Umeme umekata Zanzibar nzima, je huko kwenu upo?

silent lion

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
1,161
1,540
Tujuzane Tafadhali.

Hivi kwa nn suala la umeme haliishi TZ ata aje Rais gani?

*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*

*TAARIFA YA KATIZO LA UMEME LA DHARURA*

Shirika la Umeme Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wa Zanzibar na Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa, tumelazimika kuzima kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kunduchi kuanzia Saa 4:00 Asubuhi hadi Saa 9:00 Alasiri.

*SABABU*
Kurekebisha mkondo wa "BREAKER" katika njia ya umeme ya msongo wa 132 Kunduchi- Zanzibar na kurekebisha "loose connection" katika njia ya umeme ya Ubungo- Kunduchi.

*MAENEO YANAYOATHIRIKA NI*
Zanzibar, Bagamoyo, Bunju, Madale, Kunduchi Beach, Mivumoni, Salasala, Bahari Beach, Kawe, baadhi ya maeneo ya Makongo juu, Tegeta, baadhi ya maeneo ya Mwenge, Kondo Village, Boko Magengeni, Ras Kilomoni, baadhi ya maeneo ya Boko, Masanja, Mbweni NHC Msaiti, Mbweni na maeneo jirani,

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Kwa mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook Tanesco Yetu

IMETOLEWA NA:

OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

APRILI 18, 2018
 
Huku Tanganyika upo, alafu ulivyoandika zanzibar yote basi utadhani zanzibar kuuuubwa kumbe nikama chuo kikuu cha dodoma Udom. Mtu akibisha hodo kwako pwani ya magharibi mpa watu wa pwani ya mashariki wanasikia. ukipanda juu ya mnazi pale mchamba wima unaona nchi nzima ya zanzibari. Kunajamaa alisema kuna wakati zanzibari nzima kulikatika umeme sasa yeye na kajenereta kake ka saloon akakawasha nakuchomeka kwenye soketi bila kuzima main swichi, umeme ukaingia kwenye grid ya nchi zanzibar, zanzibar nzima umeme ukawaka kwa jenereta ya salooni.
 
SAMAHANI UNATUMIA KILEVI GANI?
 
Mambosasa anakuangaliiiiiaaaa
 
Huku upo mkuu, vipi shirika la ugavi umeme la huko visiwani hawa kuwapa tahadhari mapema...,?
 
Mkuu
Huku Tanganyika upo, alafu ulivyoandika zanzibar yote basi utadhani zanzibar kuuuubwa kumbe nikama chuo kikuu cha dodoma Udom. Mtu akibisha hodo kwako pwani ya magharibi mpa watu wa pwani ya mashariki wanasikia. ukipanda juu ya mnazi pale mchamba wima unaona nchi nzima ya zanzibari. Kunajamaa alisema kuna wakati zanzibari nzima kulikatika umeme sasa yeye na kajenereta kake ka saloon akakawasha nakuchomeka kwenye soketi bila kuzima main swichi, umeme ukaingia kwenye grid ya nchi zanzibar, zanzibar nzima umeme ukawaka kwa jenereta ya salooni.

Mkuu umetisha. Tutakushusha ngiri wewe lete dharau tu
 
SAMAHANI UNATUMIA KILEVI GANI?
alcoholicdrinkssostrongtheycanknockout652x4001_1439812985_350x163.jpg
 
Tumieni mabaki ya miwa kuzalisha umeme....
shamba la miwa kubwa kuliko yote zanzibar, wanafunzi wa darasa la pili wa skuli ya jambiani wanalimaliza kwa lisaa na nusu tu, na maganda hayatoshelei hata kirikuu moja.
 
Back
Top Bottom