Baba_Enock
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 7,076
- 2,445
Bunge la MAZUZU!
Ndiyo tunajua tanzania yote iko kwenye tatizo la umeme lakini mahitaji na matumizi yake yanatofautiana huwezi kulinganisha madhara ya kukosa umeme hospitalini na kwenye bar kwa vile wote waliomo ni wananchi walewale. Jiulize kwanini waziri wa michezo aliomba radhi kukatika kwa umeme wakati wa mashindano ya Kagame na kwa nini wasiombe radhi kukatika kwa umeme jana Bunju au Kibaha kwa Mathias.
Mkuu unazungumzia aibu gani hapa?Wanatia aibu!!
Mzee hiyo powerful generator lazima itakuwa mitambo ya Dowans.Bunge halina powerful standby generator? Ukute hata lile la Ikulu halina mafuta mpaka umeme ukatike ndio wakimbilie mafuta pale BP!!!!!!!!!!
Sasa ulitaka ataje mifano yote na wewee?Kwa hiyo wewe unaona bunge na hospitali zipo level moja? Bunge na viwanda je? Bunge ndio linalohitaji umeme kupita kwingine kote hadi iwe aibu kukosekana kwake bungeni?
ukisikiwa na Chenge wewe?
Ndiyo tunajua tanzania yote iko kwenye tatizo la umeme lakini mahitaji na matumizi yake yanatofautiana huwezi kulinganisha madhara ya kukosa umeme hospitalini na kwenye bar kwa vile wote waliomo ni wananchi walewale. Jiulize kwanini waziri wa michezo aliomba radhi kukatika kwa umeme wakati wa mashindano ya Kagame na kwa nini wasiombe radhi kukatika kwa umeme jana Bunju au Kibaha kwa Mathias.
Aibu si kwa wabunge kukosa umeme ila aibu ni kutumia mshumaa, sawa na aibu ya uwanja wa taifa kutumi taa ya gari la ambulance wakati wa kukabidhi kombe. Inakuwaje bunge lisiwe na standby generator au taa ya kandili basi walau tochi kuliko kutumia mshumaa ambao ni hatari.
Lakini kwa upande mwingine mimi naona sawa tu kwa vile bunge linaangaliwa na mataifa mbalimbali ujumbe umefika hadi kwa wafadhili wetu na investors ambao Kikwete amekwenda kuwadanganya ili waje wakijua mapema kuna tatizo la umeme.
Naunga mkono hoja.Hii ipo kwenye hansard? Ilitokea lini? Hivi aibu ni wabunge kukosa umeme au wananchi? Kwangu mimi aibu ni pale wananchi wanapokosa umeme kwa masaa 18 kila siku. Wabunge nao ni wananchi, na hivyo nchi ikiwa kwenye shida ya umeme, kwa nini wao wawe spared? Unapoweka hilo neno aibu hapo, unakuwa kama unasema wao ni special group ambalo halitakiwi kukosa umeme...
Mafuta yalikua yameisha! Si bajeti ilikataliwa kupita na million 50 wameshatoa sasa we unafikiri pesa itatoka wapi tena!!WanaJF! Huo ukumbi wa bunge haunaga genereta automatic?