Umeshakutana na watu aina hii?

Umeshakutana na watu aina hii?

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,270
Je wanaJF, umewahi kukutana na watu wenye wivu mkubwa wa kitu ulichonacho?Watu hawa hutumia saikolojia ya kuponda hicho kitu chako ili ujisikie vibaya na kuchukia kumbe wanaonyesha mauwivu yao tu.
Kama umenunua gari watasema:
'Unaringia sana hilo gari eh? Unaringia kaburi? Nyumba hata hujapaka rangi eti wanunua gari.'
Ukijenga nyumba utawasikia:

'Hio nayo ni nyumba? Nyumba ziko Masaki, sio hicho kibanda chako cha kuku!'
Uwe na binti mwadilifu na anayemudu vizuri masomo yake, maneno yataenda hivi:
'Hana lolote huyo. gesti ndo nyumbani kwake.Si ajabu ana ngoma hapo alipo.
Ukiwa na mke mwenye bidii na mchapakazi utasikia yafuatayo:
'Mwanamke anaringa kama nini sijui, tena mnafiki sana. Tena kamkalia mumewe ile mbaya!
Nk nk
Umeshawasikia au kukutana na watu wa aina hii?
 
Ukifukuzia demu mkali utasikia "aah! Huyo nilishampitia
 
Na watu wa aina hiyo kwa sasa ndio wengi:lol::lol::lol:
 
Ia nawewe hupaswi kuishi kwa kuwafuata hao...achana nao na komaa kivyako
 
ukipika maharage watasema umefulia,ukipika nyama watasema unajifanya una hela...
 
Wakiona biashara zako zinaenda vizuri nawe pia unapendeza hawaachi kusema wewe mwizi.
 
Huu ni ushenzi. Ukiwa unafuatwa na boyfriend mtanashati na mtulivu anayejiheshimu .. utasikia huyu mademu wake kibao wameshakufa kwa ngoma. Jamani acheni!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom