Umeme wakatika bungeni, waziri aomba mshumaa (aibu) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme wakatika bungeni, waziri aomba mshumaa (aibu)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Jul 22, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, ameomba kupatiwa mshumaa bungeni ili aweze kuendelea kuhitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake. Hatua hiyo imetokana na umeme kukatika mara nne bungeni hivyo kusababisha adha kubwa kwa mawaziri hao.

  Awali wakati Naibu Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu, akifanya majumuisho ya bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2011/2012, umeme ulikatika mara mbili.

  Hata hivyo wakati waziri Simba anahitimisha bajeti hiyo umeme ulikatika mara mbili zaidi hivyo kumfanya ashindwe kuendelea kujibu hoja hizo lakini Mwenyekiti wa Bunge, Sylvester Mabumba, alimtaka kuendelea ndipo aliposema: "Sioni; naomba mshumaa! "Mabumba alijibu: "Sasa tufanyeje?"

  Ukistaajabu ya musa njoo ujionee tanzania
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,878
  Likes Received: 83,359
  Trophy Points: 280
  Bunge la wala rushwa halihitaji umeme vinginevyo wasikubali kupokea rushwa toka Nishati ili kupitisha bajeti iliyojaa uozo mtupu. Bunge hili limeshapoteza heshima yake kwa Watanzania.
   
 3. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Bungeni sio Mbinguni, after all kuna matumizi ya nguvu za giza mle.
   
 4. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Wanatia aibu!!
   
 5. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Jamani tusisingizie nguvu za giza kwa matatizo ya uzembe wetu
  sidhani kama kuzimika kwa umeme kunasababishwa na nguvu za giza too low.
   
 6. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Watanzania kwa majibu mepesi mepesi una ubia na Kikwete nini maana yeye alisema siyo mawingu ya mvua anyeshe maji yajae.
  Tujaribu kuwa critical kidogo kwenye mambo ya msingi vinginevyo hatutaendelea milele.
   
 7. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii ipo kwenye hansard? Ilitokea lini? Hivi aibu ni wabunge kukosa umeme au wananchi? Kwangu mimi aibu ni pale wananchi wanapokosa umeme kwa masaa 18 kila siku.

  Wabunge nao ni wananchi, na hivyo nchi ikiwa kwenye shida ya umeme, kwa nini wao wawe spared? Unapoweka hilo neno aibu hapo, unakuwa kama unasema wao ni special group ambalo halitakiwi kukosa umeme...
   
 8. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  ukisikiwa na Chenge wewe?
   
 9. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ndiyo tunajua tanzania yote iko kwenye tatizo la umeme lakini mahitaji na matumizi yake yanatofautiana huwezi kulinganisha madhara ya kukosa umeme hospitalini na kwenye bar kwa vile wote waliomo ni wananchi walewale. Jiulize kwanini waziri wa michezo aliomba radhi kukatika kwa umeme wakati wa mashindano ya Kagame na kwa nini wasiombe radhi kukatika kwa umeme jana Bunju au Kibaha kwa Mathias.
   
 10. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mwaka 2009 wakati naenda shuleni kwetu Alqaem,ambayo ipo karbu na bungu,mkata maua wa bunge alichimbua kichwa cha mbuzi kilichozungushwa na ngoz,nan kasema uchawi haupo?
   
 11. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mkt: tuendelee,
  waziri: sioni naomba mshumaa!!!. Hivi kwa hali hii tutafika? Nimecheka sana kusikia hili. Ninacho furahia tanesco wanakta umeme kila kona haijalishi huku anaishi nani. Nitafurahi nikisikia na magogo nako unakatwa. Tuanze kufikiria njia mbadala za kujipatia umeme serikali imeshindwa kazi.
   
 12. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sasa hicho kichwa cha mbuzi kinasababishaje kukatika kwa umeme.
   
 13. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,468
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Viongozi wanapotanguliza maslahi yao binafsi,wakifikiri wao hawawezi kuaadhirika kwa lolote wanajidanganya.kuzimika umeme bungeni ni mfano mdogo.Kwa hilo sijui wabunge wamejifunza nini?je wataendelea kuwa mavuvuzela kuuga bajeti kwa wimbo wa asili mia 100?
   
 14. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kina nani
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  malawi wanatuzidi ujanja?
   
 16. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  kweli ni special yanapotoka yale mashangingi ya gari au yale mapesa ya kununulia magari mwananchi wa chini huwa anakumbukwa mmoja mmoja? Saana wanakumbukwa kwa wingi wao na kutupiwa ka bajaj kakubebea wazazi.hivyo wabunge ni wafalme na ni aibu umeme kukatika bungeni mpaka ma kwao.
   
 17. b

  batromayo Member

  #17
  Jul 22, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hayo ndo mafuta yake, waziri alianza kwa kuisifia serikali ya Jk na kusema wamefanikisha sera ya maisha bora ,,..,? shetani ameumbuliwa!
   
 18. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Aibu si kwa wabunge kukosa umeme ila aibu ni kutumia mshumaa, sawa na aibu ya uwanja wa taifa kutumi taa ya gari la ambulance wakati wa kukabidhi kombe. Inakuwaje bunge lisiwe na standby generator au taa ya kandili basi walau tochi kuliko kutumia mshumaa ambao ni hatari.

  Lakini kwa upande mwingine mimi naona sawa tu kwa vile bunge linaangaliwa na mataifa mbalimbali ujumbe umefika hadi kwa wafadhili wetu na investors ambao Kikwete amekwenda kuwadanganya ili waje wakijua mapema kuna tatizo la umeme.
   
 19. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,576
  Likes Received: 12,860
  Trophy Points: 280
  wacha huo umeme uwakatikie wanakazi gani zaidi ya kupigizana makelele?
  af jion wanaweka noti mifukoni wanaenda zao kujiachia chako ni chako lool
  sisi huku no power na matatizo chungumzima
  asa mnawaonea huruma kwel???????i.ingebidi bunge liendeshewe chini ya mti kwenye vumbi
  kama watoto weengi wanavyosoma kwa shida wamekaa chini , mi sioni sababu ya wao kulla
  kiyoyozi huku ahadi zao za kichina tu.
   
 20. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Kweli kaumbuka alikuwa anasema JK kafanikisha umeme hadi vijiji........kabla ya kumalizia.... 'ni'....umeme ukakatika akaomba mshumaa.
   
Loading...