Umewahi Kuchunguza kwanini Nyoka hamdhuru Mtoto!?

Umewahi Kuchunguza kwanini Nyoka hamdhuru Mtoto!?

Mwana Ilala

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2013
Posts
1,286
Reaction score
488
Hallo Wana JF,

Naomba kujua kutoka kwa yeyote yule Mwenye kujua kwa nn Nyoka hawadhuru Watoto.

Bibi yangu aliwahi kunisimulia visa Vingi vya Nyoka kukutwa akicheza na Mtoto. Na hakuna hata Mara Moja imeonyesha Mtoto kudhuriwa na Nyoka.
Nikamuuliza ni kwa nn, akanambia hiyo ni "NATURE/ASILI" Imeumbwa Hivyo. Ila akanipa tahadhari kuwa, Unapokutana na tukio kama Hilo ghafla Bin Vuu, Hutakiwi kupiga Kelele. Ukifanya hivyo basi hukasirika na Kumgonga Mtoto.

Akanambia kuwa vivyo hivyo nikimuona Nyoka akila Chakula kilichoachwa wazi au nikimuona Nyoka amekwea PiPa la Mbege huku akinywa Mvinyo ndani ya Pipa Basi Usije ukamshtua, kwani ukimshtua,hukasirika na kutemea huko Sumu.

Kwa yoyte mwenye uelewa Mpana naomba atupe elimu kuhusiana na jambo hili la kushangaza inakuwaje Nyoka amheshimu mtoto kiasi cha kucheza naye tu na kutokumdhuru!??

Nawakilisha kwenu wana Jf kwa ajili ya Upembuzi yakinifu.
 
sijajua kama ni kweli ila nadhani ni bahati 2 ya mtt kuto kundurika maana tuxha wahi kumuona mtt kang'atwa lakini sijajua kwa upana lakini 2kio hilo lilitokea
 
  • Thanks
Reactions: y-n
hata nyoka anazo akiri anaerewa mtoto ni mtoto kwamwe hawazi kushika lungu na kumkamua ndio maana hana wasiwasi na uhai wake.
 
Inasemekana adrenaline hormone inayozalishwa pale mtu anaposhtuka kwa kumuona nyoka ndio inasababisha ang'atwe kwani nyoka anahisi hatari inayomkabili na anajihami mapema. Na ndio maana inasemekana kama hujamuona nyoka na yeye kakuona hawezi kukudhuru, kwa kuwa hakuna adrenaline inayozalishwa. Wataalamu wanasema nyoka inahisi adrenaline inayozalishwa katika mwili wa binadamu.
Kwa watoto nadhani hiyo ishu ya adrenaline hormone ina-apply, kwa sababu hawajui hatari ya nyoka.
 
snake_1420944c.jpg
 
Uko very right ndio maana kuna baadhi ya watu wana uwezo wa kulina asali bila kuumwa na nyuki, unapo-relax na hizo adrenaline hazi-react LAKINI UKIWA NA HOFU KUNA ADRENALINE ZINAZOZALISHWA na ambazo hutoa harufu fulani na harufu hio huleta interpretation kwa either Mbwa, Nyoka, Nyuki na viumbe wengine kuwa something is wrong and you must act.....ndio pale sasa unakuwa attacked. Utasikia kwa mfano watu wanasema ukimuona SIMBA wewe tulia tu....au kwa issue ya mtoto ni kwasababumtoto yeye adrenaline yake iko chini sana......nimejaribu tu na mimi kueleza ninachokielewa
Inasemekana adrenaline hormone inayozalishwa pale mtu anaposhtuka kwa kumuona nyoka ndio inasababisha ang'atwe kwani nyoka anahisi hatari inayomkabili na anajihami mapema. Na ndio maana inasemekana kama hujamuona nyoka na yeye kakuona hawezi kukudhuru, kwa kuwa hakuna adrenaline inayozalishwa. Wataalamu wanasema nyoka inahisi adrenaline inayozalishwa katika mwili wa binadamu.
Kwa watoto nadhani hiyo ishu ya adrenaline hormone ina-apply, kwa sababu hawajui hatari ya nyoka.
 
The answer is simple: Law of Love applies. When you act lovely towards anything the reaction you receive is love. Unapomwona nyoka ukahamaki the impression he receives is that you've considered him a threat therefore anakuona wewe ni threat kwake vile vile, lazima ajihami.
 
smartapartments Sio nyoka tu,wanyama wengi hawawadhuru watoto,ni Mungu tu anawalinda kama anavyowalinda na magonjwa mbalimbali hata wale uchafu kiasi gani
 
Last edited by a moderator:
Ni kwasababu ya sense of INNOCENCE: Nitaeleza

Kwa kawaida mtu anapopata mstuko huexcrete hormones ambazo humfanya ajihami na kuwa tayari kushambulia wakati wowote. Kimsingi hutoa adrenaline, hii huongeza hasira, nguvu na mambo mengine kama hayo. Sasa.......... adrenaline hutoa harufu au hujenga muunganiko (Nashindwa kuuelezea kibiolojia) na kile kitu ambacho kitashambuliwa. Mfano mtu anapokasirika kama amemkasirikia mwingine, ile hormone humvuta na kumjenga yule anayekasirikiwa na hatimaye naye huanza kujihami. Ndo maana mtu akikukasirikia utajikuta na wewe unamkasirikia (We become suggestible to other people's emotions) au kulia unapomuona mwingine analia hata kama hujui ni kwanini analia.

Back to the topic: Kwa vile mtoto ana sense of innocence, akimuona nyoka, wala hatastuka na adrenaline haitakuwa excreted na hivyo kutomjengea hali wa kujihami. Jambo hili halitamfanya Nyoka naye kujihami so anaweza "kucheza" na mtoto bila shida na bila kumdhuru. But akitokea mtu mzima ghafla na anastuka na kuexcrete adrenaline, then huyo nyoka anaweza kumng'ata mtoto kwasababu ya "mistaken identity" (kama ulivoambiwa ukimstua nyoka atatema SUMU kwenye mbege)

Nimejibu kwa maelezo ya kawaida (a layman's knowledge)
 
The answer is simple: Law of Love applies. When you act lovely towards anything the reaction you receive is love. Unapomwona nyoka ukahamaki the impression he receives is that you've considered him a threat therefore anakuona wewe ni threat kwake vile vile, lazima ajihami.

..na hii ndio sahihi zaidi..is all about love or hatred. inacho sense kwako ni ile calmness filled with love kama ukimwona na usipo react vibaya km kumrushia mawe, fimbo n.k...vivileanaweza kusense hatred..
 
Kwa uelewa wangu wanyama karibu wote wana uwezo wa kudetect adrenalin(hormone of fight or flight) kwa hali ya kawaida ukipata kitu cha kuogofya adrenalin hutoka kwa ajili ya wewe kujihami ama kupambana nacho. Kwa mtoto hana uelewa juu ya hatari hivyo basi adrenalin yake haitoki na kufanya nyoka kutohisi hatari yoyote
 
Back
Top Bottom