UMEME WAKATIKA UWANJA WA TAIFA!!!Ngeleja jiuzulu

Status
Not open for further replies.
Inasikitisha sana inamaana serikali haioni umuhimu wa mechi hii au alioko zamu tanesko ni mshabiki wa simba!
 
Ulipogoma wimbn wa taifa wakati ule wakamtimua Kaijage,leo vp atatimuliwa nani?
 
Ambulance yatumika kumulika baada ya umeme kukatika. Serikali gani hii? Kala sekunde hamna umeme
 
ni jambo lakusikitisha sana, serekali isiyojali maisha ya watu zaidi ya 60,000. Je wote watatoka salama uwanjani?
uaribifu wa mali?
 
Ni aibu nyingine yaikumba Tanzania katika wizara ya habari na michezo. Kwa nchi kama Tanzania yenye uwanja wa kimataifa, uwanja bora kabisa Afriica mashariki na kati umeme kukatika na kukosa jenereta. Imargine kama mechi ingekuwa inaendelea je ingekuwa? Kuna kila sababu ya wazirii wa nishati na madini kujiuzuru hata kama bosi wake (KIKWETE) ANAMKINGIA KIFUA. Kwani huu ni uzembe wa kpindukia hatukubali kuendelea na aibu ya namna hii. kumbuka mwaka 2010 wimbo wa taifa ulipogoma kuimba katibu wa habari wa TFFaliwajibishwa, Tunahitaji NGELEJA Awajibishwe
 
TFF muwajibike wenyewe, halafu ngeleja na timu yake pia wafuatie
 
FADHILA ZA MAGAMBA.. Imagine kungekuwa na viongozi wa nje mf: kagame si ni aibu tupu.. Mwenyekt wa magamba angekuwepo raia c wangeweza kumdhuru
 
Ni fedheha ,aibu na faradhuli!hivi waliokuwa wanacheck ile mechi huko majuu na mataifa mengine ya afrika wanatuchukuliaje!yaani basi tu!ila sitawaacha hivi!Shame upon TANESCO NA WAHUSIKA WAKE
 
Uongozi wa uwanja wa Taifa ni mbovu kabisa, generator zipo, zilikuwa hazina mafuta! can you believe it?
Kwa hiyo nani atajiuzulu?mlinzi au mtia mafuta wa uwanja?wewe huoni kama Mhando,Ngeleja,John Nchimbi ni watu wa kunyongwa?after 50years of independence?????ndio maana nasema bora mjerumani arudi alifanya ya maana kuliko CCM.Acha kutetea ujinga ndugu yangu kwa mtindo huu hata kama CCM ikipewa miaka 1000 hatutaendelea.mtindo wa kulindana hauna tija kwa taifa letu,leaders should be responsible!!!!
 
Bado najiuliza maswali tena magumu, je kama ndo zingekuwa zimebaki dakika 20 ili mpira uishe ingekuwaje, ama kweli hii nci haina viongozi kabisa..
Hiii ni aibu dunia nzima kwani ss4 na ss9 zinaonekana dunia nzima,
 
nani atawajibiswa juu yahilii sidi ya wimbo wataifa ilivo goma aliajibiswa jee? leo ni katibu au wazili nishati tunaizihilishia dunia utendaji viongozi tz ni 0 maneno mengii yasio endana na vitendo
 
Viongozi wetu wengi ndo wako hivyo, akiwa kiongozi kwenye idara fulani, anapewa bajeti ya kusolve matatizo yeye anatunza hela hadi mwisho wa mwaka anarudisha zilikotoka kisa anapewa mgawo! Hawa jamaa wa TFF wanatamaa kama nini, utakuta tokea kipindi cha tiketi zinapatikana kwa mazabe zile za elfu tano mtu unapata kwa elfu kumi.

Inshu kama hii ya standby generator watu hawataki kuachia hela kwa ajili ya mafuta, wanataka mgawo wote, hapo ana mshahara kila mwezi anakinga. Sasa unategemea kuna sheria hapo? Lets wait and see, no body will be charged against this.

Nilikuwa naangalia online TV, inatia kinyaa wakati nikitembea kifua mbele kuwa naona mpira wa nchini wa nchini, Tanzania ikijitangaza, mwisho wa siku nabakiwa na aibu. Hata kama hakutaakuwa na watu watakaoumia, lakini hii ni hatari sana tena sana!!

Harafu hawa Tanesco hata kama kuna mgawo but inshu ilikuwa imebaki dakika kama 10, lakini wanakata, how come? hujuma au ushabiki? Am scared with this swaga.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom