Umeshindwa kabisa kuacha kupiga Pu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeshindwa kabisa kuacha kupiga Pu?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Mar 15, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,619
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  KARIBUNI sana rafiki yangu katika uwanja wetu ambao kwa namna moja ama nyingine umebadilisha maisha ya wengi. Inawezekana hata wewe umepata kitu fulani kupitia hapa, maana kila kukicha nimekuwa nikiandika mbinu mpya za kukabiliana na changamoto zilizopo katika uhusiano.

  Hebu niambie...umeshawahi kujichua? Mara ngapi? Bado unaendelea na mchezo huo? Vipi, umewahi kusikia watu wakizungumza kuhusu suala hilo? Najua unaona aibu, hasa kama una tabia hiyo. Usiogope rafiki yangu, leo nitazungumza na wewe taratibu halafu mwisho kabisa nitakuacha na tabasamu la nguvu!

  Ndugu zangu, wakati mwingine kuna mambo magumu kidogo ambayo baadhi ya watu wanayaonea aibu, lakini yanaendelea kuwa tatizo kwa watu wengi. Leo tutazungumza. Amini usiamini, asilimia 90 ya wanaofanya mchezo huo, hawapendi hata kidogo.

  Kila wanapomaliza kujiridhisha huahidi kuacha, lakini baada ya saa kadhaa kupita, wanarudi kule kule. Kama una tabia hiyo, utakuwa unanielewa vizuri zaidi juu ya kile ninachokizungumzia hapa. Hebu twende tukaone.

  KUJICHUA NI NINI HASA?
  Kwa Kiingereza tendo hili linaitwa ‘masterbation’ likiwa na maana ya kupiga punyeto. Hapa nimetumia kwa ulaini kabisa; kujichua. Lugha nyepesi na rahisi kufikika kwa wengi ni kujiridhisha! Ni kitendo cha mtu kujichezea kimahaba huku akivuta hisia za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi anapomaliza haja zake.

  Namna ya ufanywaji inategemea zaidi na jinsi ya mazoea. Wapo wanaotumia vifaa bandia (artificial) na wengine vifaa halisi kama aina mbalimbali za matunda ambazo zinafanana na sehemu pacha!

  Wengine wanatumia njia wanazojua wenyewe, lakini wanaume wengi wanatumia sabuni lengo hapa ni moja tu, unatakiwa kufahamu kwamba namaanisha kujiridhisha.

  INAWEZEKANAJE KUJIRIDHISHA?

  Ni rahisi sana kumaliza tendo la huba kwa kujifanyisha mwenyewe. Silaha kubwa inayotumiwa na waathirika ni kuwavutia hisia watu wa jinsi pacha wakati tendo husika likiendelea kufanyika.

  Habari mbaya kwa watu wenye mchezo huu ni kwamba, kwanza wakishaanza, inakuwa vigumu sana kuacha. Inashindikana kwa sababu ni jambo la aibu. Si rahisi kupata ushauri kutoka kwa watu maana ni aibu pia kumweleza rafiki yako juu ya mchezo huo.

  Kutokana na hilo sasa, kinachotokea ni kwamba ‘waumini’ wa mchezo huu wanaendelea kuwa watumwa kwa maisha yao yote. Hapa chini tutaona kwa undani jinsi tatizo hili linavyoumiza vichwa vya wengi.

  Pamoja na kwamba lina ugumu kujadilika, lakini hapa katika All About Love kwa kutumia lugha nyepesi ya kirafiki bila kuchafua hali ya hewa tutakwenda sawa. Swali lako la kujiuliza kabla hujaendelea kusoma, ni je, upo tayari kuacha lakini unashindwa?

  Ni kweli hutaki kuwa mtumwa wa mchezo huu hatari? Zipo athari nyingi sana rafiki yangu ambazo nitazieleza hapa chini. Kama ni kweli unataka kuacha au huna mchezo huo lakini unatambua kwamba, mwenzi wako anafanya, endelea kusoma ili upate elimu hii ambayo huwezi kuipata mahali popote zaidi ya kupitia gazeti hili la Risasi Mchanganyiko.

  CHANZO NI NINI HASA?

  Jambo la kushangaza ni kwamba, hakuna mdau wa mchezo huo ambaye amefundishwa jinsi unavyofanywa. Wengi wameanza wenyewe, tena wengine bila kujua nini kitakachotokea, lakini baada ya matokeo kuonekana, ndiyo mwanzo wa kutopea huko.
  Kwa vijana wa kiume, wengi huanza tabia hii wakiwa kwenye umri wa kubalehe. Mara nyingi hutokea asubuhi wakati wa kuamka, usiku wakati wa kulala au bafuni wakati wa kuoga.

  Kwa kawaida, mtu anapokuwa katika sehemu ya utulivu kwa maana ya kupumzika, wakati mwingine mkono unaweza kutembea huku na huko kwenye mwili na mwisho wake bila kutegemea mhusika anajikuta ameshaingia kwenye mchezo huo.

  Huwa kama mzaha, akiwa hajui hatma yake, lakini msisimko anaoupata ndiyo unaomchanganya na mwisho wake anashangaa kila kitu kimemalizika. Unajua atakachosema? Sikia: “Mh! Kumbe ndiyo mwisho wake ni hivi? Lakini kama nimesikia starehe hivi...”
  Hiyo hutokea pia wakati wa kuoga, ambapo wakati wa kujisugua kwa dodoki, msisimko ukitokea, madhara yanakuwa kama nilivyoeleza hapo juu.

  Wenye umri mkubwa au wa kati, huanza tabia hii hasa baada ya kuanza mchezo wa kuangalia video za kikubwa wakiwa peke yao. Kwa sababu wanachotazama kinahusisha msisimko wa mapenzi, basi bila kutarajia hujikuta tayari!
  Hii inafanana pia na kwa watoto wa kike, vyanzo nilivyoeleza hapo juu pia husababisha kwa karibu sana.

  Sababu nyingine ni kunyimwa au kutotoshelezwa kimahaba na mwenzake. Marafiki bila shaka mnanielewa vizuri...kama nilivyosema lugha inayotumika hapa ni ya kirafiki zaidi, hivyo kama kuna jambo hujalielewa sawasawa, usisite kuniuliza kwa mawasiliano yangu yaliyopo hapo juu.

  Ni hamu yangu kuendelea kuelekezana juu ya tabia hii, lakini kutokana na ufinyu wa nafasi, naomba niweke kituo kikubwa hapa. Usikose wiki ijayo, maana ni muhimu zaidi kwako.

  Tutaona madhara yanayoweza kupatikana kwa mtu mwenye tabia hiyo, jinsi tatizo linavyokua na kubwa zaidi; NAMNA YA KUACHA UTUMWA HUU. Tafadhali usikose.

  Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers, ameandika vitabu vya True Love na Lets Talk About Love vilivyopo mitaani
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kumbe ndio wanavyo fanya kina nanihiii!sasa wale wanao pewa mpaka wakambia wake zao kwakua hashindano hawaya wezi wale nao tuwaweke wapi.
   
 3. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Shosti kwani wacomoro hawafanyi hayo? mbona nasikia wao ndio wanaungozaa?lol
   
Loading...