Bidada mmoja ilikuwa mara yake ya kwanza kwenda Ughaibuni, amepanda KLM, katika siti za pembeni tatu yeye alikaa mwanzo, dada mwingine mmbongo katikati mwisho mzungu. Yule mzungu alikula kila alicholetewa na pombe aliagiza. Hawa wadada wakateta "tujiandae akiuachia, huyu mtu anakula kila kinacholetwa". Mzungu alikaa kimya, wamefika Amsterdam ndio anawauliza mnelekea wapi? Kwahiyo inabidi mbadilishe ndege? Madada nyuso kama kijiko cha chai.