Umeme umerudi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme umerudi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ground Zero, Nov 16, 2011.

 1. Ground Zero

  Ground Zero JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kutokea mlipuko kwenye mitambo ya tanesco ubungo; kumekuwa na ripoti ya kukatika kwa umeme sehemu nyingi. Je kwenu umeme umerudi?nipo ubungo , hakuna umeme.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Mtambo Tanesco waungua [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 15 November 2011 20:37 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Geofrey Nyang'oro
  Mwananchi

  MOTO mkubwa umezuka jana kwenye Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kuunguza kifaa kiitwacho ‘reactor' kinachotumika kudhibiti mfumo wa usambazaji umeme katika jiji la Dar es Salaam hali iliyosababisha jiji hilo kukosa umeme.Tukio hilo lililotokea saa 10:45 jioni, lilisababisha kukatika kwa umeme katika jiji hilo na viunga vyake huku uongozi wa ukisema haijajulikana tatizo hilo lingechukua muda gani kutatuliwa.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Sophia Mgonja aliwaambia waandishi wa habari kwamba: "Hadi sasa hatujui chanzo na wala athari zake. Umeme umekatika jiji zima na hatuwezi kurudisha hadi tutakapofanya uchunguzi kuona kiwango cha uharibifu."

  Alisema kifaa hicho kilichoungua kinachokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani 500,000 (takriban Sh 900milioni) hakitengenezeki na badala yake kinatakiwa kuagizwa kingine.

  Mgonja alisema mbali ya kifaa hicho vingine kama ‘Control Cable' pamoja na vikombe vya kwenye nguzo ambavyo vilikuwa havionekani kutokana na kufunikwa kwa moshi huenda navyo vimeteketea."Kuanzia sasa mafundi wanaanza kazi ya kuchunguza chanzo cha tukio hilo lakini pia kuona namna tunavyoweza kurudisha umeme kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam".

  Mkuu wa zamu wa Kikosi wa Kikosi cha Zimamoto wa Jiji la Dar es Salaam, Seleman Said alisema kikosi hicho kiliwasili katika eneo hilo saa 11:03 baada ya kupata taarifa saa 10:45 jioni.

  Alisema baada ya kuwasili, walielezwa kuwa kifaa hicho kina mafuta hivyo kulazimika kuchanganya maji na dawa ili kuwezesha kazi hiyo kufanywa kwa ufanisi."Kazi tuliifanya kwa muda wa dakika saba na katika muda wa dakika 20 tulikuwa tunamalizia kuhakikisha moto huo haulipuki tena," alisema Said.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. Shemzigwa

  Shemzigwa JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2011
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huku Tandika unawaka
   
 4. PROF. ENG

  PROF. ENG Senior Member

  #4
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana hawa majamaa wanalipua wenyewe makusudi!!
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Kitu kimerudi
   
 6. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  nmeamka sa nane na nusu ya usiku nmeukuta umerudi
   
 7. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  ujerudi tisa na nusu kwetu
   
 8. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  DAKIKA .15 ZILIZOPITA NDIO UMERUDI HUKU MIKOCHENI sasa najiuliza hicho kifaa ndio kimeshagizwa au walikuwa wanaandaa mazingira ya ufisadi?
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mwee ngoja nichaji simu maana usije katika tena
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  nna wasi wasi mgao unarudi tena kwa kisingizio cha hicho kifaa
   
 11. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hapa nilipo umekatika tena 0522hr.
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Nov 16, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Hicho kifaa kinatengenezwa Marekani?
   
 13. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Kuna jamaa yangu wa Mbeya anayejiandaa kuja Dar ameniambia umekatika saa 05:22Hrs...
   
 14. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #14
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Msasani umerudi 04:10 ukakatika tena 05:22 kazi ipooooo
   
 15. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwe2 hamna hadi sa hzi
   
 16. M-pesa

  M-pesa JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hapa nilipo hakuna umeme.
   
 17. n

  ngwini JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Thinza..ulirudi nane flani bt kumi na moja kushnei.
   
 18. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #18
  Nov 16, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Isijekuwa HUJUMA?
   
 19. u

  utantambua JF-Expert Member

  #19
  Nov 16, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sheria ya ununuzi vitu used itaanza kutumika hapa kununua hiyo reactor. Tutajuta
   
 20. M

  Ma Tuma Senior Member

  #20
  Nov 16, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kifaa kinapatikana ubalozi wa marekani ndio maana unapotea na kurudi,mbona rahisi tu.
   
Loading...