Yondani anazidi kuzeeka lakini bado ana usela mavi

Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
14,239
22,674
Umofia kwenu.

Wakuu majuzi ilikuwa birthday ya yondani kama sikosei. Jamaa ni moja ya ma legend katika ligi yetu na bongo kiujumla.

Hivyo u_legend wake ilitakiwa iwe mfano mzuri kwa wadogo zake kina mzize lakini bwana mkubwa bado ana usela wa kizamani.

Achana na matukio yake mengi kama vile kumtemea mate asante kwasi. Pia kumpiga mayele teke la pumbu.

Majuzi pia alikuwa akimkanyaga max nzingeli wakati wa kuweka ukuta kuzuia faulo mpaka mtoto wa watu alalamika

"bro vipi mbona unanikanyaga nimekukosea nini?"

Mwenzie juma nyoso kaamua kubadilika kule ihefu kwa sasa ila huyu yondani bado msela mavi.
 
Aliyekwambia usela huwa unaisha kirahisi ni nani mkuu….!!!??? Hata wale madingi tunaokutana nao BAR wakiwa na mambo fulani ambayo hayaendani na umri wao ndo walikuwa wasela enzi zao…!!!

Usela ukishakuwa kwny damu hautoki kirahisi…!!
Basi tufanye tu sasa ameshindikana tu mkuu maana ana mambo ya kizamani hajui hii ni ligi bora namba 5 Africa watu wanaona uhuni wake
 
Basi tufanye tu sasa ameshindikana tu mkuu maana ana mambo ya kizamani hajui hii ni ligi bora namba 5 Africa watu wanaona uhuni wake
Hapo kwenye ligi bora namba 5 Africa, nitakupinga mpaka nakufa.
Ligi bora namba 5 Africa ambayo hatuna hata refa mmoja kwenye michuano yoyote ya CAF, achilia mbali FIFA.

Wabongo tunapenda sana vya kwetu, ila ukweli sisi sio bora kwa chochote, labda kuneng'emua.
 
Back
Top Bottom