Umdhaniaye sie kumbe ndiye

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
21,410
2,000
Wanajamvi, poleni tena na mihangaiko.

Ni hivi katika shughuli zangu za stendi leo nimekutana na hii, nilikuwa na rafiki yangu tunaongozana tukakuta mzungu kasimama kituoni, yule mzungu kwa kweli alikuwa ana pua ndefu tena nyembamba.

Sasa mimi nikamwambia yule rafiki yangu kwa kilugha, (huyu mzungu ana pua ndefu sijui anakunywaje chai kwenye kikombe) tukajikuta tunacheka, kumbe yule mzungu ile lugha yetu anaijua, yeye akatujibu kwa kilugha yetu nyie mlitaka iwe kama za kwenu?

Nikabidi nianze kumwomba msamaha.

Ushauri wangu fikiri kwanza kabla ya kutenda.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,492
2,000
Niliingia dukani na rafiki ughaibuni.... hapo mwenye duka ni mzee , nikatoka kwa kusema huyu mzee vitu vyake ni ghali sana... duuh kumbe mzee lugha imetulia.. akakomalia "tafadhali chukua bila malipo"
Bidada mmoja ilikuwa mara yake ya kwanza kwenda Ughaibuni, amepanda KLM, katika siti za pembeni tatu yeye alikaa mwanzo, dada mwingine mmbongo katikati mwisho mzungu. Yule mzungu alikula kila alicholetewa na pombe aliagiza. Hawa wadada wakateta "tujiandae akiuachia, huyu mtu anakula kila kinacholetwa". Mzungu alikaa kimya, wamefika Amsterdam ndio anawauliza mnelekea wapi? Kwahiyo inabidi mbadilishe ndege? Madada nyuso kama kijiko cha chai.
 
chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
3,167

Nimecheka kwenye kuuachia.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom