Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Hivi majuzi nilienda TRA kulipa kodi nikaambiwa kuna gari sijalilipia kodi ya mapato na motor vehicle kwa muda wa miaka kumi kwa hiyo natakiwa nilipe hilo deni.
Gari hilo lilishakatwakatwa na watengeneza majiko miaka kumi iliyopita na kwa muda huo wote halikuwa barabarani, wadau hii imekaaje utalipia kodi kitu kilichotupwa zamani.
Mimi binafsi naishauri serikali kama gari linadaiwa kodi ama motor vehicle licence walisubiri barabarani wakilipata walikamate sio deni la gari moja lilete tatizo kwa mlipa kodi, nasikia kuna watu walinunua magari ama gari lakini wamekamatiwa magari kwa deni la gari lingine.
Ukikamua ngo'mbe maziwa kwa kulazimisha matokeo yake utakamua damu.