Mhh naomba kuuliza hivi Teddy Kalonga na Miriam Gerald ni wenyeji wa wapi vile????
wasukuma wana heshima sana kwa mwanaume, pesa sio isuue saana kwao,wanajua kupenda kweli kweli ila pia wanatabia ya kurundikana kwa ndugu.
Jamani mimi mbona Mwanza na Shinyanga huwa nakwenda mara kwa mara ila siwaoni?
Ni kweli wana adabu sana lakini zaidi ya yote wanajua mambo ya fargha,nafikiri wanafunzwa jinsi ya kuishi na waume zao.sihadithiwi ninae.
Julius unataka ugomvi na raia wa huko mahali(BK), NA ni wengi sana pia hapa ndani kuliko nyie wasukuma!Huyo wako katokea Bukoba na sasa anajifanya Msukuma. Au usikute katokea Ukerewe. Unajua Walerewe wengi sana wanatamanigi kuwa Wasukuma. Dizaini umepata kanyaboya wewe
wasukuma wana heshima sana kwa mwanaume, pesa sio isuue saana kwao,wanajua kupenda kweli kweli ila pia wanatabia ya kurundikana kwa ndugu.
Jamani punguzeni unazi kidogo najua kuacha haiwezekani.
Halfu Pakajimmy nilikuwa nimesahau kidogo na hii ni muhimu sana ukalijua.Jamani wasukuma wanakula msosi mwingi nakwambia unatakiwa uwe na bajeti kubwa sana ya msosi.Mwanamke wa kisukuma mmoja ni sawa na wanawake wananne wa makabila mengi kwa upande wa ulaji wa chakula.Ndio maana utakuta wanawake wa kisukuma wana miili mikubwa sana ukilinganisha na wanawake wengine.
Unaenda Mwanza na Shinyanga mjini ama??,Jaribu uende vijijini(wilayani) kama Meatu,Maswa,Kahama(maeneo ya vijijini),Malya,Tinde,Bukombe,Msalala,Buzilayombo,Bushilombo,Mwamashimba.Geita,Magu,Kwimba...Pia maeneo ya Nzega,Igunga n.k...Huko ndo utawaona hasa wamama wa kisukuma mkuu
Kiongozi,kwani kurundikana ndugu ni kosa??,hii ni ishara ya umoja,upendo na mshikamano(Sifa nyingine hii)...Hatuna mambo ya uchoyo na kujitenga sisi bana
Pia wamama wa kisukuma ni wachapa kazi hasa
Kabonde, nadhani amani inaendelea!
Lakini nadhani kula sana siyo shida kubwa saana ukilinganisha na matatizo ya wanawake wa makabila haya mengineyo!
Wasukuma tupeni jibu la hii tetesi ya Kabonde!
Hao kama wana damu ya Kisukuma basi lazima itakuwa imechanganyika na ya makabila mengine. Sio Wasukuma pure
Tedy ana ubaya gani kwani?ni binti mrembo,hard working,ana upendo.Teddy Kalonga ni msukuma Pure, Baba na Mama wote ni Wasukuma pure, nadhani ni watu wa Ntuzu zone (Bariadi, Maswa na Magu)
Kabonde, nadhani amani inaendelea!
Lakini nadhani kula sana siyo shida kubwa saana ukilinganisha na matatizo ya wanawake wa makabila haya mengineyo!
Wasukuma tupeni jibu la hii tetesi ya Kabonde!
Usawa wenyewe bado haujakaa vizuri chumba kimoja bajeti ya chakula tuaijua wenyewe,ndugu wanaanza kufurika hivi tutaweza kumudu maisha kweli.Halafu mtu kakaa kwako mwezi mzima hakuna anachosaidia akiataka kuondoka anaomba nauli fikiria unaishi Lindi itakuwaje ?
Usawa wenyewe bado haujakaa vizuri chumba kimoja bajeti ya chakula tuaijua wenyewe,ndugu wanaanza kufurika hivi tutaweza kumudu maisha kweli.Halafu mtu kakaa kwako mwezi mzima hakuna anachosaidia akiataka kuondoka anaomba nauli fikiria unaishi Lindi itakuwaje ?
Unaenda Mwanza na Shinyanga mjini ama??,Jaribu uende vijijini(wilayani) kama Meatu,Maswa,Kahama(maeneo ya vijijini),Malya,Tinde,Bukombe,Msalala,Buzilayombo,Bushilombo,Mwamashimba.Geita,Magu,Kwimba...Pia maeneo ya Nzega,Igunga n.k...Huko ndo utawaona hasa wamama wa kisukuma mkuu
Kabonde kwanza nadhani wewe ni MTANI WA KABILA HILI, unless if you prove me wrong!!Ni shida sana tena kubwa kuliko unavyofikiri,usisahau watakuja ndugus,majirani zake wa uko usukumani,rafiki zake wa zamani sasa niambie gunia moja la unga baada ya wiki lazima uende sokoni labda kama unalima ndio utawaweza lakini kama ni unga wa kupima dukani nakwambia utaongea mwenyewe barabarani.Unajua wasukuma wanavyopenda kula ugali mkubwa,
This is too general, sio wote, najua wapo ila sio mademu wote wa kisukuma. Nishabahatika kumuona mmoja ambaye yeye alikuwa anamdunda sana mumewe, by then nilikuwa kijana mdogo alikuwa anaogopwa mtaa mzima.
Huo ndio utamaduni wetu wasukuma mkuu,hayo ya ndugu kufurika unayasema wewe,lakini kwetu sisi pouwa tu,ni kama utamaduni tu sasa(sema kwa watu wa mjini wataona ni kero),nenda sehemu yoyote yenye wasukuma(maeneo ya vijijini ya wilaya za mikoa ya Mwanza,Shinyanga na kidogo Tabora,pia maeneo ya bonde la Usangu na Songwe-Chunya) utaona ni jinsi gani wasukuma wanavyoishi kwa umoja,upendo na mshikamano...Hakuna uchoyo wala kuwaza fulani atakula nini maana vyakula vipo(tunalima sana mahindi,mtama,uwele,viazi vitamu-manumbu)mang'ombe yapo(tunapata maziwa-mtindi wa kuchekecha na samli,nyama...pesa),pia tunalima Pamba na Alizeti tunapata hela za kutosha kiasi kwamba tunakuwa hatuna hata muda wa kuwaza kwamba aaargh hawa watu mbona wamekuwa wengi hapa nyumbani kwangu...Ukweli najivunia sana kuwa Msukuma aisee
Katika kila pool ya watu katika jamii, always kuna baadhi ya wachache ambao huwa hawa-conform. Katika hili, kama sample ni kubwa unachoangalia ni conformity ya majority.