UMEME na Tanzania

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Nilipita katika anga za Ethiopia kuelekea Instanbul nyakati za usiku kwa kweli sikuamini nilivyoiona ni jinsi gani Nchi ya Ethiopia ilikuwa inang'ara kwa mataa ambayo unaweza kusema hawa jamaa wana utajiri mkubwa sana.

Anga ya Tanzania ni kiza kabisa huwezi kujua kama hata kama kuna taa za barabarani hapo Darisalama.

Nikilinganisha na barabara za Darisalama basi ni sehemu moja tu ambayo Taa za barabarani huwa zinawashwa ,sehemu za Mbezi ambako kila baada ya maguzo sita unaweza kubahatika kuona guzo moja lina taa na iwakayo ni ya upade mmoja nyengine labda imeungua miaka minne iliyopita.

Nilishangaa kuona Barabara ya Kawawa ambayo ni dual haiwaki taa hata moja na na njia nyengine ambazo ni kuu hazina hata guzo na kama yako utafikiri ni miti iliyopitiwa na kimbunga kila mmoja umelalia upande wake ,kwa kweli ni aibu kubwa sana sana.

Ukienda mitaani ndio kabisa utafikiri unatembea kwenye msitu wenye giza nene na taa uzionazo ni kama vile wale wadudu waitwao vimulimuli.
Ukiangalia kwa kina ndio utagundua kuwa tatizo hili la kukosekana kwa taa barabarani ndilo linalozalisha vibaka,madereva kugonga na kukimbia na ubakaji holela japo mchana matukio hayo hutokea lakini ni kwa nadra sana.
Sijui mikoa mingine ikoje ,Mtwara haijambo wao wanatumia umeme wa gesi ila taa za barabarani sijaziona !!! Pia kuna fununu za ukiritimba na ulaji katika mradi huo !?!.

Hivi tatizo hili ni nani wa kulaumiwa ,je ni meya wa mji ,waziri au Raisi ?
Kwa kweli ni aibu kwa jiji kama la Dar kukosa taa za uhakika katika barabara kuu na hata zile za mitaa.
Nani wa kulaumiwa ?
 
Last edited:
Back
Top Bottom