Umeniharibia maisha! ...what?

Asante sana Lizzy........umesema yooote niliyotaka kuyasema. Ukweli kuharibiana maisha kupo na watu wengi wamekuwa victimize na hili. Ubarikiwe dia.
 
Pheeeeeeewwwww!.....well, well, well....kwa hapo kweli nimeona wapi "tofali" aka "Jiwe la msingi" la umeniharibia maisha lilitaka kuwekwa rasmi!

Nimekosa hata cha kuongeza bana, pole sana kamanda.

Sasa hapa mkuu unaweza kusema NIMEHARIBU MAISHA YA MTU?
 
Reactions: Mbu

daahhh hii kasheshe !
nimekosa hata la kuongezea
 
Reactions: Mbu
kaka unaonekana unaandika kwa hasira sana mpaka storuy imekuwa kama hatuelewi vizuri, pole mwaya hapo hujaharibiwa maisha wala nini, ndio kwanza umeanza nae, jipe mapumziko ili upone jeraha na uendelee na maisha, usimpe kichwa na kusema kaharibu maihsha yako mwili wako baado unao
 
Reactions: Mbu
Ngoja nikae pembeni kwanza mpaka hili sredi lianze maofu topiki....kuna watu humu nna hasira nao sana!

Subiri............!
 
Reactions: Mbu

Hapo bold hapo umenikuna ipasavyo. Na hii tabia wanayo sana wababa kumng'ang'ania mtu ili mradi amchezee tu huku akijua dhahiri hana malengo nae.
 
Mi binafsi sipendi malawama nifanyapo maamuzi yangu, kwa hiyo ningependa kuheshimu maamuzi ya mwingine akiamua, sio kulalama tu umeharibiwa maisha, kwani mzazi wako huyo? mtu umekutana nae tu ukubwani lets say una miaka 25 then ukae nae miaka miwili useme kakuharibia maisha? umesahau miaka yote 25 uliyokuwa mwenyewe mwenye furaha?
Cha muhimu ni kuangalia wapi ulianguka ili usirudie tena kosa, na umshukuru mungu kwa uzima wako
 
Naomba uwe unawafundisha na wadada wengine wasiojua haya, hasa mabinti wadogo wanaochipukia ktk mahusiano
 
Umeona eeehheee??

Na ukimkatalia kama alikua rafiki basi ujiandae huo urafiki unakufilia mbali, utanona tu anaanza kukuchunia nia, mwisho dah

Kwa kweli nawashangaaga sana wanaume katika hili na wala siwaelewagi kabisa.
 
Reactions: Mbu
Naomba uwe unawafundisha na wadada wengine wasiojua haya, hasa mabinti wadogo wanaochipukia ktk mahusiano
Mtu sononeka then anza maisha kwa sababu una moyo kama wengine, ila sio kulalama tu hadi kunywa dawa, for what umesahau hata wapendwa wako ulioishi nao tangu umezaliwa? hii ni kukufuru Mungu sasa... ndivo navochukulia maisha CPU
 
Reactions: Mbu
Maty mambo mpenzi wiki imeanzaje? naona na wewe umeanza kuwaulumu.

Na ukimkatalia kama alikua rafiki basi ujiandae huo urafiki unakufilia mbali, utanona tu anaanza kukuchunia nia, mwisho dah

Kwa kweli nawashangaaga sana wanaume katika hili na wala siwaelewagi kabisa.
 
Maty mambo mpenzi wiki imeanzaje? naona na wewe umeanza kuwaulumu.

Hahahaha lol, wiki imeanza vyema mpenzi, kuwalaumu ni lazima ili wajue wafanyacho si kizuri hata kidogo.

Imagine mtu anaanza kutaka kumdanganya mtu mzima maty akifikiri nina miaka 20 lol. Na kwa sababu nimeshapita huo umri wa kudanganyika mtu anakuchunia eti, mwe!
 
Mtu sononeka then anza maisha kwa sababu una moyo kama wengine, ila sio kulalama tu hadi kunywa dawa, for what umesahau hata wapendwa wako ulioishi nao tangu umezaliwa? hii ni kukufuru Mungu sasa... ndivo navochukulia maisha CPU

Nilipata nafasi ya kuongea na mdada mmoja anaenda kwa jina la Maty nilipoenda kule alipo kwa ajiri ya Seminar fulani hivi. Muda mfupi nilioongea nae nikagundua AMEELIMIKA bila kupita darasani. She's stable in her mind. Kuoa mtu kama huyu ni raha mpaka basi.

Nadhani na wewe ndo wale wale kama huyu Maty . . . lolz
 
Hahahaha na kupata mume muelewa kama wewe ni raha sana asee lol, unajua nini CPU nimegundua ukitendwa mara mbili tatu ukitoka hapo unakuwa mkakamavu kupita maelezo, ila inabidi na hata wewe ujue una makosa fulani ulichangia na sio kulaumu tu
 
good girl, i can see you are getting stronger and stronger
 
Hahaaa mie najifunza kwenu tu leo maana Mbu alishatuomba msamaha sie wenye mioyo dhaifu.

Hahahaha na kupata mume muelewa kama wewe ni raha sana asee lol, unajua nini CPU nimegundua ukitendwa mara mbili tatu ukitoka hapo unakuwa mkakamavu kupita maelezo, ila inabidi na hata wewe ujue una makosa fulani ulichangia na sio kulaumu tu

Wanaume wengi tunashindwaga hapa!! Sijui ni kwanini . . . ??!! Mi nimejifunza sana hapa saa hizi!!
 
Unajua wakati flani tunapingana na mioyo yetu vile inasema kabla ya kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi.Kuharibiwa maisha hakuji ghafla ni vizuri kujipa muda wa kutosha kabla ya kuchukua maamuzi mazito kama ya kumpa mtu moyo wako,mtu ambaye u will spend the rest of your life with him/her.

Zipo dalili au viashiria flani unaweza kuviona kwa mtu ambaye hayuko serious au mwenye tabia flani ambazo zinaweza kuwa mwiba huko mbele na hatimae kufikia hatua kusema "UMENIHARIBIA MAISHA".Usilazimishe mambo eti una hope mabadiliko flani kutoka kwa mtu wako ambaye tayari unaona moyo wako unauzito flani hivi.Chukua hatua sasa haitakuchukua muda kupona kuliko kuendelea na kitu ambacho baadae itakuwa majuto kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…