Umeshawahi kukata tamaa?

Yna aika

JF-Expert Member
Aug 29, 2017
349
1,010
Mimi nimekata tamaa, nimefika mahali ambapo sioni mbele, nipo mahali ambapo ni kama jangwa sioni tumaini kabisa, nimechoka sana.

Mama yangu anaumwa kansa, ana fight nayo sana sijui ni kansa ya nini ila imesababishwa na kidonda, alikuwa na kisukari akapata kidonda na icho kidonda hakijapona hadi kimeleta kansa. Tumeangaika mahospitalini sana na sasa yupo kwenye tiba ya chemotherapy

Nimetumiwa message leo kuwa hajashinda vizuri kabisa, natakiwa kwenda. Moyo unaniuma sana mama yangu bado kijana tu.

Nina mambo mengi siwezi elezea yote, nimefika mahali nimekata tamaa kabisa

UPDATES:
Wakuu mbarikiwe kwa kunitia moyo katika wakati ule mgumu niliokua nao sana,
Hakika hatutakiwi kukata tamaa,kukata tamaa ni dhambi tunatakiwa kushukuru kwa kila jamno ingawa wakati mwingime haiwi rahisi lakini yatupasa kushukuru tu Mungu yeye ni mwema siku zote.

Huu uzi apo chini nmeusoma wote na kila mtu anapitia changamoto zake katika maisha na kukata tamaa ni mwiko.
Mimi sitokata tamaa tena wala sitaruhusu ayo mawazo yanijie,
Na mama yangu anaendelea vizuri sana tunaamini kua atapigana na cancer na atatoka akiwa mshindi

Mbarikiwe

Ni kipindi gani kigumu kimaisha ulishawahi kupitia ambacho huwezi kusahau na kilikupa hasira ya kutafuta pesa kwa nguvu?
 
Pole Sana Kwa Kuuguliwa Na Mama Kupitia Hapa Tunakutia Moyo Sana Usiwaze Mabaya, Kumbuka Ni Mitihani Tu Ya Maisha Itakwisha
 
Mama yake Magufuli hata kula hawezi lakini Mkuu anaendesha nchi,pale ambapo unafika mwisho wa akili ya binadamu basi Mungu ndipo anaanzia.

Sasa ni muda wa kuwa karibu na Mungu,Mungu ni mwema...mtafute kwa sasa atakusaidia.
 
Pole sana Kipenzi... naamini kila binadamu hupitia Mitihani maishani mwake regardless ni Tajiri au Maskin wote tunapata mitihani iwe ya Familia, Mahusiano, Kazi, Marafiki, Maradhi/Ulemavu n.k.

Furaha na Huzuni zote ni hali, huwezi kuwa na Huzuni maisha yako yote, zipo siku ambazo utafurahi.. Na huwezi kuwa na Furaha sikuzote ipo siku utapata Huzuni, ndo Maisha yalivo.

weka Imani yako kwa Mungu, amini kwamba Mungu anakupenda sana na hakupi mtihani usioweza kuukabili, ww ni Jasiri. chochote kinachotokea maishani mwako ni kwa Faida yako, japo inauma sana na mda mwingine unafikia hadi kukufuru Mungu kwamba hakupendi, kakusahau au Hayupo lkn kumbuka binadamu hatuna uwezo kujua Future yetu na yaliojificha!

huenda kuna jambo Mungu anakunusuru nalo ambalo ilikua ikupate siku za mbeleni lkn kwa huruma yake anakuepusha nalo japo process yake imejaa uchungu na maumivu

Unaweza ukachukia kitu kumbe ndio Kheri kwako, na unaweza ukapenda Kitu kumbe hakina Kheri kwako, Mungu ampe Afya mama yetu, Usiache kumfariji na kumuombea Dua.
 
Pole Sana usikate tamaa hata Kama huwezi kibinadamu endelea kupambana.Jaribu Hadi tiba mbadala,
.mfano juicy ya majani ya tunda la mstafeli usaidia pia
 
Pole sana. Usikate tamaa. Usimpe shetani nafasi. Mungu yupo. Atakufuta machozi very soon.
 
Pole sana ndugu kwa kuuguza ila ndio mipango ya mungu na hatupaswi kukata tamaa kwa namna yoyote ile ndugu, wahenga wanasema masikitiko kila mtu ana yake na masumbuko yana mwisho wake.
 
Weka namba tukuchangia bukubuku angalau upate nauli Ndugu yetu. Na pole sana. Usikate tamaa Mungu yupo.
 
Pole sana OP.

Kuna kipindi unaweza ona unapitia mambo magumu hadi unahisi matatizo yote ya dunia nzima ni wewe umepewa uyabebe.

Lakini kitu ukishawashirikisha watu (kama ulivofanya) tegemea kupata relief.
Upite kusoma comments usiteseke pekee yako, tupo pamoja na wewe.
 
Huyo anayeendesha nchi kwenda wapi?
Pole sana mleta mada.Mungu atende jambo kwa mama yako.
Mama yake Magufuli hata kula hawezi lakini Mkuu anaendesha nchi,pale ambapo unafika mwisho wa akili ya binadamu basi Mungu ndipo anaanzia.

Sasa ni muda wa kuwa karibu na Mungu,Mungu ni mwema...mtafute kwa sasa atakusaidia.
 
Kukata tamaa ni makosa miongoni mwa makosa tunayo yafanya sisi binadamu.

Pole sana kwa kuuguliwa na mama, ila sababu hakuna mtu anaejua kesho yake, kwanini ukate tamaa, pambana mpaka nukta ya mwisho kumipigia mama yako.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom