Umejifunza nini kwenye uteuzi wa wagombea CCM?

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
464
Reaction score
687
Jana Halmashauri kuu ya CCM, imefanya uteuzi wa wagombea ubunge Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania na uwakilishi katika Baraza la wawakilishi Zanzibar. Naungana na wanachama wenzangu wa CCM kumpongeza mwenyekiti, kamati kuu, halmashauri kuu na wagombea wote walioteuliwa.

Baada ya mchakato huu kumalizika, kama vijana tumejifunza nini? Hili ni swali muhimu sana haswa kwa wale wenye mipango ya kushiriki siasa za kugombea na kuteuliwa siku moja. Tathmini yangu ya uteuzi wa wagombea imenifundisha yafuatayo:

1. CCM haivumilii wasaliti wa ndani.
Ndugu January Makamba, Ummy Mwalimu, Luhaga Mpina, Ole Sendeka, Fred Lowassa hawa walisemwa semwa sana kumhujumu Mwenyekiti kwenye uteuzi wake na mgogoro wa ngorongoro. Kutokuteuliwa kwao kunatoa ujumbe muhimu sana, katika CCM, Mwenyekiti hajaribiwi.

2. Mwana mpotevu, akirudi CCM tutamkaribisha.
Esta Bulaya na wenzake walitoka CDM, hawakufanya vizuri kura za maoni. Ingawa uteuzi wao umelalamikiwa na baadhi ya makada kama Shayrose Banji, lakini umetoa ujumbe muhimu kwa wapinzani, CCM inawakaribisha tujenge pamoja.

3. Wasanii wana nafasi CCM
Kama ilivyokuwa kwa mwana FA 2020, Baba Levo ameteuliwa ingawa hakushinda kura za maoni. Ujumbe uliokusudiwa hapa ni mmoja, wasanii, mkikiunga mkono chama hakitawaangusha.

4. Ukitaka ubunge, ishi vizuri na wajumbe.
Ukiacha hayo niliyoyataja hapo juu, wagombea wote waliongoza kura za maoni, wameteuliwa kuwa wagombea. Hii maana yake ni nini? Ukitaka ubunge, ishi vizuri na wajumbe.

Hii ni tathmini yangu inayotoa mwelekeo wa nini vijana wanaotaka kushiriki siasa za nchi yao kupitia CCM wafanye kuzifikia ndoto zao.
 
Hakuna lolote, hapa la kujifunza ni kwamba demokrasia ya vyama vingi ikifa basi hakuna mwanachama wa CCM mwenye mawazo kinzani ja mwenyekiti wake atapona.

Kama kungekua na tume huru na uwanja sawa wa kufanya siasa lazima CCM ingesikiliza wananchi maana inajua ikiwakata watu muhimu basi jimbo automatically litaenda upinzani.

Ila kwa sasa hawana hofu hiyo maana wameshaua chaguzi huru na siasa huru hivyo tutarajie bunge la 2025-30 kujaa machawa tu maana wakikosoa tu wataliwa kichwa 2030.

Uwajibikaji ndio umekufa rasmi
 
Majority ya walioteuliwa ni walioshinda kura za maoni
Elewa ulichoambiwa, umeuliza tumejifunza nini, mdau amekuambia amejifunza >> "your vote doesn't count."
we unasema majority, kwani minorities hawana haki wanapo pigiwa kura za ushindi na wajumbe?.
 
Jana Halmashauri kuu ya CCM, imefanya uteuzi wa wagombea ubunge Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania na uwakilishi katika Baraza la wawakilishi Zanzibar. Naungana na wanachama wenzangu wa CCM kumpongeza mwenyekiti, kamati kuu, halmashauri kuu na wagombea wote walioteuliwa.

Baada ya mchakato huu kumalizika, kama vijana tumejifunza nini? Hili ni swali muhimu sana haswa kwa wale wenye mipango ya kushiriki siasa za kugombea na kuteuliwa siku moja. Tathmini yangu ya uteuzi wa wagombea imenifundisha yafuatayo:

1. CCM haivumilii wasaliti wa ndani.
Ndugu January Makamba, Ummy Mwalimu, Luhaga Mpina, Ole Sendeka, Fred Lowassa hawa walisemwa semwa sana kumhujumu Mwenyekiti kwenye uteuzi wake na mgogoro wa ngorongoro. Kutokuteuliwa kwao kunatoa ujumbe muhimu sana, katika CCM, Mwenyekiti hajaribiwi.

2. Mwana mpotevu, akirudi CCM tutamkaribisha.
Esta Bulaya na wenzake walitoka CDM, hawakufanya vizuri kura za maoni. Ingawa uteuzi wao umelalamikiwa na baadhi ya makada kama Shayrose Banji, lakini umetoa ujumbe muhimu kwa wapinzani, CCM inawakaribisha tujenge pamoja.

3. Wasanii wana nafasi CCM
Kama ilivyokuwa kwa mwana FA 2020, Baba Levo ameteuliwa ingawa hakushinda kura za maoni. Ujumbe uliokusudiwa hapa ni mmoja, wasanii, mkikiunga mkono chama hakitawaangusha.

4. Ukitaka ubunge, ishi vizuri na wajumbe.
Ukiacha hayo niliyoyataja hapo juu, wagombea wote waliongoza kura za maoni, wameteuliwa kuwa wagombea. Hii maana yake ni nini? Ukitaka ubunge, ishi vizuri na wajumbe.

Hii ni tathmini yangu inayotoa mwelekeo wa nini vijana wanaotaka kushiriki siasa za nchi yao kupitia CCM wafanye kuzifikia ndoto zao.
Serikali inaamua nani apewe kazi ya kuisimamia!
 
siasa ni shughuli ngumu sana katika ulimwengu huu unaoweka chawa mbele kuliko wenye uwezo halisi wa kufanya mapinduzi ya fikra
 
Jana Halmashauri kuu ya CCM, imefanya uteuzi wa wagombea ubunge Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania na uwakilishi katika Baraza la wawakilishi Zanzibar. Naungana na wanachama wenzangu wa CCM kumpongeza mwenyekiti, kamati kuu, halmashauri kuu na wagombea wote walioteuliwa.

Baada ya mchakato huu kumalizika, kama vijana tumejifunza nini? Hili ni swali muhimu sana haswa kwa wale wenye mipango ya kushiriki siasa za kugombea na kuteuliwa siku moja. Tathmini yangu ya uteuzi wa wagombea imenifundisha yafuatayo:

1. CCM haivumilii wasaliti wa ndani.
Ndugu January Makamba, Ummy Mwalimu, Luhaga Mpina, Ole Sendeka, Fred Lowassa hawa walisemwa semwa sana kumhujumu Mwenyekiti kwenye uteuzi wake na mgogoro wa ngorongoro. Kutokuteuliwa kwao kunatoa ujumbe muhimu sana, katika CCM, Mwenyekiti hajaribiwi.

2. Mwana mpotevu, akirudi CCM tutamkaribisha.
Esta Bulaya na wenzake walitoka CDM, hawakufanya vizuri kura za maoni. Ingawa uteuzi wao umelalamikiwa na baadhi ya makada kama Shayrose Banji, lakini umetoa ujumbe muhimu kwa wapinzani, CCM inawakaribisha tujenge pamoja.

3. Wasanii wana nafasi CCM
Kama ilivyokuwa kwa mwana FA 2020, Baba Levo ameteuliwa ingawa hakushinda kura za maoni. Ujumbe uliokusudiwa hapa ni mmoja, wasanii, mkikiunga mkono chama hakitawaangusha.

4. Ukitaka ubunge, ishi vizuri na wajumbe.
Ukiacha hayo niliyoyataja hapo juu, wagombea wote waliongoza kura za maoni, wameteuliwa kuwa wagombea. Hii maana yake ni nini? Ukitaka ubunge, ishi vizuri na wajumbe.

Hii ni tathmini yangu inayotoa mwelekeo wa nini vijana wanaotaka kushiriki siasa za nchi yao kupitia CCM wafanye kuzifikia ndoto zao.
Nimejifunza Sani Abacha wa Tanzania Luteni Kanali Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete anapanga safu yake vizuri sana ili mwanae Ridhiwani Kikwete awe Rais wa Tanzania mwaka 2030
 
Kwa tathmini yangu, hitimisho ni kwamba maoni ya wajumbe hayana thamani kama tu zilivyo kura za wananchi. Wajumbe waliamua walivyoamua, kamati kuu ikafanya vingine kwa baadhi.

Vivyo hivyo, kupiga kura ni haki ya kila mwananchi aliyefikia umri wa kupiga kura lakini kura yako haiamui nani awe rais, mbunge au diwani. Kuna mifumo iliyounganishwa (NIDA, INEC, na CCM) ambayo matokeo yake ni kuwa hata sasa mshindi wa uchaguzi wa October 2025 anatabirika.

Wameshatiki!
 
Nimejifunza Sani Abacha wa Tanzania Luteni Kanali Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete anapanga safu yake vizuri sana ili mwanae Ridhiwani Kikwete awe Rais wa Tanzania mwaka 2030
Duh! Mengine tusimzushie mzee wa watu.
 
Back
Top Bottom