Umefanya Wema gani ukakutokea puani?(ukakuponza) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umefanya Wema gani ukakutokea puani?(ukakuponza)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Zion Daughter, Jun 3, 2010.

 1. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ngoja nianze na salamu,
  Wakubwa ....shikamoo!!!
  Tulio sawa......Mambo!!!!
  Wadogo.......Hamjambo!!!!

  Jana jioni wakati najiandaa kurudi nyumbani nilikuwa napiga story nje ya ofisi.Ghafla kijana mmoja aliyekuwa anapita mbele ya ofisi alianguka na akaanza kujikakamaza na kung'ata ulimi.Mama mmoja akamkimbilia na kumpachika ndala mdomoni.Baada ya dakika kama 5 akawa karudi kwenye hali ya kawaida.Katika kumuhoji alidai kuwa alitoka sehemu za Tanga na alileta korosho asubuhi kwa ajili ya kuuza.Lakin bahati mbaya ile hali(kifafa) ilimtokea na akawa kaibiwa pesa zote.Alienda polisi na hakupata msaada na alidai kila anayemueleza alikuwa hamuelewi.Basi mie nikawa nimefikia uamuzi wa kumbeba kwa gari hadi ubungo nimpakize kwenye mabasi.Akawa amekubali bila tatizo.Lakin mara wafanyakazi wenzangu wakaanza kunitahadharisha kuwa nisithubutu kumpeleka kwa gari bora nimpe nauli kwani naweza kujikuta matatani incase jambo lolote likitokea.Nilikubaliana nao lakini nikawaambia tuchange basi tumpe nauli,hapo tena watu wakageuka na kusema eti anaweza kuwa tapeli na hawako tayari.Niliamua kumpa nauli ili akapande gari mwenyewe kwa vile nilijiuliza what if akawa na shida kweli? ila mpaka sasa bado kuna vimawazo vinaniambia kuwa labda nilitapeliwa(huwa sipendi kufanywa mjinga).

  Ningependa wadau nipate Experience zenu kwenye issue kama hizi zilizowahi kuwatokea kwa kutenda wema au kutoa msaada wowote.
  Nawakilisha.
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,045
  Likes Received: 24,043
  Trophy Points: 280
  Charity mchumba,

  Unapoamua kufanya jambo ambalo unaamini ni sahihi, usirudi nyuma na kuanza kulikumbuka.
  Tenda wema uende zako, usingoje shukrani.
  kama alikuwa tapeli nia na lengo lako la kusaidia halijaharibika. Atajua yeye na Mungu wake.
  Vinginevyo, kama umemsaidia mtu halafu moyoni ukawa huna amani, basi hata mbele ya Mwenyezi Mungu hutapata thawabu.

  Siku nyingine huwa nakuwa na busara, sijui kwanini?
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  charity umefanya jambo jema wala huna haja ya kuanza kufikiri kama yule alikuwa tapeli au la!

  as long as unaamini Mungu, basi wewe amini kuwa wema wako utalipwa kwako na yeye muweza hata kama ulitapeliwa
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Utapata thawabu mbele za mungu Charity..
  Tena tusichoke kuyatenda mema kwani tutavuna kwa wakati wake tusipozimia mioyo.
   
 5. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Sobriety
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,045
  Likes Received: 24,043
  Trophy Points: 280
  Milele Amina Baba Askofu.

  Naomba baraka zako..........
   
 7. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Marahaba Charity,

  Watu wengi sana wana-abuse huruma za watu siku hizi... mtu anasingizia kidonda, kifafa na vitu kibao ili mradi apate pesa, mwisho wa siku unakutana naye kashapata wanzuki yuko chakari na matusi kibao...

  Lakini unapoamua kutenda wema na kumsaidia mtu, usijifikirie, mpe kwa moyo mkunjufu na Mungu wetu aonaye sirini atakujazi, ila kama anadanganya... adhabu yake anaijua Mungu
   
 8. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Endelea hivyo hivyo mwanangu.... Mungu atakusaidia
   
 9. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Ondoa pia hiyo Glesi, inaweza kukupa hamasa hata ya kuinusa ili upate japo harufu
   
 10. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,045
  Likes Received: 24,043
  Trophy Points: 280
  Askofu naona unaanza kwenda nje ya mipaka ya mahubiri yako.

  Siasa na dini sawa na mafuta na maji....
   
 11. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Eeh... kumbe hii ni Politiki... Sore...:confused2::disapointed:
   
 12. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Samahani nimejibu salamu zote kwa sababu sijui nipo kundi gani kutokana na eji yako.. Hivi una miaka mingapi vile?
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,045
  Likes Received: 24,043
  Trophy Points: 280
  Sasa turudi kwenye mada.....

  Hivi ukininunulia bia tatu ukaishia zako nami nikampa moja baameidi itakuuma au?
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  weee charity hivi huyo kijana alikuwa ni HE?....au SHE?
   
 15. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tenda wema nenda zako....

  Ninazo experince nyingi sana za kutenda wema na kuondoka zangu...

  Kuna hii mmoja:

  Nimerudi nyumbani mapema saa 10jioni, mara nasikia kelele kwa jirani, mke wangu na mimi tunaendelea kuangalia kulikoni.
  Tunapisha geti tunafunguliwa, ndani tunakuta mtoto mkubwa wa jirani anagalala chini, mapovu yanamtoka, anaonekana kama
  bado robo saa akate kauli.

  Nawasha gari, tunampakia huyo mtoto na kumkimbiza hospitali - Mimi na mke wangu. Hospitali wanampima wanasema ana-complications
  nyingi - malaria inakaribia celebral na sukari, damu, vimepungua sana, presha ipo chini. Anapatiwa first-aid na tunakuwa refered kwenye
  hospitali kubwa zaidi.

  Hiyo hospitali kubwa nakuwa attended vizuri na kama yapata saa mbili ana-rudi kwenye hali ya auweni. Unfortunately mairani wa Bongo ni kama Ulaya - hatuna hata simu za wenye mtoto na hata jina la mtoto tumetumia "mtoto wa jirani"! Namuacha mke wangu anamuangalia nakimbia nyumbani kuangalia kama majirani wamerudi na kuwapa taarifa nini kinaendelea au kimeendelea. Saa nne usiku bado hawajarudi.

  Nafanikiwa kupata namba zao za simu, nampigia mama mtoto, nampa habari ya kilichojiri. Anasema yupo na mme wake na wanakuja mara moja. Nawaachia na namba yangu na pia nawapa na ya mke wangu, in case wakiwa kufika hospital. Napitia nyumbani kuangalia usalama wa familia yangu, halafu narudi hospital. Njiani napitia baa moja maarufu hapa Dar maeneo ya Mikocheni, kupoza koo, ya kwanza, ya pili, ya tatu, mke wangu ananipigia simu, ni saa tano hivi bado wazazi wa mtoto hawajafika hospitali!

  Nasogea pembeni kidogo, nawapigia tena simu, mara inapokelewa, nawaambia kulikoni, wanajibu, kuwa watafika in 30min. Hii sehemu wanapopokelea simu ni kama baa - kuna ukelele fulani - Nakata simu namalizia kinywaji. Nakimbia hospitali, mke wangu anarudi nyumbani mimi nabaki na mtoto.

  Yapata saa sita wazazi wanaingia, nawapa taarifa, nawatambulisha kwa Madaktari na wauguzi. Nakaa kidogo naaga.

  Ile nataka kutoka wodini, Baba mtoto ananiita kando, anaiuliza, kwa nini nimemleta mtoto wao kwenye hospita ya daraja la pili?

  Natabasamu, naingia kwenye ki-gari changu narudi ile baa naongeza mbili (maan ilo swali liliniondolea stimu) yapata saa 7 nafika home.

  Sijawahi kuongea na hao majirani tangia nilipoondoka wodini yapata mwezi sasa - mtoto alipona nashukuru Mungu.
   
 16. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
   
 17. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hahahahaha!
  NOTED WITH MANY THANKS...(hata kama ulitutenga wengine,lakini POA TU)
   
 18. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Haitaniuma Xpin... lakini naomba nikuulize swali, unampa kwa roho safi au unategemea something kutoka kwake in return?
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  halafu we baba askofu weweeeeee.....!
  piijei umempeleka motoni au KUZIMU?mbona hapatikani?
   
 20. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Pole kaka...ila hao majirani wako hawana hata haya machoni wakikuona????mijitu mingine bwana wacha tu!
   
Loading...