Ukisikia milio hii kwenye gari yako jua kuna shida na sababu zake

geranteeh

JF-Expert Member
May 21, 2015
266
618
Habari za siku mabibi na mabwana kama ilivyo ada tunaendelea tulipoishia katika mada ingine tena.

Leo tutaelezea milio ambayo ukiisikia kwenye gari yako jua kuna tatizo na tatizo husika, Kiufupi unapowasha na kutumia gari sauti inayotakiwa kusikika ni ya engine au ya kitu ambacho lazima kitoe mlio kinapotumika mfano sauti ya wipers au feni either ya kiyoyozi au ya kupoza engine sauti hizo tunaweza kusema za kawaida kwenye matumizi sababu lazima zisikike pindi unaootumia gari yako na kiufupi kama ni mtumiaji wa hiyo gari kama kuna sauti tofauti lazima ujue au kama ni fundi anaweza kukwambia washa gari weka silencer akisikia tu anaweza kukwambia shida husika.

Kumbuka hutakiwi kupuuzia sauti yoyote kwenye gari yako huenda ni tatizo linaloweza likakusababishia madhara au hasara kubwa sana hapo ndo lile neno letu "Kama ningejua" huja kichwani mwako.

Nisikukawishe wacha niende moja kwa moja kwenye sauti mbalimbali nitajitahidi kuzifafanua kwa namna unaweza elewa na pia namna ya kutatua hilo tatizo.


1. Mlio kwenye tyre pindi unapofunga breki.

Pindi unaposikia mlio pale unapofunga break sababu huweza kuwa kalipa inasagana na rotor hivo jitahidi umuone fundi haraka sana. Lakini unaweza sikia huo mlio ukiwa hujakanyaga breki jua hilo nalo ni tatizo, chamsingi peleka gari yako ikarekebishwa kabla ya majanga zaidi.


2. Mlio wa swiswiswi kwenye tairi

Hii haina tofauti sana na mlio wa juu ila huwenda pia sababu ya
mlio huo ni kuachia au kulegea kwa bolt kwenye tairi yako na hii hutokea pia ukifunga breki au gari ikiwa inatembea nadhani madhara ya gari kuchomoka bolt sote tunajua hivo usipuuzie pia.


3. Mlio wa Pu pu pu kwenye bomba la moshi.

Hii ni pale unapowasha gari na ukaiacha silencer ambapo mlio huu unausikilizia kwenye bomba la moshi. Endapo utasikia mlio huu basi jua gari yako ina miss hivo basi kuna sababu nyingi zinazopelekea gari yako kuwa na miss kama vile plug za gari yako hazichomi vema au unatakiwa kubadilisha nozel za gari yako na sababu nyinginezo kumbuka endapo utapuuzia hili tatizo gari yako itaongezeka unywaji wa mafuta pamoja na kupelekea gari kukosa nguvu.


4. Mlio wa kugonga gonga kwenye matairi hasa unapopita kwenye mashimo.

Hapa naongelea milio kama mtu anatwanga kinu au pindi unapopiga shimo tairi kugonga mlio wa kustukiza ambapo mara nyingi huwa inakuonesha kwamba unahitaji kubadilisha shockup za gari yako kwani zinakua zinafeli hivo unahitaji kubadilisha. Lakini pia inaweza kuwa ni ball joint kuisha mda wake hivo unahitaji ku replace.

5. Mlio pindi unapokata kona na mara
Pindi unaposkia mlio unao sound ka ka ka ka pindi unapokata kona basi jua moja kwa moja kwamba unahitaji kubadilisha au kurekebisha cv joint ya gari yako kwa maana ya kwamba inaweza kuwa grisi imeisha kutoka na na raba kuchanika au unahitaji kubadili yote.

Hii mara nyingi husababishwa na vitu vingi lakini kikubwa ni vema kuwa makini na raba inayopatikana eneo hili pindi inapoisha basi huruhusu maji hasa tunapopita kwenye ma dimbwi hivo unahitaji kurekebisha kabla shida haijawa kubwa.


6. Mlio wa kukwangua pindi unapowasha wiper.

Watu wengi hawajui wakati sahihi wa kubadili wiper ya gari zao. Pindi unapowasha wiper haitakiwi kuwa na mlio wa kuumiza masikio bali unatakiwa usikie mlio wa ruber na kioo tu so ukiskia other wise basi jua unachuna kioo na itakuja kukugharimu kununua kioo kipya hivo ni vema kubadili wiper mapema.


7. Mlio usio wa kawaida kwa mbele kwenye boneti ya gari yako pindi unapowasha.

Gari yako kwenye engine kuna mikanda au belt nyingi ambazo zinaendesha vitu vingi mfano kuna belt ya kuendesha alternator, Water pump, power steering pump na mikanda hii au belt huwa zinaisha na kutakiwa kubadilishwa na ndo maana kuna kilometa kadhaa huwa inashauriwa kubadili hii mikanda lakini namna nyingine ya kujua kuisha kwa hii mikanda ni sauti so pindi unaposkia sauti isiyoeleweka ni vema kukagua hizi belt na kwa macho utaweza jua kwa kuona mipasuko kwa mbali kwenye hii mikanda so unapoona hivo jua belt inahitaji kuwa replaced.



IMG-20230616-WA0007.jpg
IMG-20230610-WA0014.jpg
 
Tunauza Spea za gari aina zote aina zote Taa, Mabampa, Milango, Show, Mountings, Engine, Gearbox, Radiator, shockups Nk. Tunapatikana ilala machinga complex tunaangaliana na msikiti wa songea Tucheki 0693163110, 0655513132 au
Kwa uzoefu wangu huwa mnasema hivyo tukifika hapo mnatupiga danadana au kutuuzia spea zilizochoka vibaya
 
Kwa uzoefu wangu huwa mnasema hivyo tukifika hapo mnatupiga danadana au kutuuzia spea zilizochoka vibaya
Mkuu naomba nikuelekeze kitu kimoja kuhusu spea za magari. Mteja huwa anauziwa kile anachokitaka mfano maeneo makubwa yanayouza spea dsm ni ilala temeke na tandale.

Spea za ilala ni used za dubai ila tandale na temeke ni used za tanzania yan wanakata magari hapa hapa so nadhani kuna jawabu umelipata kupitia hii reply maana nkiongea zaid naweza haribu biashara za watu

Karibu mkuu
 
Mkuu naomba nikuelekeze kitu kimoja kuhusu spea za magari. Mteja huwa anauziwa kile anachokitaka mfano maeneo makubwa yanayouza spea dsm ni ilala temeke na tandale.... Spea za ilala ni used za dubai ila tandale na temeke ni used za tanzania yan wanakata magari hapa hapa so nadhani kuna jawabu umelipata kupitia hii reply maana nkiongea zaid naweza haribu biashara za watu

Karibu mkuu
Mkuu, unaposema ukweli hakuna iharibifu wowote wa biashara.
Nadhani lengo la biashara ni pande zote mbili i.e muuzaji na mnunuzi wote wapate product/malipo yanayokidhi haja zao.
Sasa kama hao wauzaji kuna baadhi wenye janja janja ni vyema ukaeleza wazi humu ili waungwan wajue. O think that the whole point of this forum.
Kama ukiamua kuficha huo ukweli then inaonyesha picha kwamba na wewe ni mmoja wao wenye janja janja
 
Habari za siku mabibi na mabwana kama ilivyo ada tunaendelea tulipoishia katika mada ingine tena.

Leo tutaelezea milio ambayo ukiisikia kwenye gari yako jua kuna tatizo na tatizo husika, Kiufupi unapowasha na kutumia gari sauti inayotakiwa kusikika ni ya engine....

Mkuu Rear Axle ya Toyota IST new model naihitaji sana, na Gharama zako zikoje?

Pia Bearing za nyuma za toyota IST new model unauzaje kwa zote mbili??
 
Nimenunua spare parts sana mitaa ya Ilala kuna wengi ni kweli wana hizo za Dubai ila wengi pia wanazimua na hizo za Tandale na Temeke
Pole sana mkuu lakin nakushauri pia umshirikishe fundi wako pia unaponunua kitu
 
Back
Top Bottom