaona kwamba katika maisha kila ambacho unacho kuna anayekihitaji na kile ambacho hana kuna mwenye nacho. Na njia rahisi ya kupata kila unachotaka ni kuwasaidia wengine kupata kile wanachotaka.Sasa nieleze kwa kifupi leo kuhusu Angel Investors na nihamasishe watu wawe angel investors.

Nisingependea sana nitafsiri kiswahili cha neno hili bali nitaeleza kila kinachofanywa na Angel investor katika lugha nyepesi. Angel investor ni mtu mwenye kipato kizuri ambayo hutoa mtaji kwa mfumo wa mkopo, uwekezaji au umiliki kwa biashara au mawazo ya biashara yaliyoko katika ngazi ya mwanzo kabisa na ambayo katika soko la mitaji ya kawaida hayaweza kupata uwekezaji wala mkopo.

Ni muwekezaji ambaye anakusaidia katika kipindi ambacho huwezi kusaidika katika soko la kawaida la biashara na pale biashara yako inapokomaa basi uwekezaji unaweza kubailika na kuwe sehemu ya umiliki, hisa, au ukalipwa kama deni. Kwa kawaida hawa huitaji kiwango kikubwa cha riba kuliko mikopo ya kawaida lakini hukupatia mkopo kwa masharti rahisi kidogo.

Watu hawa katika uchumi ni kama hawa walanguzi wa mikopo wanaokukopesha laki moja wanatka faida laki kwa muda wa mwezi mmoja. Tofauti ya hawa ni kwamba wanawekeza kwenye biashara na wanakusikiliza wazo lako na kukuuliza maswala ya msingi kama wawekezaji na wanataka uwapatie taarifa kuhusu maendeleo ya biashara, faida hasara na changamoto. Kwa maana nyingine. Angel investor anakuwa na wewe kama mbia na sio kama mtu ambaye anataka kukunyonya. Atataka faida kubwa ila kiwango cha faida itategemea na uzalishaji na jinsi utakavyoelezea wazo lako.

Angel investor anaweza kuwa mtu ambaye unamueleza wazo lako na badala ya yeye kuliiba na kulifanya mwenyewe anakuchukua na kukuajiri ulitekeleze lile wazo huku yeye akitoa mtaji. Unajikadiria kiwango chako cha uzalishaji pamoja na mshahara na unampa taarifa kwa kina na biashara inapokuwa kulingana na mkubaliano mnapeana equity/hisa ila muwe wabia rasmi. Mnaweza hata kuamua kuuza biashara na kugawana au ukaamua kumnunua yeye na wewe ukabaki na umiliki wote.

Kwa Africa/Tanzania kuna uhitaji mkubwa sana wa Angel investors hasa katika kuhamasisha dhamira ya kujiajiri,kuhamasisha watu kufikiri tofauti na pia kutengeneza fursa za uwekezaji. Ni ukweli usiopingika kwamba kuna watu wanahitaji kuwekeza hata laki moja kwa mwezi ila hawana pa kuwekeza na kuna ambao wanahitaji uwekezaji wa kiasi hicho hicho kwa mwezi ila sasa kukipata inakuwa shida.

Nasema hivo kama mtu ambaye nimepitia hali zote hizo za kutafuta sehgemu ya kuwekeza na kukosa na pia kutafuta wawekezaji na kukosa.Ni tatizo

Ni muhimu tutengenze mfumo wa Uchumi ambao utawawezesha vijana kupata fursa a kusisimua uchumi wetu.
  1. Je ungependa kufahamu zaidi kuhusu namna ya kuwa Angel investor?
  2. Je unahitaji Muwekezaji katika wazo lako la biashara?
  3. Je ungependa kuhudhuria Pitching session ambapo utapresent wazo lako la biashara kwa muwekezaji?
  4. Je ungependa kudhamini pitching sesion katika eno ulipo?
  5. Je ungependa Kushiriki katika pitiching session kama Muwekezaji?
Kama jibu ni ndiyo basi wasiliana nasi kwa Email:masokotz@yahoo.com Hakikisha katika Heading unaeleza iwapo wewe ni MDHAMINI au MWEKEZAJI(MWENYE MTAJI) au MJASIRIAMALI

Ni muhimu ueleze ulipo na aina ya biashara ambayo ungependa kushirikishwa ili uweze kualikwa kwenye Pitching Session Sahihi na kuepusha gharama kubwa za uandaaji.

Kumbuka mahuddhurio katika Pitching session ni kwa mwaliko tu na kwa wakti mwingine tunaweza organise one on one session ili kupunguza gharama za uandaaji.Daima tutakuwepo kuhakikisha hakuna utapeli, udanganyifu na ili kueleweshana kuhusu mfumo wetu.

Tunamuhakikishie muwekezaji kwamba PESA ZAKE ZITATUMIKA KWA MALENGO HUSIKA TU na Tunamuhakikisha Mjasiriamali kwamba tutamuunganisha na MUWEKEZAJI MWENYE UWEZO na NIA tu.WADHAMINI watapata fursa ya kufikia watu sahihi kwa gharama nafuu.

Mawasiliano yetu ni kwa njia ya EMAIL.masokotz@yahoo.com.Tafadhali tumaa taarifa za muhimu tu. Maelekezo mengine utapatiwa wakati unapotumiwa mwaliko.

Iwapo wazo lako halitapa muwekezaji sahihi, tutakuunganisha na taasisi nyingine ambazo zinaweza kuwekeza kiasi cha mtaji unaohitaji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom