Umeshakutana na shida gani kwenye gari lako upewe suluhisho?

Mercedes benz c class w204 yenye M271 engine ina ulaji mbaya wa mafuta (high fuel consumption), inakula kati 6.5-7.2km/litre mjini.

Nimefanya au kucheki vifuatavyo:
Diagnosis (hakuna error au tatizo limeonekana kwenye engine au gearbox au components zinazoendana na hiyo mifumo, hata values ziko poa)
Service (engine oil, filter, air filter, ac filter)
Plugs zimebadilishwa
Alignment, tyre pressure pia iko sawa

alternator pulley haiko sawa ni ya kubadili ila bado haijabadilishwa (sina hakika kama hii ni sababu au la!)

Sijagusa oxygen sensor wala MAF sensor sababu mashine haijasoma chochote ila forums huko mbele kuna mtu alisema ilileta mabadiliko makubwa baada ya kubadili MAF sensor.

Msaada please kwa mtu mwenye idea au uzoefu wa kitu kama hiki kabla sijachokonoa gari
Nangojea majibu ya hii kitu, mimi niko na Subaru Forestet 2008, tangu nije Dar inakula 6.8 - 7.2 km/L. Hizi foleni zinachangia huu ulaji?

Ila nikiwa Moshi inafika mpaka 10.5 km/L
 
Toyota Ist inapoendeshwa ikipiga bamz hasa zile bamz ndogo-ndogo ikiwa speed, nasikia kelele(kelele kama za upepo unatoka) kwenye tairi la upande wa dreva mbele, kisha gari inawasha taa ya check Engine na inazima. Ukiwasha inaendelea. Baada ya muda inatokea tena. Shida ni nina wakuu?
 
Gari yangu ina kawaida nikiwa kwenye jam au popote pale nikiwa nimesimama na gari ikiwa kwenye gear nikikanyaga break ina vibrate, na pia nikkwasha A/C huku gari ikiwa imesimama inq vibrate
 
Ka Ushakutana na shida yoyote kwenye gari yako ikakutatiza share Hapa Usaidiwe
Toyota Ist inapoendeshwa ikiwa kwenye foleni mwendo mdogo sana inazima redio kisha inawaka dashboard inawakataa zote gari inazima na kisha ukiwasha gari inawaka na kwenye mwendo usio wa foleni haiizimi nini tatizo?
 
Gari yangu ina kawaida nikiwa kwenye jam au popote pale nikiwa nimesimama na gari ikiwa kwenye gear nikikanyaga break ina vibrate, na pia nikkwasha A/C huku gari ikiwa imesimama inq vibrate
Gari kuvibrate ukiwa umekanyaga brake ,shida huwa ni disk rotor,na vile vile ikivibrate baada ya kuwasha ac ,shida huwa ni engine mounting
 
Toyota passo, inawaka taa ya over speed na ikibadili gear inakua kama inastuka. Kwa hiyo inabidi ukiona inataka kubadili gear uachie pedo ndio ibadili. Shida yaweza kuwa ni nini maana nishabidili mpaka gear box.
 
Kimeo changu Duals leo kimenigomea ghafla

Natoka zangu posta nakwenda TbT kufika jangwani ikazima, nikatoa gia nikawasha ikawaka, kabla sijafika kigogo ikazima
Mwendo umekua ndio huo
Hapa nipo nimeipaki hapa kigogo napoza kiu nimtafute fundi wangu

Shida ni gani labda?
 
Honda CR-v, manual, year 2002

● Inakula sana mafuta
● Gari inakua nzito
● Inakosa nguvu kwenye kupanda mlima au ku overtake hadi unalazimika kushusha gear na kutumia gear kubwa 1 au 2 ili kukusanya nguvu na kupelekea matumisi makubwa zaidi ya mafuta
● ikifika speed 60 au 80 inaleta miss
● Taa ya SRS airbag inawaka na haizimiki

Shida itakua nini hapa?
 
Gari yangu ina kawaida nikiwa kwenye jam au popote pale nikiwa nimesimama na gari ikiwa kwenye gear nikikanyaga break ina vibrate, na pia nikkwasha A/C huku gari ikiwa imesimama inq vibrate
Nahizi ubadili Engine mount mkuu
 
Gari yangu nikipark, kwa siku 1 au 2, nikija kuwasha nasikia harufu kali ya petrol ndani na nje ya gari, tatizo nini?

Ila nikiitumia mfululizo nikiwasha sisikii hyo harufu, shida ni ikikaa hata siku 1 bila kuitumia, kesho yake ukiiwasha harufu inatoka
 
Hivi naweza kupata engine ya aina hii ya gari? Pia ningependa kujua bei na uzima wake,yaani sitapigwa
IMG-20240215-WA0024.jpg
 
Back
Top Bottom