Siku moja Padre mmoja na sister walikuwa safarini, usiku uliwakuta katika mji mmoja wa kigenihivyo wakalazimika kutafuta mahali pa kujihifadhi ili kutakapokucha waendelee na safari yao.Walitafuta sana lakini wakapata hoteli moja tu iliyokuwa imebaki ambayo kulikuwa na chumba kimoja tu tena chenye kitanda kimoja.Wakalaza gari yao kwenye fensi na kuamua kulala kwenye chumba hicho huku wakitenganishwa na mto wa kulalia katikati yao. Asubuhi waliamka mapema sana na kukuta gari yao ikiwa badokwenye fensi, geti limefungwa na mlinzi haonekani. Padre kwa kuona wanachelewa, alimwambia sister kuwa anataka aruke ukuta ili akalifungue geti kwa upande wa pili ambao ilikuwa rahisi kutoka...Sister akasonya, "Nyoo ulishindwa kuruka mto jana usiku utaweza kuruka ukuta?"