Umefanya Wema gani ukakutokea puani?(ukakuponza)

Umefanya Wema gani ukakutokea puani?(ukakuponza)

Matapeli Wanafanya Hata Wenye Xhda Kwel Wacpate Mxaada Kuna M2 Tuliwah Kump Mxaada Akawa Anakaa Chuch Anapewa Hela Ya Kula Deile Akiwa Chach Anaxoma Bible Kinoma Cku Anaxepa Alibeba Cm Ya M2 Na Kuja Kufatilia Alikua Mwiz Knma

king suleman, hii ni forum ya watu wanaojielewa, huku hatutumii maneno kama m2, mxaada, xhida, anaxepa nk.

Jaribu kujifunza kuandika lugha nzuri, enzi kiswahili chako.
 
king suleman, hii ni forum ya watu wanaojielewa, huku hatutumii maneno kama m2, mxaada, xhida, anaxepa nk.

Jaribu kujifunza kuandika lugha nzuri, enzi kiswahili chako.
Bora hata wewe umemsoma. Mimi sijui hata kaandika nini . naona X 2 .
Namshauri afuate ushauri uliompatia

Sent from my IPhone 7 plus by using JamiiForums mobile app
 
Nimeitumikia serikali yangu kwa miaka 40 kwa kufanya kazi kwa bidiii na kujitoa NIKIWA NA CHETI CHANGU FAKE lakini matokeo yake wamenifukuza kama "nyau"
 
Charity mchumba,

Unapoamua kufanya jambo ambalo unaamini ni sahihi, usirudi nyuma na kuanza kulikumbuka.
Tenda wema uende zako, usingoje shukrani.
kama alikuwa tapeli nia na lengo lako la kusaidia halijaharibika. Atajua yeye na Mungu wake.
Vinginevyo, kama umemsaidia mtu halafu moyoni ukawa huna amani, basi hata mbele ya Mwenyezi Mungu hutapata thawabu.

Siku nyingine huwa nakuwa na busara, sijui kwanini?
unakuwa bado hujapata kilaji
 
Nimeitumikia serikali yangu kwa miaka 40 kwa kufanya kazi kwa bidiii na kujitoa NIKIWA NA CHETI CHANGU FAKE lakini matokeo yake wamenifukuza kama "nyau"
Hiyo miaka 40 ya kuzaliwa bado hujafikisha, unaweza kuitumikiaje serikali miaka 40 [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Tenda wema nenda zako....

Ninazo experince nyingi sana za kutenda wema na kuondoka zangu...

Kuna hii mmoja:

Nimerudi nyumbani mapema saa 10jioni, mara nasikia kelele kwa jirani, mke wangu na mimi tunaendelea kuangalia kulikoni.
Tunapisha geti tunafunguliwa, ndani tunakuta mtoto mkubwa wa jirani anagalala chini, mapovu yanamtoka, anaonekana kama
bado robo saa akate kauli.

Nawasha gari, tunampakia huyo mtoto na kumkimbiza hospitali - Mimi na mke wangu. Hospitali wanampima wanasema ana-complications
nyingi - malaria inakaribia celebral na sukari, damu, vimepungua sana, presha ipo chini. Anapatiwa first-aid na tunakuwa refered kwenye
hospitali kubwa zaidi.

Hiyo hospitali kubwa nakuwa attended vizuri na kama yapata saa mbili ana-rudi kwenye hali ya auweni. Unfortunately mairani wa Bongo ni kama Ulaya - hatuna hata simu za wenye mtoto na hata jina la mtoto tumetumia "mtoto wa jirani"! Namuacha mke wangu anamuangalia nakimbia nyumbani kuangalia kama majirani wamerudi na kuwapa taarifa nini kinaendelea au kimeendelea. Saa nne usiku bado hawajarudi.

Nafanikiwa kupata namba zao za simu, nampigia mama mtoto, nampa habari ya kilichojiri. Anasema yupo na mme wake na wanakuja mara moja. Nawaachia na namba yangu na pia nawapa na ya mke wangu, in case wakiwa kufika hospital. Napitia nyumbani kuangalia usalama wa familia yangu, halafu narudi hospital. Njiani napitia baa moja maarufu hapa Dar maeneo ya Mikocheni, kupoza koo, ya kwanza, ya pili, ya tatu, mke wangu ananipigia simu, ni saa tano hivi bado wazazi wa mtoto hawajafika hospitali!

Nasogea pembeni kidogo, nawapigia tena simu, mara inapokelewa, nawaambia kulikoni, wanajibu, kuwa watafika in 30min. Hii sehemu wanapopokelea simu ni kama baa - kuna ukelele fulani - Nakata simu namalizia kinywaji. Nakimbia hospitali, mke wangu anarudi nyumbani mimi nabaki na mtoto.

Yapata saa sita wazazi wanaingia, nawapa taarifa, nawatambulisha kwa Madaktari na wauguzi. Nakaa kidogo naaga.

Ile nataka kutoka wodini, Baba mtoto ananiita kando, anaiuliza, kwa nini nimemleta mtoto wao kwenye hospita ya daraja la pili?

Natabasamu, naingia kwenye ki-gari changu narudi ile baa naongeza mbili (maan ilo swali liliniondolea stimu) yapata saa 7 nafika home.

Sijawahi kuongea na hao majirani tangia nilipoondoka wodini yapata mwezi sasa - mtoto alipona nashukuru Mungu.
mkuu bora ujaongea nao maana ungeweza kuwatolea maneno mazito
 
Nilimpeleka kwao mtoto aliepotea, kutokana na stress mtoto alivyoona wazazi wake akaanza kulia, kwa kuwa wazazi hawakujua kama mtoto wao alipotea wakadhani kulia kule kumetokana na kupigwa na mimi, yaliyonikuta baada ya hapo kilikua kipigo kwangu

Sent from my MHA-L29 using JamiiForums mobile app
 
Matapeli Wanafanya Hata Wenye Xhda Kwel Wacpate Mxaada Kuna M2 Tuliwah Kump Mxaada Akawa Anakaa Chuch Anapewa Hela Ya Kula Deile Akiwa Chach Anaxoma Bible Kinoma Cku Anaxepa Alibeba Cm Ya M2 Na Kuja Kufatilia Alikua Mwiz Knma
Shida ni nini ndugu? Kitu gani umeandika hapo?
 
Back
Top Bottom