Umeshawahi kukutana na balaa la nyoka?

Na akipiga mara tisa mfulurizo ndipo, huishia nguvu, Wale wanao kamata nyoka wengine hutumia kioo, cobra akiona picha yake kwenye kioo, huanza kikgonga akizani nyoka mwingine, ila akisha fikisha mara tisa huishiwa nguvu, ndipo wakamata hutumia nafasi hiyo kumkata na kumtoa meno.
 
Sijawahi kujua hili
 
Narudia tena mkuu...
Kama hujamkanyaga au hujamzuia kuingia shimoni kwake cobra kamwe hawezi kukufuata akudunge.
Nimeishi maeneo yenye cobra na nimewahi kuua cobra wakubwa tu nikiwa peke yangu.
Ukimpiga nshingo aliyoinyanyua na kuitanua huwa anajizinga kwenye fimbo na habari yake inaishia hapo
 
Ulivyoandika Swila umenikumbusha mbali sana Gereza, Ushora [emoji13][emoji13][emoji13]
Na swila ni jamii ya cobra, ila huyu ukiktana nae kwenye 18 za huwa anafukuza ili mradi tu akugonge, na kama akikugonga huduma ya kwanza kama iko mbali andika usia.

Huyu nyoka alisha wahi nipandia juu ya mti aje kunigonga, kilichoniokoa ujana tu nilidandia tawi la mti mwingine wa karibu kama nyani wafanyavyo, nikadanda chini nikakimbia.
 
Hapo kwenye kumrushia fimbo ndipo ulipofeli ila sababu umesema ulikuwa darasa la 5, mi nlikuwa na mfuata namchapa hadi namuua.

Ngoja kinupe kisa kimoja......
siku moja tumetoka kanisani mida ya saa saba mchana, tumekaa nje kusikilizia msosi nje kulikuwa na karundo kadogo ka matofali ya kuchoma sina hili wala lile nimekaa jirani kabisa na hayo matofali kuja kuhamaki nyoka mreefu wa rangi ya kijivu kilichokolea akamkosakosa kuku yupo kwenye yale matofali nikachukua fimbo ngumu nikaanza kupangua tofali moja baada ya jingine nikamuona nlichofanya sikumpiga nikamminya kichwani na ile fimbo kisha nikamshika shingoni jirani kabisa na kichwa kumuinua nalingana nae urefu, maza kuona alipiga ukunga hadi majirani wakajaa 🤣🤣🤣

Anyways kukamata nyoka nlifunzwa na wachina maana nlikulia kambi ya jeshi ambapo wachina waliishi kama wakufunzi wa ndegevita. Kipindi hicho nlikuwa kidato cha tatu.
 
Ni kweli mimi ilinikuta nikiwa moshi 2005 majira ya mchana nimezunguka mbele ya nyumba kuchota maji kwenye pipa lilikuwa linakinga maji ya mvua basi nikiwa nimeinama nachota maji naangalia pembeni yangu namuona cobra mkubwa sana wa kijivu katunisha shingo yake ananiangalia jamani nilipiga kelele kubwa mpaka cobra mwenyewe akachanganyikiwa na kukimbia kupanda kibarazani anatafuta pa kujificha akazama ndani kupitia chini ya mlango tukaziba na dekio ikabaki nafasi kidogo akaenda kutafutwa mkamata nyota akazama humo ndani alimtafuta na hakufanikiwa kumuona huyo cobra.
 
Mwisho ilikuwaje?
 
Mwisho ilikuwaje?
Mwisho ndo hivyo cobra hakuoneka tukahisi labda alitumia nafasi iliyobaki kutoka nje maana tulivyoziba tuliondoka kwenda kumtafuta mkamataji . Lakini angekuwa wa kuning’ata basi ingekuwa hivyo maana nilisimama karibu yake kabisa na nilivyomuona nikaanza kupiga kelele sikusogea hata hatua moja zaidi cobra ndo alianza kukimbia nilikuwa darasa la sita,imagine angekuwa nyoka aina nyingine basi ningebaki historia tuu.
 
Cobra usipomkanyaga hakung'ati hili nina uhakika nalo 100%
 
Yeah ni kisanga sana, mpaka nimecheka nikikumbuka mambo yake enzi hizo kwenye mashamba ya Gereza Ushora daaah! 😝😝

Unawafahamu Kanga na kware?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…