Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 19,147
- 43,079
Huwezi kuvaa nguo fulani sababu hawatakuelewa.
Huwezi kuishi mtaa fulani watakuona maskini sana au tajiri sana.
Huwezi kula pale kwasababu siyo hadhi yako.
Huwezi kuoa au kuolewa na mtu fulani siyo hadhi yako.
Huwezi kufanya kazi fulani sababu utaonekana umefeli kimaisha.
Huwezi kutumia simu aina fulani kwasababu za kitajiri sana au za kimaskini sana.
Huwezi kwenda beach wewe siyo mshamba wa maji.
Huwezi kwenda baa kukaa ukala au ukanywa wewe siyo malaya.
Hawezi kuwa rafiki yangu yule hana cha kunisaidia.
Umejiwekea sheria nyingi na kanuni nyingi za maisha yako ndiyo maana upo gerezani,upo katika kundi la wafungwa wanaotumikia kifungo cha nje. Upo kwenye shimo lako ulilojichimbia.
Umejawa na upweke,ukimya,huna marafiki wala ndugu,huna wa kwenda kumtembelea mkakaa wote siku nzima.
Umechagua kujitesa mwenyewe ndiyo maana unakasirika na kuchukia ukiona mlevi njiani.
Unakasirika ukiona watu wazima wanacheza mziki kwenye sherehe au baa au kwenye halaiki.
Ukisikia mtu katumia hela nyingi kwa ajili ya sherehe ya mwanae unaona hana akili.
Ukiona mtu anajenga nyumba kubwa unauliza sasa nyumba yote hii kubwa kwa ajili ya nani?
Toa hizo sheria na kanuni ulizojiwekea kuwa huru maisha ni mafupi sana furahia kila pumzi ya uhuru wako.