Umedanganywa Kuolewa?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umedanganywa Kuolewa??

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by ngoshwe, Dec 8, 2009.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Je, aliyedanganywa ndoa ana haki ya kudai fidia????

  Kama ilivyo kwa Sheria za mikataba ambapo mtu anayetoa ahadi anapaswa kutekeleza, sheria ya ndoa pia inamtaka mtu anayetoa ahadi ya ndoa kutekeleza ahadi yake vinginevyo anaweza kudaiwa fidia kwa kuvunja ahadi ya ndoa.

  Mtu aliyedanganywa ndoa (kuoa au kuolewa) anayo haki kisheria ya kudai fidia dhidi ya udanganyifu aliyofanyiwa.

  Sheria ya Ndoa ya Tanzania inasema:

  “ A suit may be brought for damages for the breach of a promise of marriage made in Tanganyika (……) whether the breach occurred in Tanganyika or elsewhere, by the aggrieved party or, where that party is below the age of eighteen years, by his or her parent or guardian.

  Ikumbukwe pia kuwa:

  • Madai ya fidia ya kudanganywa ndoa hayamhusu mtua ambaye wakati alipoahidiwa alikuwa chini ya miaka kumi na nane (below the age of eighteen years). Kisheria mtu aliye chini ya miaka kumi na nane haruhusiwi kuingia kwenye mkataba isipokuwa kwa mikataba ya mahitaji ya lazima (necessaries) .
  • Fidia itakayotolewa na Mahakama haitazidi kiwango halisi ambacho mdai atakuwa amegharimika kutokana na kuamini kwenye ahadi iliyovunjika (loss actually suffered as a result of expenditure incurred as a direct result of the promise)
  • Madai ya jinsi hii pia hayapaswi kuwa ya kumlazimisha mtu aliyevunja ahadi ya ndoa kutekeleze ahadi hiyo ( specific performance).
  • Madai ya jinsi hii yanapaswa kuwasilishwa Mahakamani katika kipindi kisichozidi miaka miwili tokea kuvunjika kwa ahadi na sio vinginevyo.
  Aidha, ni vizuri ikawekwa wazi hapa kuwa shauri lolote linalofikishwa Mahakamani linahitaji ushahidi wa kutosha ili kuiwezesha Mahakama kutenda haki. Hivyo jambo la msingi ni kuwa na ushaiudi wa kutosha kuthibitisha kuwepo kwa ahadi ambayo itaonekana ina sura ya kisheria.
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kuna ulazima wa madai kuwa ya maandishi? vipi kuhusu level ya ushahidi? ushahidi wa kutosha ni ushahidi gani

  Mana itakuwaje kama Mwajuma atataka kukukomoa kwa sababu unamwacha na kukufungulia kesi kwamba uliahidi kumuoa kwa maneno wakati hukuahidi?

  Mwajuma akileta rafiki zake watatu kama yeye wakisema walikusikia ukisema siku ya Iddi huo utakuwa ushahidi wa kutosha? Vipi kama na wewe utaleta rafiki zako watatu watakaosema siku ya Iddi hukuwa na Mwajuma ila ulikuwa na Mwanahamisi Tabata? Watakubaliwa kama ushahidi wa kutosha?.

  Pleeeeeease!
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Bluray,


  Kwa kawaida mahakama kama chombo cha serikali kinachosimamia haki kina utaratibu wake wa kupokea na kuchambua kisha kujua ushahiDi wa ukweli na ule wa kuzusha au kufundishwa ili kudanganya!.

  Katika hili, mtu anayedai kuwepo kwa makubaliano ya ndoa, sio lazima athibitishe kwa maandishi makubaliano hayo, hasha!. kwa mfumo wa kanuni za sheria za ushahidi, labda kama itakuwa vinginevyo, ushahidi wowote ili uweze kukubalika Mahakamani unapaswa kuwa wa maneno au kutolewa kwa mdomo (oral evidence). Kanuni hii inatambulikia kitaalamu kama "principle of orality" inayotaka mtoa ushahidi awe ni yule anayefahamu kwa kuona yale unayoyasema na sio kwa kusikia au kuambiwa na mtu mwingine (hearsay).


  Pia, tofauti na kesi za jinai ambazo upande wa mashtaka unabeba mzigo mkubwa kwa kuthibitisha kosa la mtuhumiwa pasipo kuacha mashaka (proof beyond reasonable doubt), kanuni kuu inayosimamia ushahidi katika kesi zote za madai inataka upande unaodai au kukanusha madai kuithibitisha mahakama kwa misingi ya kuondoa "walakini" (prove on balance of probabilty) kuwa yale yanayosemwa ni kweli tupu na sio vinginevyo!.


  Katika shauri linalohusu ahadi ya ndoa, miongoni mwa vigezo vya msingi ambavyo mdai atapaswa kuthibitisha ni pamoja na kuwepo kwa taratibu halali ambazo zilimfanya aamini kuwa ndoa itakuwepo (KWA MFANO, UCHUMBA, KUTOLeWA AU KUTOA MAHARI, KWENDA KANISANI au bomani KUANDIKISHA NDOA, ndoa KUTANGAzwa, KUFANYA MAFUNDISHO YA NDOA, vikao VYA HARUSI NK NK). Katika hili, Mahakama itaangalia pia iwapo taratibu hizi ndizo zinazofutwa kwenye jamii husika kuhalalisha ndoa??.
  !.


  Idadi ya mashahidi sio kigezo cha kushida shauri mahakamani, pengine ndo inaweza kukuharibia kesi yako.
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  OK,

  Vipi kama nilitaka kuoa, na nikatoa kauli kwamba nataka kuoa, lakini katika kipindi cha uchumba, au hata siku ya arusi, nikagundua kwamba huyu mwanamke si wife material.Mimi sikudanganya na wala sikuwa na nia mbaya, ila nimepata information mpya au simply nimebadilisha mawazo kuhusu kuoa (ever heard of cold feet or getting the marriage creeps?), sitaki kuoa tena, lakini sijawahi kudanganya kwa kudhamiria na wala sidanganyi, nabadilisha mawazo tu. Hizi sheria zinataka kunichukulia uhuru wangu wa kubadilisha mawazo?

  Hapo mtanifanyaje? Mtahakikishaje kwamba kubadili mawazo hapa ni kudanganya na hapa ni mtu ameamua kubadili mawazo.

  Hizi sheria si za kitalibani zitakazomuondolea mtu hata uhuru wa kubadilisha mawazo? Watu wanabadilisha mawazo hata dakika ya mwisho na sijawahi kusikia wakiletewa mashtaka.

  Ina maana mnataka kuuchukua uhuru wa mtu kubadilisha mawazo altareni? Mbona hata kanisa linatambua kwamba mtu ana uhuru wa kubadili mawazo hata dakika ya mwisho na ndiyo maana hata padre anayefungisha ndoa huuliza maharusi hata dakika ya mwisho wakiwa altareni?

  Kama ndoa inaweza kuvunjwa baada ya kufungwa kwa talaka, kwa nini mipango ya kufunga ndoa isiweze kuahirishwa wakati wowote kabla ya ndoa?

  This does not make sense and goes against my libertarian strains, not that I would ever dream of getting married but the precedent set here is dangerous.

  Tukianza na kulazimishana ndoa, whats next? Tutalazimisha watu wote waliojiandikisha kupiga kura wapige kura? Whats the difference?
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Mzee, haya yote ni masuala ya ushahidi. kudanganya na kughairi ni vitu viwili tofauti. kama uliahidi ndoa na badae kugundua haiwezekanai ni hoja za kiushahidi zaidi kuithibitishia mahakama kwa kuondoa walakini kuwa kughairi kwako kulitokana na sababu za msingi!.
   
Loading...